Iko haja ya upinzani nchini kubadilika mtindo na falsafa ya ushawishi kutoka kulalamika tu, hadi kuja na fikra mpya na mipango mbadala ya maendeleo

Iko haja ya upinzani nchini kubadilika mtindo na falsafa ya ushawishi kutoka kulalamika tu, hadi kuja na fikra mpya na mipango mbadala ya maendeleo

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kulalamika na kulaumu pekee ni mbinu ya kisiasa inayotumiwa na waupinzani nchini, isiyo na tija na iliyopitwa na wakati.

Haijawahi kuwa na msaada wala manufaa yoyote kwa vyama vyao wala kuleta mabadilko yoyote kwa wananchi...

Falsafa hii inawadumaza zaidi tu na kuwaacha wadumavu mara dufu.

Serikali zilizopo madarakani zinahitaji vibrant opposition ili daima ziwe active katika kuwatumikia wanainchi na kutimiza ahadi zake kwa wanainchi. ajabu ni kwamba upinzani nchini ni dormant, upo upo tu bila uelekeo wala maono..

Hawana mawazo mapya, hawana mipango mbadala yenye tija, hawana uelekeo na mtazamo wenye matumaini na kuvutia wananchi wengi n.k

Kisiasa,
mawazo mapya, mipango na fikra mbadala ndio pekee silaha muhimu ya kisiasa upinzani na vyama vya kisiasa hai, vinapaswa kua nazo ili kupata uhalali wa kukumbukwa na wanainchi na walau kuungwa mkono na wananchi kidogo kidogo na hapo ndipo kunaweza kuchochea hamasa ya maendeleo, kukua na kustawi kwa demokrasia nchini..

Hii habari ya wanasiasa hususan wa upinzani kujimwambafai kwamba ndio bora na wenye sifa na vigezo vya maana zaidi kuliko wengine, hali ya kua hamna sera za maana, hamna mipango, hakuna fikra, wala mawazo mbadala muhimu ya kuvutia zaidi ya inayotekelezwa na chama kilichopo madarakani, ni kujipotezea muda tu...

Kutengemea au kusubiri muujiza au pengine ushirikina kupata uongozi ni udumavu na u dormant wa kisiasa.

Haiwezekani vyama vingine mathalani CCM wanafanya engagements na consultations na wanainchi everyday, usiku na mchana, kwenye jua na mvua kushawishi na kuelezea wanainchi sera na mipango mikakati yake ya kuwaletea wanainchi maendeleo,

Mpinzani yupo kalala usingiz wa pono anapiga myayo tu, akiamka anajisifu tu kwamba atashinda uchaguzi kisha tena anarudi kulala mpka siku ya uchaguzi ndio huyo tena anaamka...

At the end of the day anajikuta hafahamiki kwa wanainchi, mitandao ya kijamii ilimpumbaza, matokeo yake anakataliwa kwenye sanduku la kura anaanza kulalamika kuibiwa kura na kuharibu kuchochea fujo...

Ni muhimu kutoka kwenye udomant wa kisiasa na kufanya active na vibrant politics ili kua na mchango katika kuchochea maendeleo kwa wanainchi 🐒

Mungu ibariki Tanzania..
 
Wapinzani kama CHADEMA watapata wapi sera na mawazo mbadala yenye tija wakati watu wenyewe wanaokotezana na kukusanyana pasipo hata kuwa na Dira wala muelekeo wa kueleweka.ndio maana wanakwenda kwenda tu kama vipofu gizani. Kazi wanayoiweza ni matusi tu na lugha chafu chafu tu.
 
Back
Top Bottom