Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Wana Jamiiforums
Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh?
Tunapoelekea kuumaliza Mwaka huu wa 2024 na kuelekea Mwaka mwingine siku chache zijazo. Nina maneno machache ya kuwaambia Familia nzima ya Jamiiforums siku hii ya Leo ijumaa ambayo ni ijumaa ya mwisho kwa Mwaka huu.
1. "Mwaka unapokaribia kuisha, tunashukuru kwa baraka, tunajifunza kutokana na changamoto mbalimbali tulizozipitia, na tuna kwenda kuukaribisha mwaka mpya tukiwa na matumaini na imani tele"
2. " Inatupasa kushukuru kwa kila somo lililokuja mwaka huu. Tunapoelekea mwaka mpya, inatupasa kuwa na imani utakuwa ni mwaka wa mafanikio na furaha tele."
3. "Kila mwisho ni mwanzo mpya. Tuukaribishe mwaka mpya kwa moyo wa shukrani na ndoto mpya."
4. "Mwaka 2024 umekuwa safari ya kujifunza, kukua, na kushukuru. Tusonge mbele kwa matumaini na bidii."
5. "Tunapouaga mwaka huu, tushukuru kwa kila jambo – kubwa na dogo – lililotufanya kuwa bora zaidi."
Ijumaa Kareem 🤲