OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Nene msukulu wa Mbago, Bwana Mkoba au Mfuko Nawasalimu.
Nitatumia siku tano, kuelezea baadhi ya Mazingira ya watu wa Morogoro kila siku ikiwa na mada tofauti. Lakini leo naanza na nadharia ambayo si ngeni kwa watu wengi waliomo humu.
Naam, kuhusu kabila la Waluguru. Imetajwa kuwa waluguru wametokana na mzizi wa neno 'kulu' lenye maana ya Kubwa au Iliyoinuka ambayo kwa athari za ilikuja kuwa 'guru'. Ukimsoma James Brian anaonesha kuwa neno hili ni moja kwa waluguru na wakaguru kwa maana ya kushare mzizi wa neno 'guru'
Tofauti yao ikiwa kuwa, Luguru wanakaa milimani ndipo walikopata jina hilo huku kama ilivyo kwenye kiswahili, kiambishi 'ka' kinamaanisha udogo, hivyo wakaguru ni wanaokaa eneo la miinuko midogo.
Hapa utagundua ukweli wa nadharia hii kwa kuwa waluguru walikuwa wanakaa milimani, huku wakaguru wengi wakiwa maeneo ya Msowero (Kilosa ya leo) ambayo haina milima sana kama Mgeta na Matombo. Kwa sasa wakaguru wapo wengi zaidi maeneo ya Gairo lakini wametajwa kuwa ni watu waliohamia huko baadae sana.
Mkoba Mfuko anayasema aliyonayo.