Asante kwa kuleta mada lakini naona maelezo hapa kwenye wikipedia yanaeleweka kirahisi zaidi?
Vita ya miaka 30 - Wikipedia, kamusi elezo huru
Vita ya miaka 30
Vita ya miaka 30 ilipigwa kati ya miaka
1618 hadi
1648. Ilikuwa vita ya Kiulaya lakini mapigano yake yalitokea hasa katika
Ujerumani kwenye eneo la
Dola Takatifu la Kiroma.
Ma
dola ya Ujerumani yalipigana kati yao, na nchi za nje zilishiriki zikiwemo
Hispania,
Ufaransa,
Uswidi,
Uholanzi na
Denmark.
Vita ilileta
uharibifu kupita kiasi kwa ajili ya Ujerumani kushinda vita zote zilizofuata katika
historia. Hukumbukwa hadi leo.
Hali ya kisiasa kabla ya vita
Ujerumani ilikuwa sehemu kubwa ya
Dola Takatifu la Kiroma pamoja na majimbo ambayo leo ni
Ucheki,
Uholanzi,
Uswisi,
Ufaransa ya magharibi,
Italia ya kaskazini na
Austria. Dola Takatifu ilikuwa kama maungano ya madola madogo zaidi chini ya
Kaisari.
Mkuu alikuwa Kaisari aliyetoka katika
nasaba ya
Habsburg akiwa
mtawala wa
Austria hasa na
madaraka yake juu ya Dola Takatifu kwa jumla yalikuwa madogo. Maeneo mengine yalijitegemea kwa kiasi kikubwa chini ya watawala wao wa
kikabaila.
Miaka 100 kabla ya vita
matengenezo ya Kiprotestanti yalienea katika Ujerumani na sehemu ya madola ilipokea
madhehebu mapya, lakini wengine walibaki
Wakatoliki. Madola mengi yalisisitiza ya kwamba wananchi wote wafuate dhehebu moja tu, ama Ukatoliki ama Ulutheri; hapakuwa na
uhuru wa dini kwa kila
raia.
Uhusiano kati ya madhehebu ya Kikristo ulikuwa mbaya kwa muda mrefu. Karibu katika kila nchi Wakristo walilazimishwa kufuata madhehebu rasmi. Ikiwa mtawala fulani aliona vema kukubali mawazo ya
Martin Luther mapadri wote walipewa chaguo la kufuata Ulutheri au kuhama nchi. Vilevile baada ya
kifo chake ikiwa mtawala aliyefuata alikuwa na msimamo tofauti, mapadri wakarudi na wachungaji wa Kiinjili wakafukuzwa.
Raia hawakuulizwa wenyewe wanasadiki nini, isipokuwa katika miji iliyojitawala na kuwa na utaratibu wa ki
demokrasia. Lakini hata mijini huko haikuwa kawaida kuruhusu madhehebu mawili mahali pamoja.
Mafundisho ambayo kwetu leo yanaonekana kuwa na tofauti ndogo yaliweza kumfikisha mtu gerezani au hata kifoni.
Uhusiano mbaya ulikuwepo vilevile kati ya wafuasi wa Luther na Wareformati.
Katekisimu zao zilitumika kama
bendera. Walishutumiana kuwa
wazushi wasioelewa vizuri
kiini cha
imani.
Fitina ya kidini katika Bohemia
Vita ilianza kama
fitina kati ya
Kaisari aliyekuwa Mkatoliki Mwaustria na maungano ya madola ya Kiprotestanti ndani ya Dola Takatifu. Chanzo kilikuwa
uasi wa makabaila wa Kiprotestanti katika jimbo la
Bohemia dhidi ya siasa ya Kaisari
Ferdinand II aliyechaguliwa pia kuwa
mfalme wa Bohemia.
Ferdinand alikataa kukubali uhuru wa dini ulioahidiwa na mtangulizi wake kwa ajili ya Bohemia. Fitina hii ilikuwa vita baada ya
gavana wa Kaisari kutupwa nje ya
dirisha la
chumba cha
mkutano mjini
Praha tarehe
23 Mei 1618. Wakubwa wa Bohemia waliendela kutamka ya kwamba Ferdinand si mfalme wao tena, wakamchagua kabaila wa
Palentino kama mfalme mpya.
