Wadau hamjamboni nyote?
Hakuna ajuaye ya kesho na mipango ya Mungu siyo mipango ya mwanadamu
Ni kuhusu Mheshimiwa Paulo Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa sasa.
Naomba maoni yenu kuhusu mambo kumi (10) ya kipaumbele unayopendekeza Mheshimiwa Makonda aanze nayo miaka ijayo ikitokea akachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Karibuni kwa maoni
Usiku mwema wenye baraka tele Ndugu zangu
Jambo la kwanza . Ajenge Masoko ya Kimataifa Kwenye Wilaya zote zilizopo Mpakani.
Wala hayahitaji gharama kubwa za kuanzia bali yanahitaji uaminifu.
Anagitaji watu waaminifu tu kusimamia utekelezaji wake.
Masoko hayo yawe maalumu kwa wakulima wadogo na wafanyabiashara wa kati wa ndani wa mazao kuuza mazao yao kwa wateja kutoka nchi jirani.
Aondoe Ukiritimba wa kakundi kadogo ka watu matapeli kuagiza mafuta ya petrol. Uangizwaji wa Petrol uwe ni huria kama zilivyo bidhaa nyingine. Huu utaratibu wa kishetani wa kuwafanya wahuni na majizi wachache kuagiza mafuta unaiyumbisha serikali na kujenga rushwa kubwa na ujanja mwingi wa kupandisha soko la Mafuta.
Kama Biashara ni huria basi iwe kwa bidhaa zote kuondosha vikundi vidogo vya watu kihodhi uchumi na kutengeneza urasimu ule ule ambao ungeweza kulalamikiwa endapo ungefanywa na serikali .
Hawa wahuni wanaoagiza mafuta wameshindwa kuagiza na kuweka bei ya mafuta kuwa stable hata kwa mwezi mmoja . Wanapandisha mafuta kwa sababu ya kujifungamanisha na nchi za magharibi hasa Marekani na maswahiba wao wa Kiarabu waliojitengenezea Pepo zao na familia zao bila kujali watu maskini .
Na kuangalia upya suala la Ewura na nani hasa ananufaika na hii taasisi wakati tuna TBS.
Soko liwe huria kweli kweli. Anaxetaka kuagiza toka Urusi ruksa , Toka Venezuela ruksa , toka Irani Ruksa, toka Libya ruksa. Alimradi pawe na soko la ushindani wa haki sio kunyonya wananchi na kunufaisha watu wachache ambao hata ungewapa ufalme wote wa Mungu huko mbinguni bado wangetaka na kiti cha Enzi wakikalie. Kifupi ni watoto wa shetani.
Jambo la tatu ahakikishe suala la Ushuru kwenye stendi zote za mabasi linafanywa na Watumishi wa Halmashauri. Unatoaje tenda kwa mtu binasfsi kwenye sehemu rahisi kama hii ya kukusanya mapato? Yaani ni kiasi cha kufunga Kamera ya kuhesabu mabasi ya nayoingia ma kutoka stendi kila siku na kujua kwa siku unakusanya shingapi na sio kujenga stend kwa mabilioni ya pesa kisha unatafuta wajanja wajanja wanaopeana tenda kwa Rushwa halafu anakusanya pesa za mabasi mia tano anakuletea pesa za mabasi mia moja. Mia nne zinalishia mifukoni mwa watu.
Serikali inabaki na kazi ya kkukarabati stend kila siku . Hivyo hata kwa karne nzima serikali haiwezi kamwe kurudisha gharama za ujenzi wa Stend zake zinazojengwa kwa mabilion ya pesa. Tumakusanyo tunarudi kwenye ukarabati.
Kupunguza ushuru wa magari chakavu au usedi toka Ulaya .
Ni mbinu mpya yagu mimi 1000 digits kurudisha na kurecycle madini yetu ya Chuma ,shaba na platinum. Hii itatupatia unafuu mkubwa wa upatikanaji wa Chuma chakavu kwenye viwanda vyetu kutengeneza nondo na vyuma vingine lakini pia kupata shaba ,platinum na hata alminium.
Hii tunaitumia kama mkakati wetu wa kurudisha chuma Nyumbani kupata unafuu kwenye material ya kutengeneza nondo.
Hili suala la kupandisha ushuru wa magari chakavu halifai mana linaangalia upande mmoja tu wa propaganda kuwa linaharibu mazingira wakati kwa sasa hakuna chuma wala plastiki wala shaba wala kitu chochote kinachotupwa bali vyote ni mali na ni malighafi inayojitajika kuzalisha bidhaa mpya kwa ajili ya matumizi mengine.
Hii sheria ya kuzuia magari Chakavu au kuyapandishia ushuru na kodi kubwa ndiyo iliyochakaa na kupitwa na wakati . Ilitungwa wakati huo ambao hapakua na biashara ya chuma chakavu na viwanda vya kuzalisha bidhaa kama Nondo na alminium.
Jambo la lingine ni Kupunguza au kuondoa kabisa baadhi ya matumizi ya serikali yanayowahusu wateule. Watumishi wote wa umma watafanya kazi ya kuwatumikia wananchi na sio kutumikiwa na wananchi na kujiona miungu watu huku wananchi wakiwa wanaumizwa na maisha magumu.
Mfano. Unanunua magari ya kifahari kwa watendaji wa serikali halafu wanaenda kusimamia na kupora pesa wanayoiita kodi au ushuru kwa wananchi maskini wasiokua hata na baskeli. Huu ni ushetani!!!
