Ramsy Dalai Lama
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 156
- 554
Vita fupi zaidi kuwahi kutokea ni Vita vya Anglo-Zanzibar. Vita hii ilidumu kama dakika 38. Sultani wa Zanzibar alipofariki, mpwa wake Sultan Khalid alijitangaza kuwa sultani. Lakin tatizo lililojitokeza lilikuwa ni kwamba Zanzibar ilikuwa na makubaliano na Uingereza ambayo yalihitaji lazima Muingereza aidhinishe sultani ajaye.
Na hata hivyo Mamlaka ya Uingereza ilimpendelea Hamoud bin Mohammed, ambaye waalikua na maslahi nae, na waliona angefaa kuwa sultani. Katika makubaliano ya tarehe 14 Juni 1890 Zanzibar na uingereza walikubaliana kwamba kuanzisha ulinzi wa pamoja Zanzibar na Uingereza ikawa ndie atatoa ulinzi huo pamoja meli za kijeshi na mwisho lazima Sultan ajae kabla kuingia katika Usultan anapaswa kupata kibali cha balozi wa Uingereza.
Utata ulikuja pale Khalid ambaye alitaka kurithi kiti cha usultan hakua ametimiza sharti hili na akaingia kwenye kasri la sultan bila idhini ya uingereza nakujitangaza Sultan. Waingereza walilichukizwa na hili na wakatuma ujumbe kwa Khalid wakitaka aamuru majeshi yake pamoja na yeye mwenyewe kuondoka kwenye kasri. Lakin Khalid alimwita mlinzi wa ikulu yake nakumuamuru kuweka ulinzi mkali na yeye kujificha ndani ya jumba hilo.
Waingereza wakamuambia kwa mara ya mwisho Khalid aondoke kwenye kasri yake na aache nafasi ya Usultani. Khalid alikataa. Waingereza hawakua na jinsi zaidi ya kumtoa kwa nguvu. Ilikua saa 9:02 asubuhi mnamo Agosti 27, 1896, Waingereza walianza mashambulizi yao. Ikulu ilichomwa moto na kuharibiwa. Meli tatu za Kizanzibari zilizamishwa na jeshi la wanamaji la Uingereza. Wanajeshi wa Kizanzibari waliokuwa wakiilinda walipigwa risasi.
Dakika 38 baadaye ambapo ilikua saa 9:40 asubuhi, mapigano yalisimamishwa baadaa ya majeshi ya Khalid kusalimu amri kuachiria wameshindwa vita. Na matokeo ni majeshi ya Khalid zanzibar walipata takriban majeruhi 500 na kwa upande wa mwingereza kulikuwa na baharia mmoja aliyejeruhiwa.
Hii ikawa vita fupi zaidi kuwahi kutokea na leo hii inashikiria record katika kitabu cha world Guinness ya kuwa vita iliyodumu kwa muda mfupi wa dk. 38 tu