Ijue siri ya kutochacha kwa pilipili

Ijue siri ya kutochacha kwa pilipili

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
1,744
Reaction score
3,020
Habar zenu
Natumain wazima woote

Leo tujifunze kutangaza pilipili rahc zaid,ya haraka na itakayokaa kwa muda mrefu bila hata kuweka kwenye frige

Mahitaji
Pilipili unazohitaji ww
Nyanya fresh 5
Vitunguu maji 2
Karoti 2
Kitunguu saumu 1 kikubwa
Tangawizi 1 kubwa
Biringanya 1
Vinegar nusu kikombe(husaidia saaana kutochacha kwa pilipili)
Chumvi kijiko kidogo cha chai


Jinsi ya kutengeneza

Katakata Katoti,tangawizi,vitunguu saumu,pilipili,nyanya na biringanya kisha weka kwenye mashine ya kusagia kama unayo na kama huna bac tumia kisagio cha nyanya

Changanya vyote kwa pamoja kisha uvisage
Hakikisha vimesagika vema
Vitoe weka chumvi na vinegar na ukoroge

Baadaya hapo pilipili itakuwa tayar,sio lazima kuipika inawaza pia kuliwa hvy hvy una hiyari ya kuitoa juani au usiitoe na pia Sio lazima kuiweka kwenye frige inakaa muda mrefu zaid ya wiki 2

NB;Ni vizuri zaid kuihifadhi kwenye chumba ambayo utakuwa unamimina ili kuepuka kuigusagusa pia huchangia kuchagua haraka
 
Yah ukwaju itafaa kwasababu inaongeza ladha ya uchachu kama vinega Ila sijawahi jaribisha kama itakaa kwa muda mrefu

Sidhani kama jibu lako ni sahihi!

Vinega ni additive inayofanya kazi ya kuongeza shelflife ya chakula, sasa sijui kama ukwaju nao unaongeza shelflife kama sio taste peke yake!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom