Ikiwa mwajiri amegoma au kushindwa kukuingizia hela yako ya NSSF na tayari mkataba wako umeshaisha na mmeagana kwa amani nini hasa unabidi kufanya?

Mkuu mwanangu alikuwa private amepata kazi serikalin je anaweza kupewa michango yake ya nssf?
Hapana hawezi kupata mpaka astaafu au afukuzwe kazi na siyo ku resign. Hata kama huko private sector angekuwa alifuzwa basi angepata endapo tu angekuwa hajapata kazi sehemu nyingine. Napo angelipwa 33.3% ndani ya mwaka mmoja kwa miezi sita
 
Wakuu , naomba muongozo ni hatua gani sahihi za kuchukua endapo mwajiri hataki kukuwekea pesa yako NSSF na tayari mmeachana vizuri.

Umri wa mwajiriwa umeshafika 60 yrs

Ila mwajiri hataki kuingiza pesa NSSF?
Kuna jamaa yangu amesaidiwa juzi kupitia ukurasa wa instagram wa NSSF @nssftz mwambie atume huko taarifa zake muhimu kama namba ya uanachama na majina yake kamili pamoja na mahali alikuwa anafanyia kazi atapata msaada wa haraka
 
NSSF pesa zinalipwa monthly.. imekuwaje mwajiri mmeachana na bado hajaweka pesa?
Kwamba inawezekana kuvusha mwezi pasipo kupeleka michango? Na hawa staff wa NSSF wanaopiga doria maofisini kukagua risiti hard copies hawakumfikia mwajiri wako?
Kawaida sana. Makampuni binafsi mengi yanadaiwa hadi mabilioni.
 
Kuna jamaa yangu amesaidiwa juzi kupitia ukurasa wa instagram wa NSSF @nssftz mwambie atume huko taarifa zake muhimu kama namba ya uanachama na majina yake kamili pamoja na mahali alikuwa anafanyia kazi atapata msaada wa haraka
Inbox?
 
NSSF pesa zinalipwa monthly.. imekuwaje mwajiri mmeachana na bado hajaweka pesa?
Kwamba inawezekana kuvusha mwezi pasipo kupeleka michango? Na hawa staff wa NSSF wanaopiga doria maofisini kukagua risiti hard copies hawakumfikia mwajiri wako?
WAnawajua wasiolipa na hawawafanyi chochote
Kuna mwajiri tangu 2021 hajaweka pesa na akiweka zinaingizwa 2023
Sasa sijui huko nyuma zinalipwa vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…