Iko siri gani kwenye haya mabonanza yaliyozagaa Tanzania nzima ?

Iko siri gani kwenye haya mabonanza yaliyozagaa Tanzania nzima ?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Nimelazimika kuuliza swali hili maana kuna msela wangu mtu mzima kabisa na mwenye familia amekuja kwangu kuniomba ushauri wa nini afanye ili aweze kuacha kwenda kwenye mabonanza angalau kwa wiki moja tu

Amenieleza mambo mengi sana ambayo mengine siwezi kuyaongea hapa maana mimi bado sijaleft group la wanaume

Kiufupi kaniambia kuwa hata akilala usiku anaota yuko kwenye mabonanza na eti akienda kucheza hata akiwa amekula laki hawezi kabisa kuwa na ujasiri wa kusimama na kuondoka bali huhisi kama kuna msukumo unamsukuma aendelee kucheza

Sasa nimekuja kwenu wadau mnieleze japo kwa ufupi je upo uwezekano wa wachina kuyafanyia matambiko haya matoy ili kuwafanya wachezaji kama mazuzu wasiokuwa na ujasiri wa kuyaacha

Please uncle Mshana Jr njoo huku upesi upesi kwa ushauri
 
Asante sana ngoja nitarejea
 
Hakuna lolote, ile ni kamarii na huwa ni tamu sanaaaa.

Nilikua mchezaji ila niliacha nimebaki nabet tu mpira, mambo mengine tunaanza kumsingizia shetani au uchawi..tunasaka excuses.
 
HAPA NILIPO PAMOJA NA BARIDI LA SEHEM ILA NIPO NJE NIMEVUA SHAT NAHS JOTO KISA DUBWANA!
MAMBO YANGU MENGI YAMEGOTA KISA DUDE.. NIMEKUWA BABA WA AJAB SANA!

KUNA MENGI YALISHAONGELEWA HUKO NYUMA JINSI YA KUACHA LAKIN MBINU ZOTE KWANGU HAZIFANY KAZ,UKWEL KAMAL NI MBAYA MNOO!
MBAYA ZAID YAMETAPAKAZWA KILA MTAA NA UKISHALIWA MARA MOJA NI NGUMU KUACHA.LABDA MSHANA ATAPATA DAWA!
 
Hayo madude yana ulevi na uraibu kama vilevi vingine tuu na haya yako ngazi ya chini, ngazi ya kati ni kwenye tv na kubet michezo mbalimbali na ngazi ya juu ni casino
Serikali kwasasa inafurahia kukusanya kodi lakini haitafakari nadhara yake ya baadae
20230131_044651.jpg
 
Niliwahi kuwa mraibu wa makamari haya ya karata,makamari makubwa ambayo yalinirudisha nyuma kimaendeleo pamoja na kuondoa uaminifu kwa watu ambao ni muhimu sana,majuto ya hali ya juu na maumivu ya hali ya juu zaidi,nilikuwa na marafiki ambao nikiwa na hela na nikiwa nashinda mara kwa mara kwenye hayo makamari huwa wana ni heshimu,kunisifia juu ya uwezo wangu pia na kunikubali kuwa me ni wina,nishavunja{kushinda} sana kwenye makamari makubwa makubwa,ila sijawahi kuingia CASINO na kucheza kamari,ila nikianza kupunwa na kuishiwa kabisa nilikuwa nanyanyasika,kutengwa na mifano mengine ifananayo na hayo,nilitamani saana niache huo mchezo wa haramu,nilisha acha na kurudi mara kwa mara.Niwahi kuyaona hayo MADUBWI na hata kukaa nayo karibu ila hayo MADUBWI {MABONANZA} sikumbuki kama nishawahi kucheza kwa kuwa siwezi kusubiri mia mbili {200} ambazo zinazotoka mule hata kama zikiwa na uwezo wa kufika Million,napambana na nafsi yangu kule nisirudi,maisha ya mateso na manyanyaso,watu washaliwa hela muhimu.Mtu unaweza kufanya tukio la kuogopeka,kukutana na watu ambao wanafanya shughuri mbali mbali ambazo si za halali.
Naona watu wanasifia tu sijui CHAFU TATU {3} sijui nini,ila madhara yake si ya kitoto

Nikisema imenirudisha nyuma basi muelewe,na ukipata hela yake sidhani kama unafanyia kitu cha maana.

Piga vita kamari
 
Haya lazima Mchina ana ubia na kigogo wa nchi hii. Huu ni upumbavu ambao kila mtu anauona lakini serikali inajidai hauuoni.
 
Nimewahi kuwafirisi wachina na haya mabonanza mpaka wakanizuia kuwa nayacheza ni mwendo wa kuhack mitambo tu.
 
SERIKALI HEBU INGILIENI KATI HAYA MAMBO..VIJANA HAWAFANYI KAZI NI KUBET NA KAMARI ZINGINE TUU.....
 
Back
Top Bottom