Kuwatoa wanawake katika Utiifu kwa waume zao.
Hilo limewekwa naturally na Mungu, Mimi nitaweza wapi kulibadilisha?
Waambie wanaume wenzako wa play part zao, wakiwapenda na kuwaheshimu wake zao, utii ni sehemu ya maumbile yao. Unakuja tu Kama utelezi kwa umpendae.
Vitabu vitakatifu vya dini kuu mbili duniani uislamu na ukristo
Maybe duniani ya Tanzania lakini Kama ni nje ya mipaka ya TZ, basi unayo kazi kubwa ya kujielimisha.
vimekubaliana katika majukumu na Nafasi ya mwanamke na Mwanaume katika jamii.
Niliposema tangu kuumbwa kwa Mfumo Dume ulielewa nini?
A council of men seating down and deciding on how to manipulate and turn women to be their sex slaves & house maids instead of fair human partners like the creator intended it?!?
Eti walikubaliana?! Unakaa chini kuamua matumizi ya maisha ya kiumbe kilichoumbwa independently along side You?!
Mwanamke ni mlezi wa familia katika kuchunga mali na watoto na mwanaume ni Kiongozi wa familia na breadwinner wa familia.
Niambie karne za bibi zetu na mama zetu kufanya haya na mengi zaidi ni Yapi yalikua malipo yao?
Wengi waliambulia kupandishwa vyeo na kuwa wake wakubwa na bado hata hizo mali unazozisema wapo billions of women walioko chini ya ardhi wameondoka bila hata kuzionja.
Tunaweza tukaqoute maandiko kama utayahitaji.
ipo siku hawa mnaowaita Feminists wataenda a step ahead na kuandika nao “Maono” yao kutoka kwa Mungu, Dunia imeamua kuzunguka upande wao kwa sasa hatujui wataishia wapi!
Mjiandae kulia zaidi.
Kama huamini katika hizo Dini pia sema tujadili kwa upande Mwengine.
Speculating much?!
Pia wewe ufahamu kuwa kuna mambo yapo duniani kama zao la mwanadamu (manmade) na mengine yapo kwa mujibu wa nature(maumbile na mazingira) Sio kila kilichopo hapa duniani katika mifumo ya maisha ya binadamu kimetengenezwa na binadamu. Bali kuna mchango wa nature. sisi tunaamua kufuata au kwenda against.
Nalitambua hili kwa asilimia 100!
Ila linafanya kazi zaidi ikiwa kila mmoja kati yetu atakubali kusimama na kuchukua majukumu yake head on bila kulalama na kuumiza wengine in the process Kisa tu jinsia tofauti!
Usichokielewa hili ni swala la kijamii na jamii Tunaishi nayo kila siku Mitaani.
Nami pia ni sehemu ya hiyo jamii, naelewa sana na ninatambua uhalisia kwa maana Mimi pia ni Mwanamke.
Athari chanya au hasi zinaonekana. Labda utuambie wewe Mwanamke athari chanya za Hizo itikadi zenu ni zipi katika jamii jaribu kusema pia na athari hasi kama unahisi zipo.
Narudia tena, ni mwanamke tu ndio ataelewa mateso na raha anazopitia mwanamke, Kama ilivyo kwenu ninyi wanaume, shida na raha zenu mnazitambua wenyewe na mnachagua wa kumshirikisha, na mara nyingi sio mke/mwenza.
Kwa mwanamke ni tofauti, yeye raha zake na shida zake pamoja na kuzitambua mwenyewe lakini zina reflect kwenye jamii inayomzunguka kwa kizazi atakachozalisha/nurture.
Sasa ili zisiwepo reflection hasi basi tuangalie chanzo cha hizo stress zake, ni Nini? Ni Nani?
Tujifunze kuwajibika.
Sio kweli ninyi mna exaggerate mambo tena kwa kutumia rare cases ambazo hatuwezi kuhukumu jamii nzima ya kale kuwa wanaume walikuwa wanapiga wake zao sijui Wanawake walikuwa watumwa sio kweli.
