Ijuwe katiba ya Tanzania

Ijuwe katiba ya Tanzania

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
*```TUJIFUNZE SHERIA```*

*IJUE KATIBA YA TANZANIA*

```Katiba ni msingi mkuu wa uendeshji wa nchi, ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Katiba kama Sheria mama hutaratibu muafaka wa jamii husika kwa kuweka bayana misingi ya utawala, vyombo vya utawala, mgawanyo wa madaraka baina ya vyombo vikuu vya dola- yaani Serikali Bunge, na Mahakama. Vivyohivyo Katiba ya Nchi hueleza bayani Haki na Wajibu wa Wananchi, na Mahusiano baina ya Wananchi na Serikali yao.```
*```Aina za Katiba```*
```Kuna aina nyingi za Katiba lakini zote zaweza kugawanyika katika aina kuu mbili;

1.Zilizoandikwa/ Katiba Andishi/ Written Constitution:
Ni katiba ambazo zimeandikwa katika mfumo wa Kitabu au machapisho mbalimbali yaliyo katika mfumo wa Kitabu. Ni katiba iliyotungwa na bunge la Katiba ya Nchi husika. Katiba za aina hii zaweza fanyiwa marekebisho tu kutokana na taratibu zilizomo katika Katiba hiyo. Mfano wa Nchi zenye Katiba ya aina hii ni Tanzania, Kenya, Ujerumani, Uganda, Marekani, India nk.

2. Ambazo hazijaandikwa/ Katiba Mapokeo/ Unwritten Constitution:
Ni katiba ambazo hazijatungwa na bunge la katiba na haziwezi kupatikana katika mfumo wa kitabu. Zinapatika katika machapisho mbalimbali. Mfano wa Nchi yenye Katiba hii ni Uingereza.```

*```Historia Ya Katiba Tanzania```*

```Kwa ujumla wake nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina Katiba zilizoandikwa. Katiba nyingi kati ya hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka. Kwa mantiki hiyo katiba nyingi katika nchi zilizoendelea Kama Tanzania zina uhusiano/Kushabiana na Katiba na Tawala za kikoloni kabla ya Uhuru.```

```Tangu tupate Uhuru, Tanzania imekua na Katiba Nne kabla ya Katiba ya Kudumu ya sasa ambayo ni ya Tano. Katiba hizo ni hizi zifuatazo;```

```1. Katiba ya Uhuru (1961)
Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1961 ilitokana na azimio la sheria ya uhuru (Order in Council) lililopitishwa katika Bunge la Uingereza na kuletwa Tanganyika kama Katiba ya awali. Katiba hii ilitengenezwa na waingereza nchini Uingereza na kuletwa Tanzania. Hata hivyo Katiba hii ilikuwa na mapungufu kadhaa kubwa ikiwa mambo mengi ya kutegemea kufanyiwa maamuzi toka Uingereza.```

```2. Katiba ya Jamhuri (1962)
Katiba hii ilitambua Tanzania (Tanganyika kwa kipindi hicho) kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge. Utengenezaji wa katiba hii haukuhusisha wananchi wa kawaida. Ushiriki ulibaki mikononi mwa wabunge wa TANU ambao walijigeuza na kuwa bunge maalum la Katiba lililopitisha Katiba hii.
Katiba ya hii ndiyo ilianzisha mfumo wa Urais ambaye pia alikuwa Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa serikali. Baraza la Mawaziri na waziri mmojammoja sasa waliwajibika kwa Rais badala ya bunge.```

```3. Katiba ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964)
Hii ndiyo Katiba ya kwanza ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Katiba hii ilitokana na hati za makubaliano ya muungano ambazo zilifikiwa kuelekea siku ya muungano ulifanyika tarehe 26 Aprili 1964. Katiba hii ilianzisha mambo 11 ya Muungano ambayo kwa sasa yamefikia 22. Katiba hii ndiyo iliyoanzisha muundo wa serikali mbili. Rais wa Zanzibar alikuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na mjumbe wa Baraza la mawaziri. Katiba hii ilitazamiwa kuwa Katiba ya muda ya Muungano ambayo ingetumika kwa mwaka mmoja tu na iliweka utaratibu wa kuandaa Katiba ya kudumu ya Muungano kwa kuunda Tume ya Katiba na bunge la Katiba. Tume hii ndiyo ya kwanza ya Katiba ya Tanzania na ilikuwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa.```

```4. Katiba ya mpito ya mwaka (1965)
Katiba hii ilijulikana kama Katiba ya mpito. Katiba hii ilileta sura mpya ya mambo katika siasa za Tanzania.Mabadiliko haya yalilenga kuweka mfumo tofauti kabisa wa kisiasa na ndiyo iliyorasimisha nchi kuwa ya chama kimoja cha siasa. Hata hivyo kulikuwa na vyama viwili vilivyokua madarakani. Tanganyika iliongozwa na Tanganyika African National Union (TANU) wakati Zanzibar ikiwa chini ya Afro Shirazi Party (ASP). Katiba ya chama cha TANU ilikuwa sehemu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba hii ilitokana na mchakato wa Tume ya Rais ya Katiba iliyokusanya maoni ya baadhi ya wananchi. Katiba hiiilitamka chama kushika hatamu ya uongozi na nchi. Mambo ya Muungano yalianza kuongezeka na utata wa uhuru (autonomy) wa Zanzibar nao ukazidi jambo ambalo limeendelea kutatiza muungano hadi sasa. Miaka kumi na mbili baadaye ikaundwa Katiba ya Kudumu na ndiyo iliyopo hadi hivi sasa.```

```5. Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
Hii ilikuwa ni Katiba ya tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba hii ilipatikana kupitia Tume ya Rais iliyokuwa na wajumbe 20 (10 toka kila upande wa Muungano) ikiongozwa na Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake akiwa Ndugu Pius Msekwa. Tume hii ilianza na kazi ya kutunga Katiba ya CCM ambayo ilizaliwa baada ya kuunganisha vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) tarehe 5 Februari, 1977.
Katiba yenyewe ilijikita katika misingi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na muundo wa serikali mbili. Katiba hii ilipitishwa na bunge maalum lililoteuliwa na Rais kutokana na bunge la kawaida. Kwa ujumla Katiba ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko mara 14 tangu ilipopatikana.```


```Ni Mabadiliko gani yaliyofanywa katika Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, tafadhali usikose kufatilia sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hii ya IJUE KATIBA YA TANZANIA.```

*```Tafadhali usiache kulike ukurasa wetu facebook wa Tuzungumze Sheria na kushare na Marafiki.```*
1474319993084.jpg
 
Back
Top Bottom