Uiiteuliwa haki yako itakua ni mshahara mkubwa kuliko kule jalalani ulipokua basi ili upate mahitaji yako kwa wepesi na familia yako . Pia tutakupatia usafiri wa kawaida Kama RAV4, Suzuki kwa Wale wa mijini. Wale wa vijijini watapewa Toyota Land Cruiser Hard top. Huu ushetani wa kumteua mtu kutoka jalalani ambapo alikua anatembelea ki iST halafu anageuka na kuanza kusema kuwa hadhi yake ni kutembekea VX V8 au Lexus ni Ushetani. Ni yale yale ya shetani baada ya kufika mbinguni akataka kuwa juu na kupata ufahari wote. Mungu hakupendezwa na kiburi cha shetani na kusahau kuwa alikotoka. Katokeo yake Mungu alimfukuzilia mbali.
Leo Mkuu wa nchi anamteua mtu halafu anampa uhuru wa kupendekeza na kujigharamikia gharama kubwa ya kuvuruga uchumi wa nchi kwa mambo ya kifahari wakati hospitalini hakuna dawa. Taifa la Viongozi wa matumizi na ufahari.
Atakayetaka gari la kifahari serikali itamkopesha kama ilivyo kwa wabunge. Hii ni kwa wote mpaka Majaji .
Tunataka viongozi waadilifu sio wenye ufahari na wapenda starehe . Timekua na wimbi kubwa la watawala na viongozi na wakuu wa Idara hasa wateuliwa ambao ni wapenda anasa . Hata wakiwa maofisini wanawaza muda wa kazi uishe wakanywe pombe na wanawake na wanaume . Siku hizi mpaka wanawake wamegeuka kuwa walevi na wapenda starehe na kujirusha ndio maana hawakai ofisini wale hawapendi kuwahudumia wananchi.
Wakuu wa mikoa na wilaya wengi hawapenda anavyofanya makonda kwa sababu muda mwingi wanatamani wautumie kwenye starehe. Na hili ni janga lingine lililoletwa na kile kizazi cha watu waliosoma Urusi na Ulaya bila kujua kuwa kule hali ya hewa ni baridi sana ndio maana wanakua wanywaji sana wa pombe.
Uteuzi uzingatie namna bora ya kuweza kudhibiti matumizi ya fedha na mali za umma. Wapenda anasa wakafanye biashara tutawapa mitaji na riba nafuu kwenye mikopo lakini sio ofisi za umma.
Pia Endapo Mtu yeyote mzalendo kama Lisu , akiingia madarakani basi suala la Ardhi kuwapa wageni liwe ni kama kuwapa wageni Ikulu.
Amani ya nchi yetu ni kwa Sababu ya ardhi.
Hawa mawakala wa Vita na wapenda vita wanafanya makusudi kabisa kuuza ardhi yetu kwa lengo la kuivuruga nchi na kuleta mgawanyiko ili waje wabebe madini na radilimali zetu kama kule kongo.
Iko hivi : Wanufaika wakubwa wa kuuza ardhi kwa wageni ni Watawala wa CCM na makada wao . Lakini pia Waathirika wakubwa wa Kuuza aridhi ni Chama cha Mapinduzi kama chama kwa sababu amani ya nchi ni kwa sababu kuna watu zaidi ya 70% ya watu wanaishi vijijini na ajira yao ni kilimo . Hawa hawana habari na vyama vingine kwa sababu hawategemei pesa yoyote kutoka serikalini katika kuendesha maisha yao duni yanayotegemea kilimo cha jembe la mikono na kuongeza vishamba vyo huko maporini kwenye ardhi kubwa waliyopewa na baba yao aliyeko Mbinguni na mfalme na Bwana wa wote. Sasa anapokuja mtu akaiuza ardhi hii basi anawanyima watoto wa Watanzania kwa mamilioni kukosa maeneo ya kulima mashamba yao binafsi hivyo kuwafanya wategemee ajira kwa Makabaila na mabepari wachache. Panakua na mkusanyiko wa watu wengi kwenye shamba la mtu mmoja ambaye atakua ndiye anayepanga maslahi ya wengi. Pakitokea hamasa za kisiasa na vuguvugu la maandamano hawa watu wataandamana mana hawana cha kuwaweka bize zaidi ya kudai nyongeza za mishahra . Ukitishia kuwafukiza watachoma moto mashamba na mali za Wale wanaowanyonya. Migomo na vurugu zitakua ni kama Afrika kusini.
Lakini watu wenye ardhi hawakubali kupoteza muda wao kufanya vurugu wakati mvua inakaribia na wasipolima au kupanda au kupalilia au kuvuna au kutunza mazao yao . Hapa ndipo Baba wa Taifa hili aliona Mbali akataifisha ardhi yote ya Wanyonyaji na kuifanya iwe ni mali ya umma.
Hapo wenye nia njema na amani yetu ,uhuru wetu na umoja wetu watajua Watawala wa leo wanapotupeleka na sijui kwa nini wameamua kuharakisha kutupeleka huko?
2025 tuwaondoe kabla hawajatufikisha huko mazima.
Nchi hii ina amani kwa sababu ya misingi yake iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere na sio kwa sababu ya vyombo vya Dola peke yake. Hata Kongo palikua na vyombo vya dola.