Ikitokea wachezaji 20 wa Yanga wanavunja mikataba katikati ya ligi. Itakuwaje?

Ikitokea wachezaji 20 wa Yanga wanavunja mikataba katikati ya ligi. Itakuwaje?

Mwanasheria na Wakili msomi kashasema kijana ana haki ya kukataa kufanya kazi, jamani maajabu hayaishi kwenye hii nchi
 
Nilivyomsikiliza Fatuma Karume nikaamini kwamba tuna wanasheria vilaza... nilimshusha nyota... wanasheria wanaweza mpoteza mtu hivi hivi and then wanakwambia ndio mteja wao anavyotaka wakat wanampa ushauri wa ajabu.

Tujifunze kitu hapa hata kama unaajili Mwanasheria ila akili yako ndio inatakiwa kufanya kazi zaid yake coz mwathirika sio Mwanasheria ila ni wewe mwenyewe.

Akili zake changanya na zako kisha fanya maamuzi ambayo yataku favour wewe
 
You're missing the point, at this point Yanga haina shida na Fei ila inafuata matakwa ya mkataba na kumkomoa which I rightly support...
Hili linaeleweka. Ila Fei kutokwenda mbele au kurudi nyuma akiwa ni mchezaji wa Yanga, kuna faida gani kwa Yanga?
 
Fatma Karume na mpira wapi na wapi.

Hata hao wanasheria wa Yanga nao wanaonekana ovyo.

Kwanza kwa kanuni za FIFA ni illegal team nyingine kuongea na mchezaji aliye kwenye mkataba au mwakilishi wake; bila ya kuongea na club husika kwanza kama wapo interested kumuuza huyo mchezaji.

Yanga wangesema hawapo interest story inaishia hapo.

Yanga wangepeleka malalamiko yao kwenye shirikisho la mpira nchi ambayo club inayotaka kumsajili Fei Toto sasa hivi wangekuwa washalipwa hela ndefu, kwa kuingilia mkataba wa mchezaji na kuzuiwa kumsajili ata akinunua mkataba wake atoke yanga.

Mambo mengine ata sijui yanakuwaje mzozo wa muda mrefu Tanzania, kwengine sasa hivi kama Fei Toto ataki kucheza na kwa kuwa bado yupo chini ya Yanga wangeweza ata kutomlipa mshahara kama adhabu na hakuna kitu angeweza fanya.
 
Hili linaeleweka. Ila Fei kutokwenda mbele au kurudi nyuma akiwa ni mchezaji wa Yanga, kuna faida gani kwa Yanga?

Hakuna faida. Nani anayeumia?
 
Fatma Karume na mpira wapi na wapi.

Hata hao wanasheria wa Yanga nao wanaonekana ovyo...
Sasa wewe una ufahamu wa mambo haya. Embu wanayanga watusaidie, kwa nini wanaendelea kumlipa mshahara na hawajamuadhibu mchezaji ambaye amegoma kucheza?

Halafu juzi juzi baada tu ya game, Hersi alizungumza na mchezaji wa TP Mazembe na kumwambia wangependa aje achezee Yanga.
 
Sasa wewe una ufahamu wa mambo haya. Embu wanayanga watusaidie, kwa nini wanaendelea kumlipa mshahara na hawajamuadhibu mchezaji ambaye amegoma kucheza...
We ulisikia maneno waliyokuwa wakiongea au ndio unadakia tu hadithi za mtandaoni
 
Wanao pinga hili la feisal.

Hawajawah dhulumiwa alf wakaenda polis wakaambiwa hii ishu n makubaliano nenden mahakamani sababu hakukua na maandishi acha kbsa mkataba unaweza fanya upate haki za msingi
 
Sasa wewe una ufahamu wa mambo haya. Embu wanayanga watusaidie, kwa nini wanaendelea kumlipa mshahara na hawajamuadhibu mchezaji ambaye amegoma kucheza?

Halafu juzi juzi baada tu ya game, Hersi alizungumza na mchezaji wa TP Mazembe na kumwambia wangependa aje achezee Yanga.
Hayo sasa ni maamuzi yao ya ndani, lakini wakiamua kutomlipa ni sahihi kabisa.

Mara nyingi mikataba ya wachezaji huwa inaenda sambamba na uwepo wao kambini, kufanya mazoezi na kuwa tayari kucheza; usipotokea hiyo ni breach ambayo team inaweza kutokukulipa mshahara na bado ukawa chini ya mkataba.

Ukigoma kabisa kutokea na wenyewe wakiwa kichwa ngumu wanaweza kuendelea na wewe hivyo hivyo utokei na wao awakulipi mpaka mkataba wako unaisha.

Ni kama Cristiano Ronaldo na Manchester; mpaka walipofikia makubaliano ya pande mbili kuuvunja mkataba.

Kutamka ungependa kuona fulani anakuja kuchezea club yako mbele ya umma, sio sawa na kuongea nae nyuma ya pazia kwa namna ya kumshawishi aje kwenye club. Anyway club nyingine ata hilo jambo watatoa warning kama uchokozi lakini sio kosa la kupelekana kwenye sheria.
 
Kama wachezaji wana haki ya kuvunja mikataba wakati wowote, kuna uwezekano wa kutokea kitu cha ajabu sana. Swali ni je pale Yanga ikitokea wachezaji zaidi ya 20 wamepata deals nzuri na wameamua kuvunja mikataba yao (kama alivyojaribu Feisal), timu itaendelea na kushiriki mashinano?
Acha ndoto
 
Basi hiyo sheria inayoruhusu wachezaji kuvunja mikataba wakati ligi inaendelea ni ya kifala sana
Mpira ni ajira, siyo biashara ya utumwa. Kama mkataba wa ajira una kipengele cha kuvunja mkataba mwajiriwa ruksa kuvunja ilimradi akidhi masharti ya vile vipengele vinavyomruhusu kuvunja. Hata wakivunja wachezaji wote kama wamefata masharti ya hicho kipengele ni sawa.
 
Hakuna faida. Nani anayeumia?
Nia ya viongozi wa Yanga ni kuumiza pasipo faida? Au ni kiu yenu mashabiki kumuona akiumia sababu hawaitaji?
 
Nia ya viongozi wa Yanga ni kuumiza pasipo faida? Au ni kiu yenu mashabiki kumuona akiumia sababu hawaitaji?

Nia ya Yanga na TFF ni kufuata sheria na taratibu no more no less.
 
Mpira ni ajira, siyo biashara ya utumwa. Kama mkataba wa ajira una kipengele cha kuvunja mkataba mwajiriwa ruksa kuvunja ilimradi akidhi masharti ya vile vipengele vinavyomruhusu kuvunja. Hata wakivunja wachezaji wote kama wamefata masharti ya hicho kipengele ni sawa.
Na uvunjaji una taratibu zake, izi nguvu mgezitumia kumuimiza kufuata utaratibu mngekua mmemsaidia mno, tofauti ya hapo Hamna tofauti na wapotoshaji.

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
Nia ya Yanga na TFF ni kufuata sheria na taratibu no more no less.
Anayebaki ni yule anayesema atakaa benchi mpaka apotee. Kimtokacho mtu.
 
Back
Top Bottom