Kaisari alichukua
silaha na kwenye mapigano ya kwanza tarehe
8 Novemba 1619 karibu na mji wa Praha waasi wa Bohemia walishindwa. Makabaila wengi wa Kiprotestanti kutoka madola mengine ya Ujerumani waliamua kuwasaidia wenzao wa Bohemia. Vita hii ilielekea kwisha kwa ushindi wa Kaisari mnamo
1623.
Uswidi kusaidia Waprotestanti
Hapo nchi jirani zilijiunga na vita. Nchi za
Skandinavia zilifuata Uprotestanti na watawala wao waliamua kuwasaidia wenzao Wajerumani. Wa
denmark kwanza halafu Waswidi walifika kwa wanajeshi wengi. Mfalme
Gustav Adolf wa
Uswidi alishinda jeshi la Kaisari mara kadhaa hadi alipouawa kwenye
mapigano ya Lützen tarehe
16 Novemba 1632.
Kuingilia kwa Ufaransa
Baada ya kuona ya kwamba Kaisari aliendelea kusogea mbele, mfalme wa
Ufaransa alijiunga na Uswidi akashiriki katika vita tangu mwaka
1635. Nia yake ilikuwa hasa kuzuia enzi ya
nasaba ya
Habsburg iliyotawala
Hispania ikashika pia Austria pamoja na cheo cha Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma.
Hivyo vita iliyoanza kama mapigano ya kidini katika dola moja la Ujerumani iliendelea kuwa vita ya Kiulaya ambako nchi ya Wakatoliki kama Ufaransa ilishikamana na Uswidi ya Kiprotestanti dhidi ya Kaisari Mkatoliki.
Vita ilileta uharibifu mkubwa mno katika Ujerumani. Kuna makadirio ya kwamba karibu
theluthi moja ya wakazi wote walikufa kutokana na ma
uaji,
njaa na
magonjwa. Katika maeneo ya Ujerumani ya Kusini zaidi ya nusu ya watu walipotea.
Wanajeshi walikuwa
askari wa kukodiwa ambao mara nyingi hawakulipwa bali walipewa
uhuru wa kupora chochote walichotaka.
Amani ya Westfalia
Uchofu ulileta majadiliano juu ya
amani. Mwaka
1648 wawakilishi wa wafalme walipatana katika
amani ya Westfalia kanuni za amani.
- Madhehebu matatu yaliyokubaliwa Ulaya ni Wakatoliki, Walutheri na Wareformed.
- Kila mtawala aliamua kwa dola lake ni dini ipi itafuatwa lakini raia walikuwa na haki ya kutoka katika nchi kama mtawala alikataa dini yao. Sheria ilikuwa: "Cuius regio, eius religio" (mwenye nchi ni mwenye kuamua dini)
- Uholanzi na Uswisi zilitoka katika Dola Takatifu la Kiroma kama nchi huru za pekee.
- Mfalme wa Uswidi alitwaa maeneo makubwa katika Ujerumani ya Kaskazini
Mapatano hayo yaliunda ramani ya kimadhehebu kule Ulaya yenye maeneo ya Wakatoliki, Walutheri au Wareformati watupu.
Jumuiya ndogo ziliendelea kugandamizwa wakapata ustahimilivu mahali pachache. Hivyo wafuasi wa madhehebu madogo walilazimika kuficha imani yao au kuhamahama katika Ulaya.
Wakati ule nafasi mpya ilitokea: Mfalme wa Uingereza alikuwa na ma
koloni Marekani lakini alikosa watu. Akatafuta
walowezi kwa ajili ya makoloni yake akiwaahidia wote kwamba watapata
shamba pamoja na
uhuru wa dini. Hivyo watu kutoka nchi nyingi za Ulaya walianza kuhamia Marekani, hasa wale waliokosa uhuru huo.
Mpaka leo nchi mbalimbali za Ulaya zinafuata hasa madhehebu moja, na Marekani ina madhehebu makubwa ambayo hayana wafuasi wengi Ulaya, k.mf.
Wabatisti.