Ikiwa mmeshindwa kuishi pamoja si muachane kiungwanana tu

Ikiwa mmeshindwa kuishi pamoja si muachane kiungwanana tu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
kuelezea utu na haiba ya za ndani za mwenzi wako kwa matusi ya fedheha mbele za watu au kwa marafiki zako, na kufichua siri na madhaifu ya utu na heshima ya mwenzi wako khadharani sio ungwana na sio ustaarabu....

ulipokua nae uliweza kuvumilia, na kustahimiliana mengi sana miongoni mwenu.

leo hii mmetofautiana na mmeshindwana kuendelea kua pamoja, basi, yaishe kistaarabu na kila moja akatafute uelekeo anaoona unamfaa kwa majaaliwa yake Mungu, na kusonga mbele kwa amani...

hii ya kusindikizana kwa matusi ya nguoni ya aibu, na status za kuchokozana na za kuudhi mitandaoni zinachochea uhasama na uadui usiokoma kitu ambacho naona hakina maana wala umuhimu wowote....

mkikutana kimjini mjini, achaneni kimjini mjini, mkikutana kibongo bongo basi vile vile muachane kibongo bongo....

show love sio deal, haijawahi kuacha mahusiano, uchumba au ndoa salama 🐒
 
Mkuu toka nimefahamu matatizo ya akili kwenye jamii yetu yapo kwa kiwango kikubwa,kutokana na utamaduni wetu wakutokupenda kucheki afya zetu mara kwa mara , kila nikisikia hayo matukio ya ovyo kwenye mahusiano huwa ninayaunganisha na matokeo ya magonjwa ya akili.
 
Mkuu toka nimefahamu matatizo ya akili kwenye jamii yetu yapo kwa kiwango kikubwa,kutokana na utamaduni wetu wakutokupenda kucheki afya zetu mara kwa mara , kila nikisikia hayo matukio ya ovyo kwenye mahusiano huwa ninayaunganisha na matokeo ya magonjwa ya akili.
uko sahihi,
kulimbikiza mambo mengi usio na uwezo nayo na kuyahifadhi kuchwani na moyoni badala ya kutafuta suluhu ya mapema kunakufanya utengeneze bomu la mihemko, hasira na ghadabu ndani yako zitakazokuja kukuathiri wewe mwenyewe binafsi, tena ni kwasababu ya dosari, kasoro au changamoto ndogo sana 🐒

inashangaza sana watu wanakutana kwenye nyumba za ibada, wanapendana na kuanzisha, mahusiano uchumba, na hatimae ndoa halafu eti baadae simu ya mkononi kupitia meseji inawatenganisha..

kana kwamba simu inauwezo mkubwa mno kuliko utashi wao kiasi kwamba inaweza kuwatenganisha...🐒
 
Back
Top Bottom