Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Umeona ni point sana hii lakini nikukumbushe, fuatilia elimu ilivyo yaani shule na watu gani wanakazania zaidi, shule zipi ni bora zaidi, jamii gani ya watu inakazania zaidi 'ilmu dunia' hata ukanda au makabila gani yanakazania zaidi kusoma hiyo itakupa majimu kwa grassroot ndiyo msingi unaosimasha mafanikio katika elimu hence watu kuwa na chances zaidi kuongoza sectors muhimu.
That link ukiwa shallow minded utaitafsiri kama ambavyo unalenga wewe but it don't mean shit, angalia wahamiaji wa Kichina na Kihindi katika nchi za Magharibi wanavyofanya vizuri professionally lakini hawako katika uongozi kwenye sectors za elimu.
Cheap excuses mkiziendekeza mtaishia kulalamika miaka nenda rudi.
 
Umenikumbusha uchaguzi wa 2010 nipo mwaka wa wisho UDSM aisee lilipigwa zengwe la dini balaa yani Jumapili watu wakirudi church story ni ubaya wa JK tu na uzuri wa Slaa kwa mrengo wa kidini, waraka juu ya waraka i was to vote Slaa ila kwa mashambulizi ya dhulma yalivyozidi kwa JK nami nikasema wacha tu nimpe muislam mwenzangu maana hawa watu washaharibiwa na privilege yani wanaona waislam hatustahili chochote sasa kama mbwai iwe mbwai tu. KIukweli kwa mtu huru na usie nafikra hizi inaumiza sana.
Kuna Taasisi inaratibu hizo chuki .
Ndo maana unaona Dr Slaa sasa taratibu anatoka CCM kurudi Chadema kuongeza nguvu...
Dr Slaa alikuwa katibu zamani wa Taasisi husika
 
Monster,
Naamini kabisa kuwa hujui historia ya Waislam katika kuitafuta elimu toka wakati Tanganyika iko chini ya ukoloni.

Baada ya uhuru kupatikana 1961 mwaka wa 1962 Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin chini ya mwamvuli wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) aliitisha Muslim Congress kujadili suala la elimu kwa Waislam.

Katika mkutano huu Sheikh Hassan bin Ameir alisema kuwa uhuru tulioupigania Waislam kwa nguvu zetu zote umepatikana sasa tupiganie elimu.

Congress ikapitisha azimio la kujenga shule nchi nzima na kujenga Chuo Kikuu.

Kazi ikaanza chini ya EAMWS shule zikawa zinajengwa.

Mwaka wa 1968 Nyerere akaalikwa na EAMWS kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu Chang'ombe.

Nyerere na Kanisa hawakupenda kuona juhudi hizi zinafanikiwa.

Chokochoko za chinichini zikaanza dhidi ya EAMWS na uongozi wake.

Serikali ikaivunja EAMWS na kuunda BAKWATA na ikachukua mali za EAMWS na kuipa BAKWATA.

Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kufukuzwa Tanganyika.

Huu ndiyo ukawa mwisho wa miradi yote ya elimu.

Tusimame hapa kwa sasa ukipenda tutaendelea kwani ni kisa kirefu sana cha mapambano baina ya Waislam na serikali na mawakala wa kanisa ndani ya serikali waliokuwa na mipango maalum ya kuhakikisha kuwa Waislam wa Tanganyika hawatopewa fursa sawa na Wakristo katika elimu.
 
Unawafaham kirilo wewe au unajisemea tu. Mzee usilazimishe historia ya dini kuwa ya watu. We unajua uchaggan kulikuwa na mamangi wangapi na walitawalaje na mfumo wao ulijiendesha vipi. Unajua uchaggan kulikuwa na bunge bendera na hata wimbo wake.? Kwa kukusaidia huyo mtu nenda kwenye maktaba za dini ndio wanamjua ila kama unataka historia ya wachagga nitakuelekeza pa kuipata sio ngumu kama unavyofikiria. Maana mangi wetu wa mwisho alikuwa msomi kuliko Nyerere na kila kitu kaweka kwenye maandishi.
 
Huoni ukweli ndg yangu.
sasa tz bara unajaza wanzanzibar kwenye teuzi huku zanzibar haruhusiwi mbara kuteuliwa na hata kumiliki ardhi
 
mmetafuta elimu ila hamsomi whats wrong.
shule za kiislam na vyuo vyake ndivyo vinavyoshika mkia.
 
Kitali,
Unaniuliza kama namfahamu Japhet Kirilo.

Naam namfahamu Japhet Kirilo vizuri na mchango wake katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kitabu cha Abdul Sykes (English) nimemtaja mara 25 na katika (Kiswahili) mara 32.

Nakuwekea na picha nilipofika nyumbani kwake Ussa River mwaka wa 1989 nikiwa na Abdulwahid Ally Sykes mtoto wa Ally Sykes ambae yeye alikuwa rafiki yake sana kwa ajili ya urafiki uliokuwapo baina yake na akina Sykes wakati wa kwanza Meru Land Case kisha katika kamati ya Japhet Kirilo, Abdu Kandoro na Abbas Sykes aliyotembea Tanganyika kueleza yaliyojiri UNO katika safari ya Kirilo na Earle Seaton mwaka wa 1952.

