Ijumaa ya leo siielewi kabisa

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Kwanza leo asubuhi naona kama maaskari wengi wapo barabarani mpaka kwenye magari ya mwendokasi.

Nimefika job kazi haziendi kabisa, nawaza tu hapa juu ya Tundu Lisu..

Honestly kazi haziendi kabisa leo, hapa naongea nusu nipitishe famba hapa kwa mawazo.

Hakika hii ijumaa imejaa majonzi makubwa.

Maisha haya magumu halafu mtu kama Tundu Lisu akituondoka tutakuwa wakiwa sana, nani atapaza tena sauti za wanyonge?

Eeeh Mungu wa mababu, Mungu muumba wa Nchi, Mungu wa Adam na Hawa, Mungu mwenye uwezo wa kila kitu.. Eeeh Mola,, eeeh Yehova.. Tunakuomba usiuzime mshumaa huu uangaziao wanyonge watanzania na wapenda mabadiliko..

[HASHTAG]#Hakutakuwa[/HASHTAG] na siku ijumaa ngumu kama ya leo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewaza kitu sahihi sana, nchi nzima hali ni hiyo hiyo. Lumumba tu ndio watakàokanusha hii hali.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Wewe jana siulikua unafurahia mkasa wa TL?
Hapana mkuu jana nilikuwa natetea ile hatua ya Magufuli kwenye zile report. Ila naomba nikuambie tukio la Lissu linaniuma roho sana sana sana..

Huyu mwanasiasa mi nampenda sana kuliko viongozi wote wa upinzani.. Siwezi hata siku moja kutokuacha kumpenda Lissu.

Jana nusu nidondishe chozi mbele ya staff wenzangu maana nilitoka kula ndo nikapewa hiyo habari ningeweza kupata pressure..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote ili nchi isonge lazima watu wafe..mtetezi wa nchi kwa sasa ni magufuli..hao wengine wananenepesha vitambi tu..wamesongwa na anasa za dunia..we endelea kutafuta ugali wa wanao
 
Siku zote ili nchi isonge lazima watu wafe..mtetezi wa nchi kwa sasa ni magufuli..hao wengine wananenepesha vitambi tu..wamesongwa na anasa za dunia..we endelea kutafuta ugali wa wanao
We ni pepo.. Unafanya nini kwenye jamii ya binadamu?.. Mijitu mingine ndo mnatuletea laana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…