Ikiwa nadaiwa mkopo na nikakiri nimeshindwa kulipa ni hatua gani naweza kuchukuliwa?

Ikiwa nadaiwa mkopo na nikakiri nimeshindwa kulipa ni hatua gani naweza kuchukuliwa?

Pole kwa changamoto unazopitia...
Kwanza note kuwa "kesi ya madai haimfungi mtu"
Kama utapelekwa mahakamani, usitumie kauli ya kwamba hauna uwezo wa kulipa kwa sababu utazalisha kesi juu ya kesi, na hio ya pili itakuwa ni kesi ya jinai itakayopewa title ya "kukataa deni". Kwa wanaofahamu sheria wanajua uzito wa neno " Sina" pale unapodaiwa.

Hapo ni kukubali kuwa kweli unadaiwa, na utalipa kidogo kidogo kulingana na kipato chako. Uzuri n kwamba utumishi utakulinda (kama upo serikalini)
 
Sio kwamba hiyo hela nilichukua kwa wakati mmoja na kutoka kwa mtu mmoja ni kuwa watu na taasisi tofauti zinanidai ambapo nikipiga Total ni 10,000,000 na kuhusu hela niliifanyia nini nilifungua business imebuma nimelipia watoto ada na nyingine imetumika katika gharama za kawaida za maisha
Poa Mkuu,umeeleweka;
Good luck.
 
Mwalimu, kwanza pole kwa hali unayopambana nayo. Ukishaingia katika mikopo hiyo (kanyaga twende) ujue, utakuwa mtumwa mpaka utakapo, lipwa kinuamgongo chako cha kustaafu, nacho kitakatwa kufidia mikopo hiyo donda ndugu, ya kupe. Nini ufanye basi? Fanya hivi, kaongee, na mkurugenzi wako wa kazi(ajira), anunue hiyo mikopo yote. Ukawalipe taslimu, yaani riba itapungua, na kuhakikishia utalipa milioni tano kamili. Hizo tano,nyingine ujue ni riba na penati. Na ukitoka weka makubaliano ya kulipa laki mbili, kila mwezi kwa miezi 36, kisha jibane na hiyo laki tatu kwa matumizi na kucheza laki laki kila mwezi kwenye vikoba kwa ajili ya kupata mikopo ya dharula kama magonjwa na kulipa ada za watoto. Kingine siku za wikendi tumia hiyo bodaboda yako,kusanya(tafuta) hela ya mboga. Kwa maelezo zaidi usisite kuomba msaada pale utakapokwama.
 
Nadhani huo mkopo unakiuka taratibu zilizopo za mtumishi kubakiwa na theluthi. Unless ulikuwa udanganya juu ya kiasi unachobakiwa. Kukaa na kadi ni utapeli. Cha kufanya ni kujiridhisha uhalali wa hao waliokukopesha na terms zao. Pitia sheria mpya ya bot ya kusimamia huku kukopeshana. Kama aliyekukopesha hayupo kisheria, basi hakuna mkopo.
 
Mwalimu, kwanza pole kwa hali unayopambana nayo. Ukishaingia katika mikopo hiyo (kanyaga twende) ujue, utakuwa mtumwa mpaka utakapo, lipwa kinuamgongo cha cha kustaafu, nacho kitakatwa kufidia mikopo hiyo donda ndugu, ya kupe. Ni ufanye basi? Fanya hivi, kaongee, na mkurugenzi wako wa kazi(ajira), anunue hiyo mikopo yote. Ukawalipe taslimu, yaani riba ita pungua, nakuhakishia utalipa tano kamili. Hizo tano,nyingine ujue ni riba na penati. Na ukitoka weka makubaliano ya kuli laki mbili, kila mwezi miezi 36, jibane na hiyo laki tatu kwa matumizi na kucheza laki laki kila mwezi kwenye vikoba kwa ajili ya kupata mikopo ya dharula kama magonjwa na kulipa ada za watoto. Kingine siku za wikendi tumia hiyo bodaboda yako,kusanya hela ya mboga. Kwa maelezo zaidi usisite kuomba msaada pale utakapokwama.

kama mkurugenzi ni hiki kizazi cha mwinyi anawezatoboa.kama ni wale wazee wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kazi ipo kwakweli.[emoji21][emoji21][emoji21][emoji21].
 
