Ikiwa kama Wananchi wa Tanzania hawataki Katiba mpya, Maoni yaliyokusanywa na Tume ya Warioba yalitoka wapi?

Ikiwa kama Wananchi wa Tanzania hawataki Katiba mpya, Maoni yaliyokusanywa na Tume ya Warioba yalitoka wapi?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ccm wananchi wa Tanzania si wanaotaka Katiba mpya , bali Katiba mpya inatakiwa na wanasiasa ili watimize malengo yao, hii ndio kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo.

Swali langu ni hili, yale maoni ya Tume ya Warioba yaliyopelekwa kwenye Bunge la Katiba yalitoka kwa nani ? ikumbukwe kwamba Maoni yale ni ya wanachi nchi nzima, kwa maana ya bara na visiwani yalipelekwa kwenye bunge Maalum la Katiba lililoongozwa na Mwenyekiti wake Samuel Sitta na Makamu mwenyekiti akiwa Samia Suluhu Hassan ambaye sasa ndio Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.

Katibu Mkuu wa CCM anataka kutuaminisha kwamba Mchakato huu muhimu wa serikali ya awamu ya 4 ulikuwa mchakato Batili?
 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ccm wananchi wa Tanzania si wanaotaka Katiba mpya , bali Katiba mpya inatakiwa na wanasiasa ili watimize malengo yao, hii ndio kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo

Swali langu ni hili , yale maoni ya Tume ya Warioba yaliyopelekwa kwenye Bunge la Katiba yalitoka kwa nani ?
Yale yalikuwa ni maoni ya Tume.

Wananchi hawajawahi kuhitaji katiba ndio maana hata UKAWA ilikufa!
 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ccm wananchi wa Tanzania si wanaotaka Katiba mpya , bali Katiba mpya inatakiwa na wanasiasa ili watimize malengo yao, hii ndio kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo...
Yalitoka kwa WALIOKUWA wananchi wa Tanzania na sasa kuna wananchi wa Tanzania ambao hawadai katiba.
 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ccm wananchi wa Tanzania si wanaotaka Katiba mpya
Kwa maoni yangu naona ni sahihi alichosema katibu mkuu wa CCM(kama ni kweli alisema)
bali Katiba mpya inatakiwa na wanasiasa ili watimize malengo yao, hii ndio kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo
Ndio kwa sababu wanasiasa ndio wameanza kudai tena hoja kubwa ni tume huru ambayo wanadhani itawaweka madarakani.
yale maoni ya Tume ya Warioba yaliyopelekwa kwenye Bunge la Katiba yalitoka kwa nani ?
Hili ndio swali kubwa katika uzi wako,naomba nichangie katika kujibu kama ifuatavyo.

unatakiwa kufahamu kwamba kuna tofauti kati ya kuhitaji na kuchangia,wananchi walichangia kwa sababu fursa ilikuepo ya kuchangia maoni yao.

Ni kama vile ikija fursa ya waandishi wa habari wanahoji jambo lao wanakusanya maoni wannanchi watatoa maoni kwa sababu jambo limejileta lenyewe.

Kuja kwa waandishi wa habari kukusanya maoni kwenu mtaani alafu nyie mkachangia haimaanishi kwamba eti nyie ndio mlianza kudai jambo hilo.

Kwa hivyo kama fursa ilitokea ya wananchi kuchangia hiyo haina maana kwamba wao walianza kulidai.

Na pia unatakiwa ujue kwamba kutokulidai jambo haina maana kwamba halina faida,unaweza usilidai jambo lakini likawa na maslahi fulani.

Kwa hiyo mtoa mada haikuwa sahihi wananchi kususia kutoa maoni juu ya katika wakati fursa tayari ilikuwepo ya wao kuchangia.

Kwa mantiki hiyo katika suala hili hoja sio wananchi kuchangia bali hoja ni kwamba je wananchi walianza kudai katiba mpya ama fursa ya wao kuchangia ndio ilikuja wakaona wasiisusie.
 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ccm wananchi wa Tanzania si wanaotaka Katiba mpya , bali Katiba mpya inatakiwa na wanasiasa ili watimize malengo yao, hii ndio kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo...
Kwani ilifanyika kura ya maoni au warioba na kamati yake walikuja tu na mapendekezo yao. Kwenye bunge la katiba ndio kulikua na uwakilishi bunge likachuja warioba likaja na katiba ya kupigiwa kura na wananchi.
 
