GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kama si Wakoloni, huenda Tanganyika kwa sasa ingekuwa ni nchi ndogo sana au kubwa sana kuliko ilivyo sasa.
Isingelikuwa Wakoloni, huenda Arusha na Kilimanjaro zingekuwa nchi zinazojitegemea!
Isingelikuwa ukoloni, huenda Rwanda na Burundi zingekuwa nchi moja au zingekuwa moja ya mikoa ya Tanganyika!
Isingelikuwa ukoloni, huenda bara la Afrika lingekuwa na mataifa mengi zaidi au machache zaidi kuliko ilivyo sasa.
Hii ni kwa sababu Waafrika wangejitengenezea mipaka ya nchi zao kwa kuangalia uhitaji walio nao na si matakwa ya Wazungu.
Huenda leo hii usingekuta kabila moja linapatikana zaidi ya nchi moja. Kwa sasa utakuta:
1. Mmasai wa Kenya na Tanzania!
2. Mmakonde wa Tanzania na Msumbiji!
3. Mjaluo wa Tanzania na Kenya!
4. Mkurya wa Tanzania na Kenya!
5. "Mhaya" wa Tanzania na Uganda!
6. "Muangaza " wa Tanzania na Rwanda!
7. "Muha" wa Tanzania na Burundi, n.k.
Japo mipaka tuliwekewa na Wazungu, tumeziheshimu sana kiasi kwamba hatupo tayari kurekebisha kwa namna yoyote ile. Ni kama vile tunajivunia kazi tukuka tuliyofanyiwa na Wazungu ya kutuamulia mipaka ya nchi zetu na hata majina ya baadhi ya Mataifa yetu. Ndiyo maana kipindi fulani Tanzania na Malawi zilitaka kuingia kwenye mtafaruk wa kugombea Ziwa Nyasa. Kisa? Ramani ya Mzungu iliwawmbia watu wa Malawi kuwa hilo Ziwa ni mali yao.
Japo Afrika ni moja lakini kuingia baadhi ya nchi ni mpaka viza. Unaweza ukakuta nchi zingine za Kiafrika Mzungu wa Ulaya ana urahisi wa kuingia kumzidi Mwafrika anayeishi Afrika.
Mbona Wazungu wamejitengenezea utaratibu huko kwao unaowawezesha kusafiri kirahisi bila bughudha ndani ya bara lao zurila Ulaya?
Mbona Wazungu wameweza kuwa na sarafu moja?
Mbona Wazungu wa Ulaya wameweza kuuimarisha umoja wao kwa manufaa yao?
Sisi tungali tunatii kile kilichofanywa na Wazungu: wagawe ili uwatawale? (Divide and rule). Tumeshindwa kuondokana na athari za ukoloni ndani ya bara letu ambalo ni bara bora na tajiri duniani?
Ili kuonesha kuwa tumeamua kuachana na ukoloni, kwa nini hatujarekebisha au kuondoa kabisa mipaka tuliyowekewa na Wakoloni?
Kwa nini hatujaachana na kila kitu cha kikoloni ikiwemo mipaka ya "kimagumashi" waliyotuwekea?