Ningeweza kukueleza mengi lakini naamini hayo hapo juu yanatosha la unhitaji taarifa zaidi nifahamishe.

Kulia Mwandishi na Abdul Ally Sykes nje ya nyumba ya Japhet Kirilo Ussa River 1989

Umeniuliza kama najua Uchaggani kulikuwa na mangi wangapi.

Ukweli ni kuwa sijui idadi ya mangi lakini wale ambao walihusika katika maisha ya Muro Mboyo baba yake Rajabu Ibrahim Kirama wote nimewatafiti na wamo katika kitabu cha Kirama: Mangi Ndeseruo Mamkinga, Mangi Renguo, Mangi Ngulelo, Mangi Abdiel Shangali, Mangi Ngamini, Mangi Sina, Mangi Rindi Mandara, Mangi Marealle na Mangi Meli.


Chief Abdiel Shangali

Paramount Chief Thomas Marealle


Mangi Ngulelo​
Unaniuliza kuhusu utawala wa Wachagga.

Nimesoma mengi katika historia ya Wachagga hadi barua za Joseph Merinyo na Paul Njau katika Nyaraka za Rajabu Kirama.

Nimesoma kuhusu vyama vya Wachagga to hofu najua mengi na yote yamo katika kitabu cha Rajabu Kirama.

Vitabu vya waandishi hawa wawili: Bruno Gutmann na Charles Dundas ndiyo vyenye historia kubwa kuhusu Wachagga.

Kote huko nimetalii.

Lakini nataka nikufahamishe kitu ambacho huenda hukijui.

Nimefika Kidai na nimeona maktaba iliyoko pale na nimesoma baadhi ya taarifa kuhusu utunzwaji wa kumbukumbu.

Pita tena uangalie hali ya hizi maktaba.
 
Sikuambii mmeru Chief nakuambia mchagga si unaona sasa. Uliwah kujua mangi meli kuna watu aliwah kuwatuma mpaka ujeruman kama wawakilishi wake Chief.
 
Sikuambii mmeru Chief nakuambia mchagga si unaona sasa. Uliwah kujua mangi meli kuna watu aliwah kuwatuma mpaka ujeruman kama wawakilishi wake Chief.
Kitali,
Katika utafiti wangu sikupata kumsoma Mangi Kirilo popote.

Nitashukuru sana kama utanipa taarifa zake zaidi na alitawala wapi na miaka ya utawala wake.

Halikadhalika sijaona popote pale Mangi Meli alipotuma ujumbe kwenda Ujerumani.

Historia ya Mangi Meli na Wajerumani ni historia ya uhasama.

''Mangi Meli akiwa bado kijana mbichi wa miaka 40 alinyongwa kwa idhara kubwa pamoja na majemadari wake wawili mbele ya watu wake tarehe 2 Machi 1900.

Inasemekana kukamatwa kwake kulitokana na usaliti uliofanywa na baadhi ya machifu wenzake waliokula njama na Wajerumani.

Kitanzi hakikutosha kumaliza uhai wa Meli.

Ilibidi wammalize kwa risasi akiwa amelala chini akivutia roho.

Kosa la Mangi Meli lilikuwa kupinga ukoloni wa Wajerumani katika nchi yake alimozaliwa na kama walivyofanya kwa fuvu la Mtwa Mkwawa ni hivyohivyo walikikata kichwa cha Mangi Meli na kukipeleka Ujerumani.

Wajerumani hawakuthamini ihsani aliyofanya Mangi Mandara ya kuwakaribisha na kuifunga nchi yake kupokea Injili.

Wajerumani kwa kumyonga Mangi Meli mtoto wa Mangi Mandara walipeleka ujumbe mzito kwa watawala wote wa Uchaggani nini kitegemewe kuwapata ikiwa watathubutu kunyanyua silaha dhidi yao.''

(Mohamed Said, ''Rajabu Ibrahim Kirama Jemedari wa Vita Kuwa Jemedari wa Uislamu,'' (2020).


Sheikh Rajabu Ibrahim Kirama​

Hii ndiyo historia ijulikanayo.

Ikiwa wewe una historia kinyume ya hii tafadhali tufahamishe.
 
mmetafuta elimu ila hamsomi whats wrong.
shule za kiislam na vyuo vyake ndivyo vinavyoshika mkia.
Lap...
Hili ulilosema ni jambo linahitaji muda mrefu kuelezwa hapa.

Naamini hujui hujuma zilizokuwa zinafanyika NECTA kiasi ya kusababisha maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.

Taarifa zipo na wahusika wanazo.

Mengine nafanya staha siwezi kuyaeleza hapa kwani hapana haja ya kuiamsha fitna iliyolala watu wakachukiana.