Hivi hizi hela huwa mnapeleka wapi? Kuna mtu mshahara ukiingia hizo taasisi zinabeba anabakiwa na elfu80. Hivi mtu mwenye familia 80elfu unafanyia nini na una mke(mama wa nyumbani) na mtoto[emoji2297][emoji2297][emoji2297]
AISEE
 
Kuna taasisi za kifedha hasa hizi za mtaani wakikukopesha fedha huwezi kuilipa yaani utawalipa had siku un astaafu. unaweza kukopa milioni tano ukaja kulipa milion arobaini hawa jamaa n wa ajabu sana. sasa Nirudi kwako mtoa mada ukishindwa kulipa na ukakiri umeshindwa wadhamini wako watahusika
 
Mtu ambaye amepitia struggle ya kudaiwa kiwango cha pesa ambacho kipo nje ya uwezo wake atakuwa ashaelewa nini namaanisha.

Mfano unafanya kazi unalipwa 500,000/= per month una madeni sehemu tofauti lakini Total ya madeni yako ni 10,000,000/= ikumbukwe kwamba kwenye hayo madeni kuna madeni umiza(yaani kadri unavyochelewa kulipa ndivyo kiasi unachodai kinaongezeka).

A part from that wewe ni Baba, Mume, Kaka na mtoto unategemewa na kuhakikisha kuwa panapotokea tatizo basi liwe under control kwa kutumia akili na uwezo wako.

Bila ya kusahau kuwa gharama za maisha zipo palepale.
-kodi ya nyumba
-chakula
-bili za umeme na ving'amuzi
-mavazi
-ada. etc

Ikumbukwe Sina assets zozote zinazoweza kucompensate mikopo yangu dhamana niliyonayo ni kazi pekee.

Kwa situation kama hii unahitajika muujiza tu kulipa hiyo pesa sasa nikikubali na kukiri siwezi kulipa madeni yangu je kisheria ntachukuliwa hatua gani?

Mara mwisho nilisikia Zambia ilikiri kushindwa kulipa madeni yake lakini heri Zambia sababu ni nchi wanaweza binafsisha serikali.
Pole aisee, nenda kaongee na wadai wako waombe riba isimame, kisha jitahid kukomand laki 2 ilipe madeni laki 3 jibane katika matumizi.
Watoto/mtoto peleka shule za bure si zipo aisee.
Kuna jamaa nae alikua anasomesha eng.medium mwanae + madeni + gharama za maisha akaelemewa.
Swali, taasisi zote wanamiliki vipi kadi ya benk kama dhamana!?
 
Kuna taasisi za kifedha hasa hizi za mtaani wakikukopesha fedha huwezi kuilipa yaani utawalipa had siku un astaafu. unaweza kukopa milioni tano ukaja kulipa milion arobaini hawa jamaa n wa ajabu sana. sasa Nirudi kwako mtoa mada ukishindwa kulipa na ukakiri umeshindwa wadhamini wako watahusika
Hizi Taasisi za mtaani unaingia kama utani kumbe ndio unaingia king imagine mtu anakukata mshahara wote ili hali anajua wewe ni mtu mzima na una familia inakutegemea mpaka uanze kutia huruma na anakupa hela ambayo inakuja kukutesa mwisho wa mwezi kwa hiyo inakuwa mzunguko mara mwaka umeisha mara miaka bado style ni ile ile
 
wapo wenye ubinaadam sana aisee.tatizo ni wale wanaofanyia tamaa hiyo bishara.ndio wale deni linaanza 1ml unakuja kulipa 4.6mln.
wizi mkubwa.

unakopa kwa mtu unalia udhuru miezi mitatu hakati kitu!!!
 
wapo wenye ubinaadam sana aisee.tatizo ni wale wanaofanyia tamaa hiyo bishara.ndio wale deni linaanza 1ml unakuja kulipa 4.6mln.
wizi mkubwa.

unakopa kwa mtu unalia udhuru miezi mitatu hakati kitu!!!
Wapo wachache wenye utu ni kweli ila walitokea ukanda wa Mara kweli wametumwa pesa
 
Sio kwamba hiyo hela nilichukua kwa wakati mmoja na kutoka kwa mtu mmoja ni kuwa watu na taasisi tofauti zinanidai ambapo nikipiga Total ni 10,000,000 na kuhusu hela niliifanyia nini nilifungua business imebuma nimelipia watoto ada na nyingine imetumika katika gharama za kawaida za maisha
Mkopo kwa biashara mpya huwa ni mtihani Sana kusonga
 
Hela ya Mkopo,hela ya ada,hela ya rushwa,hela ya michango ya watu ni nadra Sana kutoboa nazo.Wengi uishia kulia tu
 
Back
Top Bottom