Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hili ziwe ni siku za kuwakumbuka waliotekwa, kuteswa na kuuawa.

Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hili ziwe ni siku za kuwakumbuka waliotekwa, kuteswa na kuuawa.

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Ndugu zangu Watanzania, itambukwa kuwa kumekuwa na utekaji, utesaji na mauaji kwa ndugu zetu Watanzania hapa Nchini. Kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo viovu, binafsi napendekeza siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hili ziwe ni siku pekee za kuwakumbuka Watanzania wenzetu waliopatwa na majanga haya.
Nashauri ibada zote zitakazofanyika katika siku hizo Makanisani na Misikitini, mahubiri yote 100% iwe ni kukemea maovu haya.
Hakuna maana kabisa kama tunakwenda Makanisani na Misikitini na hatimaye tunaambiwa nendeni na amani na sisi tunaitikia, Amina wakati huo wenzetu wengi wamepatwa na majanga kama hayo, hiyo amani inatoka wapi katika mazingira hayo?
Kama kweli viongozi wetu wa Dini wanaguswa na matukio haya mabaya, watayakubali na kuyafanyia kazi mapemdekezo yangu haya, lakini kama viongozi wetu wa Dini matukio haya kwao si kitu, watayapuuza mapemdekezo haya na kuyatupilia mbali.
Mungu mkubwa.
 
Back
Top Bottom