Ni miaka 6 imebakia kufika mwaka 2030 ambapo kwa hali ya sasa ya wanawake na tabia na mienendo yao then kuna uwezekano mkubwa wakaingia umri wa utu uzima a.k.a Ukuta wa babeli wakiwa hawana watoto, familia, mume, ndoa ya kueleweka wala anuani ya mji wao.
Hii ni matokeo ya matumizi mabaya ya rasilimali za thamani sana yaani mwili na muda, walizopewa na MUNGU bure bila kulipia hata mia.
Ni ukweli usio pingika kuwa wanawake wa sasa wamejiweka mbali sana na uanaumke kiasi kwamba wanajiendea tu na trends na upepo wa walimwengu wasijue kesho inawajia kwa kasi ya fuso isiyo na break.
Huo mwaka nimeutaja nimelenga uzao wa kuanzia miaka fulani sitoitaja hapa ili kupunguza tension but ukipiga hesabu unaweza jua kama wewe unaangukia wapi.
Najua watakuja wadada wapenda ligi akina
Jadda na wengineo na kupinga haya nisemayo ili tu kuipa amani mioyo yao ila ndani ya nafsi wanajua kuwa hali si nzuri.
Watasema wanaume kwao itakuwa same story. Wanaume story yao huwa si sawa na ya mwanamke. Mwanaume huo wakati target audience yake ni younge females ambao wewe watakuwa wanakuita mama au shangazi.
Tazama akina auntie Ezekiel,shilole, wolper, wema, buheti, kajala, etc hao nimewataja sababu ni maarufu ila huku mtaani wapo wengi zaidi ya hao ambao kwa umri wao wanavulia chupi vibwana vidogo umri sawa na wadogo zao au watoto zao wa kuwazaa. Imagine hao 2030 haijafika bado.
Hiki kitakuwa kipindi kigumu sana katika historia ya mahusiano watakachopitia wanawake katika taifa letu na ulimwenguni sababu ya kujitoa ufahamu, kukengeuka, na kuishi nje ya mfumo wa jamii vile uliagiza.
Siku zote kukopa raha kurudisha maumivu. Wengi kwa sasa mnataka kufosi kuishi mafanikio ambayo muda wake hamjaufikia. Matokeo ni kusaliti, kuumiza hisia, kukufuru, kukaranganya jamii, na kuharibu ustawi wa jamii.
This is the price you will pay when that time gets here. Maisha yakianza kukuadabisha hakuna atakaye kutetea wala kuingilia hata awe anakupenda vipi na yupo tayari kwa namna gani kujitoa kukupigania.
Mjiandae kisaikolojia. Maumivu yake si ya ulimwengu huu.