Matokeo yapo kwenye resistance iliyowazi kwenye kizazi cha leo, na hayo matokeo ndio yametuweka mezani hapa.
Trauma inaishi through DNA, studies kibao zina prove that factor, sasa why tujifanye vipofu?
Hayo mambo yalikuwepo ndio ila sio katika jamii nzima.
Ungesimama pale pale uliposema kwa hakika kwamba hakuna kabisa, hakuna!
Utiifu wa Mwanamke kwa mwanaume ni zaidi ya Matakwa ya binadamu ni jambo la kiasili na ndio maana hata kama utakachukua kibenten uwe unakalisha,, kukutii wewe kwa asilimia mia ni ngumu bado ule uanaume wake utakataa.
Naungana na wewe kwa asilimia 100 na huko juu nimeshakwambia hivyo lakini bahati mbaya tuko nyakati za nipe nikupe, sasa huwezi kuomba utiifu wakati wewe hutoi Upendo wala japo heshima.
Bibi na babu zetu na hata sasa katika ndoa zenye maelewano sio kwamba wanawake hawana sauti bali kuna ile kila mtu kusimama sehemu yake.
Naam, hapa umezungumza lugha yangu. Nashukuru umenielewa.
Mwanamke amtii mume wake na mume ampende mkewe. Tatizo linaanza kama mwanamke akitaka kuvaa viatu vya mwanaume na ajione nae ana ndevu hapo ndio wanaume wanakuwa wakali wenye roho mbaya na ndoa inaishia hapo. Wanaume wana hulka ya asili ya kutawala na kutaka kusikilizwa.
Sasa huwezi kutaka kusikilizwa Kama wewe husikilizi, nyakati zimebadirika, watu wamepata sauti.
Haizuiliki ila it can be adapted na kugeuzwa in our own ways/cultures kuliko kuendelea kupambana na upepo.
Umesema kweli chanzo ni baadhi ya wanaume wanaowapa majukumu Wanawake kinyume na uwezo wao Na wanaoupa nguvu u feminism.
Hebu waulizeni wanaume wenzenu waliodumu kwenye ndoa za mke mmoja and they still stayed faithful, what they endure?!
What demons they had to fight to make it to where they are now?
Same question waulizwe wanawake.
HAPO MWANZO MLIANZA "TUKIWEZESHWA TUNAWEZA" ila sasa Mnaona ninyi mnaweza kwa sababu mnaweza.
Ni kweli wanawake wanaweza, na kadiri siku zinavyosonga wanazidi kuthibitisha kwamba wanaweza mno zaidi hata ya Baadhi ya wanaume. Ajabu!
Na ndio sababu ya hizi hasira na vilio kutoka kwa wavulana.
Nini shida ya huo mfumo unaouita Mfumo dume? Madhara yake ni yapi bainisha Mwanaume akiwa kiongozi na mwanamke akiwa anamtii mumewe kinatokea kipi kibaya?
Kizazi cha sasa ni matokeo ya huo Mfumo na wala sio Siri. Na hayo madhara ndio tunayazungumzia hapa sasa hivi.
Absolute power corrupted our men, sasa wanayaogopa matokeo ya matendo yao wenyewe.
Mwanaume alifanya na anaendelea Kufanya makosa kutumia jambo hili(kuupa nguvu u feminism )for political interests na kusahau kuwa Jamii inaenda shimoni.
Matendo ya hao wanaume kwenye jamii unayaona? Bila unafiki?
Feminism ni harakati za ukombozi wa mwanamke zilizoanza miaka ya 1800s baada ya Vuguvugu la Abolition of slave trade.
Harakati hizo zimegawanywa katika phase tatu muhimu first wave,, second,, third and sometimes fourth wave.
Zilianza harakati hizo kwa wanawake wa kizungu huko ulaya kudai haki ya kupiga kura ambapo walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura kwa wakati huo.
Sahihi.