Niseme ukweli, mtaani kwangu cjawahi kusikia watu wakiongelea katiba mpya zaidi ya kuona hayo mambo mtandaoni
 
Ulitaka wananchi waonyeshe hisia gani ili ujue wanahitaji katiba ?
Hisia wanazozionesha kwenye kukataa chanjo ndizo ziwe mfano katika kudai katiba.

Kuna shule huko wazazi walienda shuleni kisa walisikia chanjo zimekuja shule.

Na wala hutosikia kuna wazazi wamegoma kupeleka watoto wao shule au wameenda shule kuandamana kisa hakuna katiba mpya inayoboresha elimu ya watoto wao,kwa maana hii bado hakuna hisia za katiba mpya kwa wananchi wa kawaida.

Leo vijijini wanaandika mabango shida zao,sijawahi kuona kijiji kimeandika bango kinasema eti wanataka katiba mpya,hii ni kuonesha wananchi wana shida nyingi za kutatuliwa kuliko katiba.

Mifano ni mimgi kuonesha kwamba wananchi hawahitajii katiba mpya kwa kiasi ambacho tunaaminishwa
 
Maoni ya Tume yalitoka wapi ?
Hata kama yalitoka kwa wananchi bado sio hoja kwamba wananchi walidai katiba.

.bila shaka maoni hayo wananchi walipewa fursa ya kutoa maoni na wananchi wakashiriki kutoa maoni.

Kama ambavyo mtu anaweza kuja kwako kutaka maoni juu ya jambo fulani utatoa malni kwa ssbsbu kakupa fursa,huwezi kususia fursa ya kutoa maoni.

Kwa hiyo hata kama maoni yalitoka kwa wananchi bado haiwi hoja yenye kutegemewa
 
Hebu tumia akili yako japo KIDUCHU badala ya kuonyesha ujuha wako hadharani!!! Uchaguzi huru ná wa haki ni muhimu kwa Mtanzania yoyote yule mwenye akili timamu na aliyechoshwa na uhuni wa maccm wakishirikiana na Tume feki ya uchaguzi na polisiccm.
1628707277365.jpeg

Kwa maoni yangu naona ni sahihi alichosema katibu mkuu wa CCM(kama ni kweli alisema)

Ndio kwa sababu wanasiasa ndio wameanza kudai tena hoja kubwa ni tume huru ambayo wanadhani itawaweka madarakani...
 
Niseme ukweli, mtaani kwangu cjawahi kusikia watu wakiongelea katiba mpya zaidi ya kuona hayo mambo mtandaoni
Haya mambo hapo mitandaoni tu humu,lakini mtaani watu wanalilia maji,umeme na vitu vingine kinyume na katiba
 
Uchaguzi huru ná wa haki ni muhimu kwa Mtanzania yoyote yule mwenye akili timamu
Nakubali lakini tume huru tayari ipo.

Kama unaona kuna shida Tatizo sio tume pengine ikawa tatizo ni wanaosimamia tume aidha wanafanya mambo kwa mahaba au kwa maslahi fulani.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Utakuwa na utindio wa ubongo wewe. Kama Tume Huru tayari ipo unadhani ni kwanini Mkapa mwaka jana wiki chache alitaka uchaguzi wa 2020 usimamiwe na Tume huru!?

Mkuu mkapa kwangu sio hoja,kitu akisema mkapa kwangu mimi SIO HOJA ya moja kwa moja ya kuninyamazisha.

Unaweza kunipa tafsiri ya tume huru ni ipi kwa mujibu wa huyo mkapa ?
 
Haya mambo hapo mitandaoni tu humu,lakini mtaani watu wanalilia maji,umeme na vitu vingine kinyume na katiba
Huo ndio ukweli, kuna wengine hapa watauliza tunaishi maeneo gani hayo ambayo hawazungumzii katiba na tukitaja tunapoishi bc watatuita kuwa mtaa mzima sisi ni wapumbavu ila hiyo haiondoi ukweli kwamba MTAANI HAKUNA ANAYEONGELEA KATIBA MPYA
 
Huo ndio ukweli ambao ni mchungu sana kwa wanaharakati uchwara.
 
Back
Top Bottom