Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261
Ikiwa utalazwa hospitalini kwa dharura, kuna uwezekano mkubwa hutapata muda wa kujiandaa. Lakini pia kuna wakati unaweza ukawa unajua kwamba unaenda kulazwa hospitali kwa ajili ya tiba fulani. Hivi ni baadhi ya vitu vinavyopaswa kupelekwa kwa mgonjwa.
- Nguo za kuvaa. Ni vyema nguo za kuvaa zikawa zinaendana na mazingira ya eneo husika, kama kuna joto au baridi. Inashauriwa mgonjwa avae nguo ambazo hazitaleta usumbufu pindi watumishi wa afya watakapo toa huduma. Mfano kama mtu kavaa gauni mathalani 'dera', itakuwa vigumu sana kwa daktari kutaka kufanya kipimo cha tumbo au kupima kifua. Hivyo nguo kama sketi na blausi, tshirt na kaptura, trakisuti zinaweza zisilete usumbufu.
- Kadi ya bima ya afya au kitambulisho cha kutojiweza toka serikali za mtaa au afisa mtendaji
- Vipimo vya X-rays, ECG, ECHO, damu na makabrasha mengine yahusuyo afya au ugonjwa wa mgonjwa
- Dawa zozote au prescription ya dawa anazotumia mgonjwa
- Ndala au viatu vyepesi
- Nguo za ndani, au diapers pale inapobidi
- Sabuni, dawa ya meno, mswaki, taulo na kichanio
- Box ya tishu
- Kiasi kidogo cha pesa
- Si vizuri mgonjwa kuwa na simu, vidani, kadi za benki au vitu vyovyote vyenye thamani ili kuepuka upotevu. Lakini ikibidi simu na kompyuta zinaruhusiwa. Ni vyema matumizi ya simu yakapunguzwa ili kutowasumbua wagonjwa wengine