Ikitokea Ghafla Ukakutana na Mh Raisi Magufuli

Mie ningeuliza style yake ya kuongea anapindisha shingo upande na anachapa mikono hewani kwa msisitizo mtoto wake yupi karithi?
 
Ningemshauri kwamba achunguze mali za kila mkuu wa idara na taasisi.
Kuanzia mawaziri ,makatibu wakuu,wakuu wa majeshi,wakuu wa mikoa na wilaya.
Na wakurugenzi wote wa mashirika mbalimbali nchini.
Kwa sababu hawa wengi wao ndio. waliofilisi hii nchi kwa awamu tofauti tofauti na kujinufausha sana. Hata migogoro ya ardhi na kufa kwa viwanda wengi wamechangia.
Hawa ndio walioua mfumo wetu wa elimu na kujenga mashule yao binafsi.
Hawa ndio waliokua wanaingia tenda za kuchapisha vitabu vya kufundishia mashuleni na kubadili vitabu kila mwaka na kuharibu mfumo wa ufundishaji na usomaji.
Hawa ndio majipu makuu kwenye taifa hili.
Wameharibu hii nchi kwa maksudi na sasa wanakuja kama malaika wa nuru wa kuwakomboa watanzania. Hawana nia njema kwa taifa letu kwani miaka yote walikua na nia ovu.

Kila atakayebainika kuwa na mali nyingi kupitiliza na zisizo halali basi akae tu pembeni na kuachia kizazi kingine chenye nia njema na taifa letu. Vinginevyo awaombe wale walioliibia taifa hili wajitokeze na kurudisha vile walivyoiba bila hata riba.

Hawa waliokwapua kwenye serikali hawataweza kufanya kazi kwa haki kwani wanamuingiliano na mgongano wa kimaslahi kila kona ya nchi.
 
1) Ilikuwaje Jeska alifika chuo kikuu?
2) ulisema Hapa Kazi tu mbona sijapata hio kazi mpaka leo.
3) Najua wakati wa kampeni uliogopa kupanda chopa sasa na ndege pia unaiogopa?
 
Kwa Kuwa Watz wengi tunalalamika sana ama kusengenya sana

Ukikutana na Rais Magufuli Utamuuliza swali gani?

au utamwambia nini cha maana kwake na kwa Taifa?
Ningemuambia aliposhikilia asiachie maana heshima imeanza kurudi mtaani huku.
 
hata
watumishi wa taasisi nyeti kama TRA Bandari etc
 
imeenda
1) Ilikuwaje Jeska alifika chuo kikuu?
2) ulisema Hapa Kazi tu mbona sijapata hio kazi mpaka leo.
3) Najua wakati wa kampeni uliogopa kupanda chopa sasa na ndege pia unaiogopa?
shule hii
 

Na mimi ningemuuliza swali hilo hilo. Aingii akilini kwa jinsi alivyoongelea tatizo la UDOM. Kama kweli mwanae ana matokeo hayo na yuko hapo UDOM anawezaje kutumia neno la VILAZA????
 
Tuacheni mizaha. JPM anapita humu na anasoma hivi vitu...Mimi namuuliza hivi:

1) Hivi dhamira haimsuti hata kidogo kila akijiuliza kwa nini alipiga kimya wakati anaona kabisa Jecha na wahuni wenzie wanapora uchaguzi wa Zanzibar?

2) Ni lini exactly ataanza kudeal na majipu ya ukweli (wizi mkubwa kwenye migodi yetu, unyonyaji wa kutisha kwenye mikataba tata kama Symbion etc) badala ya kudeal na ''petty'' issues kama kuzuia posho ndogondogo za vikao kwenye ofisi za umma?

3) Akiwa kiongozi aliyejipambanua kwamba atatumbua majipu kwa nguvu zote, kwa nini anajaribu (na anaelekea kushinda with flying colours...) kuliziba bunge mdomo huku akijua Bunge live na lenye makali lingemsaidia sana kujua majipu yamejificha wapi ili ayafuate na kuyatumbua kwa uwazi?

4) Anaweza kupata ujasiri wa kuitupilia mbali rasimu ya katiba iliyoletwa na wanaCCM na kuirudisha ile ya akina Warioba ili mchakato uanze upya? if yes, lini hili linaweza kufanyika?
 
Ningependa sana kusikia kutoka kwake kwamba ni kweli ishu ya sukari imemshinda kabisa na kama la nini mtazamo na uwamuzi wake juu ya hilo.
 
Kwanza nitampongeza kwa kazi nzuri ya kuwatumbua wasiokuwa na uzalendo na nchi yetu hasa waliopewa majukumu ya kulitumikia taifa katika mashirika ya umma lakini wanajinufaisha binafsi. Pili ningemshauri arudishe katiba ya warioba kwani ndio mwarobaini wa wala rushwa.
 
Wewe umejoin leo unaleta kujua! Tulia uone veteran wanasemaje! Unajuaje kuwa hawana uzalendo? Una ushahidi?
 
nimeipenda hii
ya Katiba ya Warioba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…