Listen, hata hiki ulichoandika hapa kwangu ni muendelezo wa fikra duni, ujinga; sioni kama taifa tunaweza vipi kupiga hatua kimaendeleo ikiwa bado tutakuwa tunatazamana kwa jicho la dini, kabila, au rangi.
Wewe umekuja hapa kuwatetea wale wa dini yako, simply umekuja kuongeza tatizo, hukumbuki wapo wasio na dini, wakina
Kiranga na wenzake wao wamenyamaza kimya, hawana msemaji wao, na wala hawana hivi viherehere mlivyonavyo wengine.
We need to stop this kind of ignorance, kwasababu kutaka watu wa dini yako wawepo kwenye mamlaka hakutakusaidia chochote kama hutakuwa na mahusiano nao ya moja kwa moja, zaidi, kinachowafanya wengi wazungumzie hii issue ni kama ulevi tu, usio na tija kwao wala kwa taifa.
Huu upuuzi una extend mpaka pale anapokuwepo kiongozi fulani, halafu wale wa dini yake wanakuwa hawaoni baya lolote toka kwake, huu nao ni ujinga mwingine mkubwa zaidi, kusifia/tetea kila linalofanywa na yule wa dini yako upuuzi.