Ikeda air Freshener Vs matatizo ya kifua!

Asee umenifumbua macho, mwezi july nikiwa Mtwara nilipanda gari ya jamaa yangu ikiwa na harufu nzuri sana , alikuwa anatumia uturi wenye jina hilo hilo
Kimbembe kilianza siku ya pili baada ya kupanda gari lile , nilipatwa na mafua makali sana mixer homa na macho kuvimba kama mchina ,nilisota na hali hiyo karibu siku kumi ndo nikapona.
Yani kama sio wewe kuleta huu uzi nilikuwa naamini kuwa gest niliyolala ndio ilinisababishia mafua yale
 
Pole sana mkuu...huo msamiati "uturi" sijausikia siku nyingi sana.
 
Aisee hii kitu ina ukweli, the very first time niliikuta kwenye gari ya jamaa yangu tulikuwa na roadtrip moro-iringa-dom-mikoa ya kanda ya kati.. zile siku mbili kifua kilikuwa kizito mno.. baada ya safari nikapigwa na mafua makali na maumivu ya kichwa (nikawa na mixed thoughts kuwa labda ni kacovid au niko alergic na yale manukato)

Over time nikaja kuconfirm kile kidude kwangu ni changamoto kuna jamaa yangu aliazima usafiri na akajiongeza akakanunua kile kidubwasha akakiweka, alivyorudisha nikawa napitia hali ya kifua kuwa kizito, mafua feki, kichwa kinagonga na usiku kama nakuwa nawashwa hivi, halafu ile harufu inabaki kwenye mwili..

Yale manukato hayajatengenezwa kwa ajili ya mjumbe kama mimi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…