Hilo lilipofauru likazaa mengine hadi kufikia hatua kusema hata haya majukumu ya kijamii ni BATILI na wameyaweka Wanaume ili wawakandamize wanawake so Wanawake nao watoke wakahangaike kwani haki ni sawa.
Sioni uwongo hapa.
Hili jambo limekuja miaka mingi sana tangu Harakati hizo kuanzishwa.
Na wanasema baadhi ya waandishi kama wale walioanzisha hizi harakati wakija kujulishwa zilipofika harakati hizo hata wao wenyewe watashangaa. Kwa sababu malengo hayakuwa kumfanya mwanaume na mwanamke ni sawa katika majukumu.
Bado unapinda pinda kwenye maana halisi ya feminism na lengo kusudiwa.
Malengo yakiwa ni kutafuta matokeo chanya inakuwaje jambo zima lawama atupiwe mlengwa wakati yeye hawajibiki kwenye tafsiri na mapokeo ya jambo hilo kwa jamii mbali mbali kulingana na mila na desturi zao?
Kuna kengine kipya??
Hili ni jambo lengine kabisa.
Mambo mabaya katika jamii kama hayo uliyoyataja hakuna anayeyafurahia na yanapaswa kukemewa vikali ila halifanyi kuondoa dhana ya Utiifu wa mwanamke kwa mwanaume.
Hayo mambo unayosema yanapaswa yakemewe ndio kiini haswa cha Tatizo kwa ujumla.
Yanatakiwa yakomeshwe! Mwanaume mshenzi na mchafu ni laana kwa jamii yake!!
Ni lazima Kama jamii tukubali kuwajibika kwa madhira tunayosababisha in pursuit ya Starehe zetu.
Na wanaume watambue kwamba with great power comes great responsibilities.
Sio tu waitake fahari ya kuwa kichwa cha family huku matendo yakiwa ya teenage boy alietoka boarding school!
Mwanaume kutoonyesha upendo katika familia yake ni kosa na pia kuto muheshimu ni kosa na zipo hatua za kufatwa katika hali hiyo.
Kwamba, msingi wa suluhisho la kilio chenu ni jambo linalohitaji upembuzi yakinifu na tume ya uchunguzi?
Wanaume, kumbukeni real and benefiting brotherhood ni pamoja na kusimamia misingi ya jamii zenu wenyewe kwanza.
Sasa endeleeni kuendekeza ngono, Mtaa mzima unajisifu kutembea na wake/mademu wa washkaji zako unasahau kanuni kuu ya ulimwengu ni Mzunguko, liendalo laja upya!
lakini hilo halifanyi Wanawake wakatae utiifu katika jamii kwa sababu hiyo.
Nani atakubali kumtii mwanaume mfano wa vijana hawa wa sasa?
Matusi na kejeli zao juu ya wanawake humu ndani ni picha halisi japo kwa unusu wa kile haswa kinachoendelea kwenye maisha nje ya mtandao.
A “the battle of the Sexes, and the worst is yet to come njia zisipobadirishwa.
Hayo yametoka wapi?? Wanawake muwe makini na wanaume wasio na malengo Ukiingia tamaa ya pesa au u handsome usije kulalamika baadae ni akili yako hiyo.
Sawa na hapo hapo mnataka wawe watiifu.
Wanaume ongeeni kwenye vikao vyenu maisha ni zaidi ya ngono vinginevyo Segere halisi linakuja.
Mwanaume asiye timiza majukumu yake sio kwamba hastahili kutiiwa bali hastahili kuwa na Familia kabisa.
Ndio mukanyane wenyewe Kama mnavyowatupia wanawake mzigo wa malezi ya mabinti.
Unaweza usione uhusiano ila Nimekwambia idea za kifeminism zinaharibu ndoa nyingi.
Tafsiri ya mtu juu ya kitu mpaka kupelekea kupata matokeo hasi sio kosa la hicho kitu.
Elimu zitolewe kuanzia majumbani na sio malalamiko na vilio mtandaoni.
Ni matusi wanaume kulialia hovyo!
