Mkuu the
Big Eagle , kwanza asante kwa kutukumbusha "Mwandishi Huyu wa 1980s", kitendo cha kutomtaja ni mwandishi gani, wa wapi na maneno hayo aliyaandika wapi, sio tuu unakuwa hujawatendea haki wasomaji, bali unakuwa hukitendei haki, chombo chetu cha utoaji haki kwa ku insinuate kuwa uamuzi umeisha fanyika hivyo hii kesi ni kesi tuu ya kuuhalalisha, kitu ambacho sio kizuri.
P
Kwenye kesi ya Dumisani Dube Vs Republic, kwa kifo cha Skoine kwa ajali ya gari kule Morogoro, kesi ilikuwa hivi:
Siku ya kwanza, Mashitaka matano kwa Dumisani Dube yalitajwa mahakamani
Dumisani Dube alikataa kabisa kuhusika na - Kesi iliahirishwa
Mara ya pili Mashitaka yale yale yalitajwa Dumisani Dube akakubali Makosa Yote, na alihukumiwa miaka 5 jela..
Wananchi tulishangaa lakini tulikubali,
Baada ya miezi kadhaa, Dumisani Dube aliibukia London,
Ameishi huko hadi Africa Kusini inapata Uhuru, akarudi Africa Kusini, akapewa na cheo, kama nilisikia alifariki, labda nipekue tena.
Paskali, hii ndiyo Tanzania, "communist" kantri, uongo mwingi, laghai wengi, na hii ndiyo tabia CCM imetuhusisha, tutaamini kila kitu, kwa sababu kila kitu tunafanya kuaminishwa ingawa hatuamini.
Labda CCM ifutwe hapo baadaye, lakini uwepo wake hakuna mabadiriko yatakayotokea kwenye "mindset" ya waTangnganyika.
We fought JK, then Magu, now Samia; but we forget that these also are victims of the system, the system which they can manipulate to their advantages, WE have to fight CCM - The System providers