Waislam siku zote hudai haki zao kwa upole.


Moja ya bango katika maandamano dhidi ya NECTA 2012​
 
Hakuna mangi kirilo chief ila narudia tena hujui historia ya wachagga Chief. Kwa kukusaidia Mangi Meli alikuwa mtu wa karibu sana wa wajeruman kabla hawakosana. Na ndie aliyewatumia kumsaidia kuwapiga tawala nyingine uchaggan. Mzee huongei na mtu mwepesi. Sio kwamba sisi tunaongea bila tafiti. Nimekuambia ukihitaji historia ya wachagga zipo sio hizo za kidini. Unatakiwa kujua wazungu wa kwanza kufika walifikia wapi kabla ya kuja wazungu ni koo gan ilitawala uchaggan nk
 
Kitali,
Wewe ndiyo uliyoleta jina la Kirilo katika Mangi.

Ndugu yangu unaandika umekasirika kwa Wachagga kuhusishwa na Uislam.

Hii ndiyo imekuvuruga.
Mimi sisemi kuwa ni bingwa wa historia ya Wachagga ila nimeingizwa katika historia ya Wachagga kwa kuandika kitabu cha Mchagga Sheikh Rajabu Ibrahim Kirama.

Ukaribu wa Mangi Meli na Wajerumani inategemea wewe unavyotafsiri siwezi kukuingilia kwa hilo.

Historia inaonyesha urafiki ulikuwa baina ya baba yake Rindi Mandara na Liepzig Mission kwa kuwapa ardhi bure na kuwafungulia milango ya kutangaza Injili.

Mangi Mandara alipokufa ndiyo Meli akaanza kudai ardhi yao ilipiwe.

Hapo ndipo ugomvi ukazuka.

Unazungumzia uzito wako katika historia?

Sawa mimi nashukuru kwani nataka nisome nisiyoyajua kuhusu Ibrahim Kirama kutoka kwako lakini bahati mbaya historia yake imekuudhi kwa kuwa ni historia ya kuenea kwa Uislam Uchaggani.

Lakini elewa mimi nimeandika kitabu cha Rajabu Kirama si historia ya Wachagga kama kabila.

Wazungu waliofika Uchaggani nawafahamu nina historia yao yote.

Nimemsoma Baba wa Wachagga Mjerumani Bruno Gutmann vizuri.

Alikuwa rafiki mkubwa wa baba yake Rajabu Kirama Mzee Muro Mboyo Kamanda wa Majeshi ya Chief Shangali.
 
Narudia kukuambia Mzee huijui historia ya wachagga Chief. Acha kung'ang'ania. Ukitaka historia niambie nikuelekeze pa kuipata.wewe elezea historia ya uislam lakin sio ya wachagga. Tofautisha mandara aliyewapokea wamishenari na Meli aliyepokea utawala wa kijeruman. Nikuulize swali dogo. Unamfahamu mjeruman aliyeitwa "mbuuya" na wachagga?
 
Wewe mwenyewe ni Mdini

Ulipaswa ukileta mada iwe neutral na ubalance bila kuonesha kutetea upande wa dini moja

Wewe umetetea Uislam na kuonesha chuki kwa Wakristo
 
Huyu Mleta mada ni Mpuuzi mmoja aliyejiandikia tu bila ushahidi wowote

CHUKI wanayo wao, angalia huko Zanzibar Wakristo wanavyofanywa na hata huku bara katika misikiti yao na mihadhara wanatusema vibaya sana
 
Weka na Wakuu wa Nchi (Marais), Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu kwa Upande wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania : -

Tuanze :

1) Rais Awamu ya kwanza Mkisto
Rais wa Zanzibar. Muislam


2) Awamu ya Pili. Muislam
Rais wa Zanzibar. Muislam
Makamu/Rais. Muislam
Waziri Mkuu. Muislam


3) Awamu ya 3

Rais Mkristo,
M/ Rais. Muislam
W/ Mkuu. Mkristo
Rais wa Zanzibar. Muislam
M/ Rais Muislam
W/Mkuu. Muislam
Jaji Mkuu. Muislam


4) Awamu ya 4 -


  • Rais. Muislam
  • Makamu wa Rais Muislam
  • Waziri Mkuu. Muislam
  • Jaji Mkuu. Muislam
  • Rair wa Zanzibar. Muislam



5) Awamu ya 5

- Rais. Mkristo

  • Makamu Mkristo,
  • Waziri Mkuu. Muislam
  • Rais wa Zanzibar Muislam
  • M/Rais Zanzibar Muislam
  • Waziri Mkuu Muislam
  • Jaji Mkuu. Muislam


6) Awamu ya 6

  • Rais. Muislam
  • M/ Rais. Mkristo
-W/ Mkuu. Muislam
Rais wa Zanzibar. Muislam
M/ Rais. Muislam
W/ Mkuu. Muislam

Hapa viongozi wakuu wa JMT, 80% ni Waislam Tangu kupatikana kwa Uhuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…