WINDOWS 7 ZAIDI
Hapo mwanzo tulijaribu kuona tofauti zilizokwepo kati ya windows vista na Windows 7 kwa mifano kadhaa ya muonekano wa baadhi ya vitu ndani ya Windows 7 pamoja Utendaji wake kazi , Ila tukubaliane kitu kimoja nacho ni kwamba Windows 7 iko fast sana na nyepesi kwenye kufanya shuguli nyingi sana zaidi ya Window vista , Ukiwa na windows 7 ni kama uko na windows Xp windows 7 inazidi baadhi ya vitu vya kiusalama na Graphics .
Wakati naandika Toleo la kwanza la Ijue Windows 7 nilikuwa sijapata Office 2010 , kwa siku za karibuni ndio nimeipata Office 2010 nikafanikiwa kuweka katika windows 7 kuona inavyofanya kazi , kwa kweli haina tatizo sana na Windows 7 zaidi ya kuchelewa kuload wakati inapoistart hiyo application ya office sio kama office za nyuma kama xp , 2000 , 2003 na 2007 .
Kuna wale waliokuwa wanalalamika kwamba Baadhi ya Programu professional hazifanyi kazi katika windows Vista mfano Prokon 2.1 , Master series 2006 , hizi programu zinafanya lakini mpaka wakati unaanza mara ya kwanza Right Click Juu ya Icon ya Programu husika Run As Administrator , hili ni kosa la Microsoft ila kosa hili kwenye Windows 7 haliko tena .
Lingine nililoona ni kuhusu Antivirus , katika version ya Windows 7 niliyotumia mimi , sikufanikiwa kuingiza antivirus yoyote ya nyuma mpaka sasa imekubali kuingiza Symantec Enterprise Server Edition ( 2009 ) antivirus hii huwa naitumia zaidi katika windows 2003 server hata client yake imekataa kuingia katika windows 7 sijafanya uchunguzi kujua ni kwanini lakini bado tunaendelea kuona itakavyokuwa , hata Kaspersky 2010 Antivirus nayo inakubali kuingia sema haikubali kufanya activation Ukiwa Nje ya Mtandao mpaka uwe katika Mtandao ndio huwa inakuli hata kama una Keys zake tofauti na zile editions za nyuma za antivirus hii .
Kwa wale waliokuwa wanaogopa windows vista kutokana na Utaratibu wake wa kufanya Kazi , badi sasa wahamie Windows 7 waone mambo Makubwa zaidi , nitaendelea kuwaandikia zaidi jinsi ninavyoweka programu zinavyofanya kazi na mengine zaidi