Hivyo malezi pia yanayumba katika jamii. Watoto wa kiume wanaolelewa na Single Mothers wapo hatari sana kuingia kwenye ushoga kama sio umarioo.
Hao single mothers hawakupata mimba za miujiza kiasi wahusika na wabeba majukumu wasahaulike kwenye mgao wa lawama.
Kibaya zaidi ni hao hao sperm donors ndio wataalamu wa kuvunja watoto wa watu viuno kwa kufanya ngono kwa njia ya haja kubwa!
Nyoka anatafuna mkia wake?! Mwisho ukoje?!
Jamii ipi inaruhusu uzinzi??
Angalia jamii iliyokuzunguka, wala sio Siri.
Tuambie na wewe kwa uelewa wako.
Mwanamke ajitunze na atunze usichana wake hadi aingie ndani ya ndoa na akiingia atulie na mumewe aache Kutengeneza ligi na mumewe.
Turudi wote kwa pamoja huko kwenye misingi ya uumbwaji wetu na kusudio la uwepo wetu.
Ngono kabla ya Ndoa ni haramu kwa binaadam mwanamke na binaadam mwanaume. MUNGU HANA UPENDELEO.
Single mothers watapungua sana.
Sana, wanaume wakianza kuchukua majukumu yao na kuacha kukojoa hovyo na kufuata misingi ya utu na heshima.
Wanaume wa hovyo wapo katika jamii hatukatai. Tatizo ni wanawake katika rika la usichana huwa wanavutiwa sana hao wanaume akitokea mtu serious anataka kuoa anaona bado aendelee kula ujana hilo nalo ni tatizo.
Only a boy can give such a weak excuse!
Mwanaume wa miaka 50 anaweza kuoa binti wa 25 na wakapata watoto kama kawaida.
Na hili ndio ninalosema! Ni jamii ya hovyo tu ndio itaona ni sahihi baba/babu kumvua nguo binti umri Sawa na mjukuu wake na kumtungisha mimba, simply because He can! Pathetic!
Vipi Bibi wa miaka 50 na kijana wa 25 nao wanajenga familia?
Sasa ninyi na Mfumo Dume wenu mumefanikiwa kutufikisha hapa kwenye haya mapinduko ya dunia na jamii yake, unashangaa nini?
Mwanamke ni binaadam na huyo benten naë binaadam tu, sasa unachodhani kitawazuia nini wao nao kutamani hayo ya babu na binti yake?
Usitumie makosa ya wachache kuupinga mfumo mzima hilo ndio tatizo lenu feminists.
Tumefanikiwa kufika mpaka hapa bila kubandikana labels, Tafadhali stay in your Lane.
Kwani mnavyowalaumu humu halaiki nzima ya wanawake wote ni kwamba wote tumeoza that much?
Sio kweli ninyi wanawake hata katika hizo Harakati zenu za ki Feminism mnawategemea kwa kiasi kikubwa Wanaume (wanaume wajinga)
Unayo mifano halisi ama ushahidi juu ya hili?
Unazo taarifa za maendeleo na hatua za wanawake mbali mbali walioshika usukani wa maisha na ndoto zao nje ya mipaka ya Tanzania? Na hapo Tanzania je?
Jielimishe.
hakuna jambo watakalo achiwa Wanawake pekee yao likawa na muelekeo wa kudumu.
Jitahidi sana kujielimisha kuhusu wanawake, inasikitisha kusoma hayo kwa mtu unaejinasibu kutambua haki na batili.
Mumeanza lini kusaidia wanawake kubeba mimba??
Hapa ndio tunaposema mnapotosha jamii.
Huo ni mtazamo wako (wenu?!), sio dhambi.
Lini ilikuwa waliokuwa wanaolewa ni wengi kuliko single?
Sina takwimu za ndoa na usimbe Tanzania hii ila experience ya family, ndugu, jamaa na marafiki (hata majirani na jamii kwa ujumla) ina majibu mengi na bahati Nzuri sana (mbaya kwako?!) haipo static, we are all Humans after all.