Ikiwa Serikali yenyewe imekishindwa hiki kisiki cha Mpingo, unadhani nani ataweza?

Ikiwa Serikali yenyewe imekishindwa hiki kisiki cha Mpingo, unadhani nani ataweza?

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Ikiwa Serikali yenyewe imekishindwa hiki kisiki cha Mpingo kiitwacho "Watumishi wa Umma" unadhani ni nani ataweza?

Wananchi wamekuwa wakipiga kelele sana kila mahali ya kwamba, watumishi wa Serikali na wale wote walioko kwenye ofisi za Umma wasiwe wanatumia Simu mida ya kazi lakini ni kama tunapigia mbuzi gitaa!

Watumishi wengi kama si wote walioko kwenye ofisi za Umma wamekuwa na Viburi,Nyodo na dharau sana kwa wananchi wanaopaswa kuwahudumia!

Unakuta mtumishi wa Umma ambaye anapaswa kufanya kazi Saa zisizopungua 8 na kuzidi 10,muda mwingi anautumia kwenye Mitandao ya kijamii pamoja na kuchati na Marafiki zao,muda ambao mteja anapaswa apewe huduma yeye unakuta anatumia muda huo kwenye mambo ya kijinga kwenye simu yake!

Hivi serikali imeshindwa kabisa kuweka kanuni na sheria kali ya kwamba kila mtumishi wa Umma aingiapo ofisini simu yake iachwe kwenye Ma-Locker au simu zote saa za kazi zikabidhiwe kwa mtu maalumu ambaye kazi yake itakuwa hiyo tu hapo ofisini na muda wote kama ni huduma ya simu zitumike simu za Ofisi!

Simu za ofisi siku hizi zimekuwa kama mapambo tu,unakuta unapiga simu ofisi fulani ya Umma simu inaita hadi inakata!.

Nani ametoa ruhusa sikuhizi watumishi kuingia na simu zao binafsi ofisini?,wengine wameenda mbali sana,wakati wa kazi wao wako bize na CHUDAI,hawajali wateja tena!.

Nimewahi kutoa wazo ya kwamba,watumishi wote wa Umma walipwe kwa masaa (Kama wenzetu huko Ughaibuni),Hii itasaidia sana kuondoa huu ubabaishaji kwasababu kila mtu atalipwa kadri anavyofanya kazi!

Hivi mnadhani wenzetu huko ughaibuni wao kuja na sera ya kulipa wafanyakazi kwa saa wao ni mbumbumbu?

Hii minyani ndiyo mnairuhusu kuingia na simu ofisini?,Na vile amejua wananchi hawana cha kuifanya ndiyo imejaa viburi kinoma!

Hebu Fikiria tu Daktari ameingia na simu Hospitali saa za kazi halafu akapokea taarifa mbaya kutoka kwa ndugu zake,halafu akiwa ni dokta bingwa,unadhani ufanisi utakuwepo tena siku hiyo?

Wengine siku hizi kazi hawafanyi,kazi yao ni kuangalia YouTube huko na Mitandao mingine ya Kijamii wakibishana U-Simba na U - Yanga tu!

Wengine kwakuwa tu unakuta amechoka na hataki Usumbufu atakwambia "Mtandao leo unasumbua rudi kesho" ,Anashindwa kuelewa ya kwamba umetoka mbali na umetumia fedha zako nyingi kufika hapo lakini anajibu kama vile amekuwa Mkeo au Mumeo!.

Huu Ujinga kwenye Hii nchi yenye laana utaisha lini?
 
Wifi ya bure tena . Acha kelele
CCM MBELE KWA MBELE acha muisome namba
 
watu wanafanya kazi ili kipata fedha na sio kitatua changamoto tulizonazo!.
Ukitaka kupata fedha ni lazima uje na mbinu za utatuzi wa Changamoto za jamii mkuu,vinginevyo labda uwe Dragi Dila!
 
Kuna dada mmoja mweupe mnene ofisi ya NIDA Iringa mjini, saa 7 mchana tu uyo ashaondoka zake
 
huu uzi ulibidi ukae story of change lbd ungefika kirahisi kwa Gavoo
 
Utumishi wa umma ni sehemu ya kupumzika na kutafua namna ya kujitafunia watoto wazuri
 
Back
Top Bottom