Ikiwa wameweza kumteua marehemu, viongozi wetu wazuiwe kutukopea na kusaini mikataba, watauza Nchi!

Ikiwa wameweza kumteua marehemu, viongozi wetu wazuiwe kutukopea na kusaini mikataba, watauza Nchi!

Nchi tamu sana. Wenye shida ya ajira hawaajiriwi marehem aliyekua na ajira amebadilishiwa ajira.
 
Taarifa sio ya kweli hakuna darasa la saba amewahi kuteulowa kuwa mkurugenzi TPDC hata hivyo natoa benefit of doubt kutukumbusha alikua nani huyo na lini

sababu magufuli alimkuta Dr.mataragio akiwa mkurugenzi tpdc baada ya muda alipata shida akasimamishwa kazi baadae akaendelea na kazi hadi magufuli anafariki

mama Samia alipoingia baada ya muda akamtengua nafasi yake akateuliwa yule ndugu Thobias Mweesiga ambae alikua uvccm udom, baada ya kugundua makosa yamefanyika mama Samia akamtengua huyu kijana ndani ya masaa machache na kumrudisha Dr.Mataragio ambae aliendanae hadi baadae alipomteua Bw. Mussa Makame kuwa mkurugenzi ambae ndio yupo hadi sasa

Sasa unakunusha na kukubali hapo hapo?
 
Sasa unakunusha na kukubali hapo hapo?
Nimekubali magufuli alimteua rasa la saba kuwa mkurugenzi wa tpdc? Wapi nimesema hivyo kwenye hiyo comment? Hata huyo kijana wa uvccm ambae mama Samia alifanya makosa kumteua hakuwa darasa la saba.

Nimekuomba utuambie ni darasa la saba gani amewahi kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa tpdc, usitake kukwepa swali maana huku mtandaoni huwa mna tabia ya kuongopa kutuona wote hakuna tunalojua. Tunasubiri majina na mwaka wa huyo darasa la saba aliyeteuliwa
 
Salaam, Shalom!!

Kusaini mikataba inayohusu nchi kunahitaji Umakini wa Hali ya juu, mikataba yenyewe ni very technical na inahitaji muda kuusoma na kujua hila za vifungu vya mikataba vinavyoweza kuiumiza nchi yetu,

Sasa viongozi wetu wameonyesha hawana Umakini wowote, maana kiutaratibu, ukimteua kiongozi, ni sharti umtaarifu na kumuuliza ikiwa ataafiki kabla ya kutangaza, sasa ikiwa wamemteua mtu aliye mortuary kuwa kiongozi wetu, wanaweza kabisa kutegewa ka kifungu fake kanakoongelea wageni kununua nchi yetu yote, na kwa kuwa lugha ni ngumu na huwa hawasomi na hawana Umakini watasaini tu.

Naleta HOJA mezani ya kuwapiga pin viongozi wetu wasisaini mikopo kwa niaba yetu maana yawezakuwa huwa hawazingatii masharti nyuma ya mikopo hiyo, ndiyo maana vitabu vinavyohamasisha uchafu, ushoga kwa watoto wetu vinazagaa mashuleni na mitaani!

Ushauri: Iundwe Taasisi huru yenye wataalamu wabobevu watakaohusika na kupitia vetting na mikataba yote ya nchi kabla ya kusainiwa Ili kulinda Nchi yetu.

Swali: Ni nani wa kumfunga paka kengele?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Unajuaje kama unalolihofia halijafanyika?

Ila Ikulu imezidi kutia aibu!
1. Alishawahi kuteuliwa Form Four Leaver nafasi ya ukaribu tawala na kutengukiwa muda mfupi baadaye baada ya kufahamika kuwa ni kada tu ila hajashule!

2. Wakati wa kutangaza msiba wa Mwinyi, Rais alisikika akielekeza sehemu ya hotuba yake kufutwa bila kujua kuwa alikuwa "live". Yote hayo ni kwa sababu ya ukosefu wa umakini wa watumishi wa Ikulu.

Inawezekana wamepata hizo nafasi si kwa sababu wana sifa bali wanafahamika.
 
Ushauri: Iundwe Taasisi huru yenye wataalamu wabobevu watakaohusika na kupitia vetting na mikataba yote ya nchi kabla ya kusainiwa Ili kulinda Nchi yetu.

Ushauri mzuri:
sema usije shangaa taasisi iina wataalamu bobevu kina Dr Kumbuka, baba levo, mwijaku, stive nyerere, gigy money, masha love, na amba ruti
 
Utekelezaji wa ushauri huu Kwa ukamilifu,

Ni tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu aliyosimamia Judge Warioba, tena ipatikane kabla ya Uchaguzi wowote.
 
Suluhisho kuu nchi hii ni katiba mpya iliyojitosheleza. Tutarukaruka tunavyoweza, ila tusipokubaliana na hilo tunapoteza muda tu kushangaa.

Tuna viongozi mizigo kwa sababu sisi ni jamii ya mizigo
 
Sasa unakunusha na kukubali hapo hapo?
Wewe ni muongo tu,tutajie Magufuli alimteua Nani darasa la Saba kushika wadhifa wa ukurugenzi pale Tpdc,huyu kawaweka wote walioshika madaraka kabla ya Magufuli na baada ya Magufuli darasa la saba ni yupi hapo?Kubalini kipenzi chenu Samia ni uwezo mdogo kumfananisha na Magufuli ni kumvujia eshima Magufuli.Maana nimeona humu Samia hakiboronga mnaokoteza visababu kuonyesha Magufuli naye aliisha wahi kufanya hivyo.
 
Ushauri: Iundwe Taasisi huru yenye wataalamu wabobevu watakaohusika na kupitia vetting na mikataba yote ya nchi kabla ya kusainiwa Ili kulinda Nchi yetu.

Ushauri mzuri:
sema usije shangaa taasisi iina wataalamu bobevu kina Dr Kumbuka, baba levo, mwijaku, stive nyerere, gigy money, masha love, na amba ruti
🥲🥲🥲
 
Jiwe alimteua la saba kuwa Mkurugenzi TPDC.

Sijui ni kwanini mwendazake anaonekana malaika ila sa100 ni mkosaji.

Hata jiwe alikuwa na makosa sana!
Sio Jiwe ni huyuhuyu mama baada ya kuingia tu
 
20240607_092510.jpg
 
Kweli na yeye alikubali kuingia mkenge? Kama ni hivyo vitakuwa vingi vimepita kwa muelekeo huu
 
Back
Top Bottom