tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Jambo wakuu?
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Ni ukweli usiopingika kwamba makato kwenye miamala ya simu, LUKU na mabenki yanawaumiza kichwa wananchi wanyonge, hasa ukizingatia kwamba watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha kama Rais, Makmu wa Rais, Waziri mkuu, wabunge, mawaziri, majaji na TISS, maRC, maDC, nk wao hawakatwi hata senti moja kwenye mishahara na marupurupu yao.
Jambo jingine wasilolifahamu wananchi wengi ni kuwa, mbali na makato ya simu, serikali pia imeanza makato kwenye LUKU na kupitia kwenye mabenki. Juzi jamaa yangu mmoja alitoa Tsh 800,000 kwenye ATM ya benki moja hapa nchini akakatwa zaidi ya Tsh 24,000! Haya ni maumivu makubwa sana, hasa ukizingatia kwamba mtu unalipa PAYE lakini ukienda benki kuchukua fedha pia unakatwa, ukituma au kutoa pesa kwa simu unakatwa kodi ya miamala, ukinunua LUKU unakatwa na ukinunua sukari dukani unakatwa VAT kama kawaida. Yaani ni mzunguko wa makato hadi mwisho wa siku mtu unabaki huna kitu mfukoni. Sasa maisha haya yaliyojaa milolongo ya makato tunaishije?
Kana kwamba hilo halitoshi, serikali pia inaanda mkakati wa kukata kodi kwenye laini za simu kama ilivyofafanuliwa kwenye link hizo hapo chini:
Phone users brace for new Sim-card levy in August
New digital taxes: A test for economy
Kwa hali kama hii ndugu zangu watanzania tutaendeshaje maisha au tuhamie Burundi kama tulivyoshauriwa na mchumi msomi Dr Mwigulu Nchemba?
Na bado. Serikali yetu tukufu imepanga pia kuanza kukata kodi kwenye sadaka na matoleo ya kanisani na misikitini ili kutunisha zaidi mfuko wake wa maendeleo ya wabunge na serikali:
President Samia on taxation of religious institutions
Yaani unaambiwa kwamba hakuna kupumua; ukilala unakatwa, ukiamka unakatwa. Mbona hii sasa kero? Hata kama ni kuhamia Burundi, mbona nauli haitabaki?
Zamani LUKU tulikuwa tunanunua bure kwenye simu lakini sasa serikali ya Samia imeamua kuwakandamiza wanyonge kwa kukata kodi kila mtu anaponunua LUKU! Inashangaza na inasikitisha sana. Ikumbukwe kuwa mitandao ya simu iliamua kuweka huduma za ununuzi wa umeme kupitia simu ili kuwarahisishia maisha wananchi kama mojawapo ya huduma za bure, yaani Value Added Services (VAS). Serikali inapokuja kukamua kodi kwenye LUKU inawakatisha tamaa wanyonge na kuwafanya waishi kwenye nchi yao kama digidigi. Mkumbuke pia kwenye LUKU kuna kodi ya REA, EWURA na VAT. Hizi zote serikali imeona hazitoshi, imekuja kuongeza tozo mpya? Inauma sana.
Katika nchi za wenzetu, hapa hapa Afrika, wananchi wake wanajitambua sana. Hawakubali kuburuzwa na serikali kama nyumbu kwa masuala ya ajabuajabu yasiyokuwa na mwelekeo. Huko Ghana wananchi wamekataa mchele waliogawiwa na wabunge wao. Wamekataa kutumiwa kama daraja la wanasiasa kupandia uongozini.
Fikiria tukio kama hilo kama linawezekana kufanyika hapa nchini Tanzania. Haiwezekani. Watanzania wanaendekeza mno njaa.
Wakati tukiendelea kutafakari haya tukumbuke kwamba wabunge hawalipi kodi wala mafao yao hayakatwi kodi lakini wafanyakazi wengine wote wanakatwa kodi kwenye mishahara yao na mafao pia pindi wakistaafu. Suala la wabunge kukatwa kodi liliwahi kuibuka bungeni lakini wabunge walikuwa wakali kama mbogo:
Sasa kama wao hawataki kukatwa kodi katika mishahara yao ya Tsh 12,800,000 kwa mwezi pamoja na posho na marupurupu kibao watahalalishaje wakatwe wananchi tu, tena kwa nguvu? Hebu msikilize kinara wao anavyolazimisha wananchi wakatwe kodi kwa lazima:
Nini kifanyike?

- Nashauri wananchi twende mahakamani kuishitaki serikali kwa kuhujumu uchumi wa wanyonge huku wao wakiendelea kula bata kila kukicha. Kitendo cha serikali ya CCM kuwarundikia kodi wanyonge wakidai eti ni kodi ya kizalendo, ni upuuzi mtupu. Uzalendo gani huu unaoegemea upande mmoja tu?
- Vyeo vya kipumbavu kama vile Ukuu wa Mkoa na Wilaya vifutwe kwa kuwa havina tija kwa wananchi ili fedha zitazookolewa zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo. Wakurugenzi wanatosha kuendesha halmashauri. Tusitwishane mizigo isiyokuwa na tija.
- Wabunge wote waanze kukatwa kodi kwenye mishahara, mafao na posho zao.
- Serikali ibuni vyanzo vipya vya mapato kwenye kilimo, uvuvi na utalii badala ya kuwarundikia wanyonge kodi zote hizi.
Nawasilisha.