S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,689
- 7,145
IKIWA CDF, IGP NA CDI WATASEMA WALIFUATA AMRI: SWALI NI JE: AMRI HIYO ILITOLEWA NA NANI?
Hapa ndipo tunapaswa kutumia critical thinking, si hisia.
Kama CDF, IGP na CDI watatoa ushahidi kwamba walichofanya kilitokana na amri au maelekezo ya mamlaka ya juu, basi chanzo, maudhui na mlolongo wa amri hizo vinaweza kuwa masuala muhimu sana kwa utetezi.
Haiwezi kuwa sawa upande mmoja kuruhusiwa kusema:
“Tulikuwa tunatekeleza amri.”
Lakini mtuhumiwa anapotaka kuchunguza nani alitoa amri, amri ilikuwa nini, ilitolewa lini na nani alikuwa anajua nini, anaambiwa ushahidi huo ni irrelevant.
Hapo ndipo swali kubwa la haki ya kusikilizwa linapoibuka.
Twende kazi sasa: Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda haki ya mtu kusikilizwa kikamilifu, na mahakama za Tanzania zimesisitiza kwamba kunyimwa haki ya kusikilizwa kunaweza kuathiri uhalali wa mwenendo wa shauri. Sasa kama Jaji amesema kwamba Rais anaweza kuitwa, lakini ombi la utetezi kuhusu ushahidi wake linakataliwa, basi umma unastahili kuelewa msingi wa kisheria: Kwa nini ushahidi huo hauna relevance ikiwa utetezi unasema unahusiana moja kwa moja na mlolongo wa amri unaotajwa na mashahidi?
Na hoja hii inakuwa nzito zaidi kwa sababu tunazungumzia kesi ya uhaini. Chini ya kifungu cha 39 cha Penal Code, ambayo adhabu ya kifo. Hili si shtaka dogo ambalo mahakama inaweza kuruhusu mashaka kuhusu kama mtuhumiwa alipata nafasi halisi ya kujitetea.
Kama Serikali inataka mtu ahukumiwe kwa kosa linaloweza kupelekea adhabu ya kifo, basi haki yake ya kujitetea lazima ilindwe kwa kiwango cha juu kabisa.
Hatuwezi kusema:
“Anaweza kuhukumiwa kwa ushahidi wa watu wanaosema walifuata amri,”
halafu wakati huo huo tukazuia uchunguzi wa utetezi kuhusu chanzo cha hizo amri bila sababu madhubuti ya kisheria.
Na kama sheria inampa Rais kinga dhidi ya kulazimishwa kufika mahakamani, hilo nalo lielezwe wazi. Kinga ya shahidi fulani na relevance ya ushahidi anaoweza kuwa nao ni masuala mawili tofauti. Mahakama bado inapaswa kuhakikisha kwamba utaratibu unaotumika haumwachi mtuhumiwa bila njia ya haki ya kuwasilisha utetezi wake.
Kwa hiyo swali si: “Kwa nini Rais hajaitwa?”
Swali kubwa zaidi ni:
IKIWA MTUHUMIWA ANAKABILIWA NA ADHABU KALI KIASI HIKI- YAANI KIFO, JE, AMEPEWA NAFASI HALISI, KAMILI NA YA HAKI YA KUCHUNGUZA USHAHIDI, KUPINGA Mlolongo WA AMRI UNAODAIWA, NA KUWASILISHA MASHAHIDI WANAOWEZA KUUNGA MKONO UTETEZI WAKE?
Kama jibu ni hapana, basi tunakuwa na tatizo kubwa zaidi kuliko jina la shahidi mmoja.
Tunakuwa tunazungumzia uadilifu wa kesi yenyewe.
Haki ya kujitetea si mapambo ya Katiba.
Haki ya kusikilizwa si hisani ya Jaji.
Na katika kesi inayoweza kuamua kama mtu anaishi au anakufa, fair trial lazima iwe halisi, si maneno kwenye karatasi.
Haki haitakiwi tu kutendeka- lazima ionekane bila shaka kwamba imetendeka.