The25824
Member
- Sep 8, 2024
- 20
- 82
Kwenye maisha kila mtu ana haki ua kutoa maoni yake kwa vile anavofikiria.
Bahati mbaya wengi tumeshindwa kufikia ndoto zetu au kuamua mambo yetu kwa kuishia kusoma comments za watu humu ambao bila kutafakari tumeishia kufanya maamuzi ya juu kwa juu.
Ni wangapi wameacha kuanza biashara kwa kuambiwa tu hailipi hata kabla ya kuifanya?
Wangapi wameacha kusoma kozi fulani kwa kuwa tu kuna uzi ulielezea ugumu wake?
Ukienda mbali,wangapi wameacha wake au waume zao kwa kigezo tu alisoma mada fulani jukwaa la mahusiano na akaona uamuzi wa mwenzake basi uwe wake kwa familia alionayo?!
Sikwambii wale ambao ni rahisi kukasirika hata urushiana maneno na mtu asiyemuona kisa tu kajibiwa kinyume na matarajio yake.
Ili kujitibu hali hii vema kutambua ;
Mosi,Amini mengi ya yanayotolewa mtandaoni sio sheria ,bali ni maoni ya mtu binafsi hivyo una wajibu wa kuchuja nawe kwa upande wako ukaja na jibu ambalo utojutia.
Pili,Kuwa na muda wa kutosha wa kutafakari mambo yako kabla ya kuamua kuyaleta hadharani.Namaanisha lijue jambo kwa undani wake kabla ya kuamini watu wa mtandaoni
Watakupa majibu ya kila kitu.
Tatu .kama jambo ni la kufanya zaidi,Jikite kwenye vitendo zaidi kuliko maneno.
Kuna mambo ukifanya kwa vitendo vyepesi kurekebisha au kuboresha kwa usahihi kuliko kama utaliacha tu kwenye maneno.
Mwisho jiwekee nia ya kujifunza kila uchao mambo mapya nje ya yale unayoyajua au kuyazoea.
Likija kwako usilidharau wala usilipokee na kufanyia kazi moja kwa moja,bali kaa chini kisha jiambie ni sehem ya kulifanyia uchunguzi au kujifunza zaidi..