Ikifika wakati unaomba nafasi ya mwisho basi jiandae Kisaikolojia kuanza Maisha bila yeye

Ikifika wakati unaomba nafasi ya mwisho basi jiandae Kisaikolojia kuanza Maisha bila yeye

but why

Member
Joined
Nov 18, 2020
Posts
27
Reaction score
161
Kuna binti tulikuwa na mahusiano, yalikuwa yanaenda vizur tu baadae mapicha picha yakaanza, mwanzoni nilihisi mimi ndio ninazingua maana kila argument ikitokea shida inarudi kwangu, nisichokijua kumbe napigishwa shoti kimkakati

Kila mabishano yakitokea yale yote niliyowahi kukosea nyuma yanarudishwa halafu anajiposition kama victim naishia kuomba msamaha, nakiri sikuwah kupenda vile kabla, hiyo ilinifanya nisitake kumkosea.

Kadri nilivyozidisha jitihada za kumjali na kumuonyesha nampenda ndio kama nilikuwa nazidi kumsogeza mbali na kutafutiwa makosa zaidi, nilipochoka na ile hali nikakaa naye chini kumuuliza nini shida yakarudishwa makosa yale yale ya zamani nikafanya kosa lile wazungu wanaita "rookie mistake" kuomba nafasi ya mwisho moyon mwake ili nimuonyeshe kwanini namdeserve, kwamba ikitokea nimezingua tena nisisamehewe tena hahah

Of course niligeuka mtumwa kwa muda hadi ukikaa peke yako unawaza mbona huyu sio mimi, at last mahusiano yaliisha lakini yalinifunza mengi, kubwa ni kuwa ukiona inafika hatua unaomba last chance ujue mnaelekea ukingoni wa mahusiano ujiandae maisha mengine bila yeye kwa maana kama binadamu utamkosea tu na tayar ulishampa ticket mkononi.
 
Ukiona unaomba last chance ujue ni chance ya kuwa mchepuko
 
Mwenye Kupenda Haoni Chongo Atasema Kengeza
UUngeijaza Dunia Kupitia Mimba
 
Umefanya ulichoweza, kama kashindwa kukupenda na kutambua upendo wake kwako..!! Let her go!

Mademu tuko wengi, mi mwenyewe niko single njoo unipende..!! 😹😹😹
 
Back
Top Bottom