Iko siri gani kwenye haya mabonanza yaliyozagaa Tanzania nzima ?

Iko siri gani kwenye haya mabonanza yaliyozagaa Tanzania nzima ?

Nimewahi kuwafirisi wachina na haya mabonanza mpaka wakanizuia kuwa nayacheza ni mwendo wa kuhack mitambo tu.
Ulikula pesa mkuu haujawafilisii ikiwa hivyo wangeondoka.

Hawajafilisika, wape mbinu na vijana wengine wale pesa kwa huo mtindo wako.
 
Soma kwa Makini hapa:

Mimi nilikuwa ni mhanga sana wa hayo mabonanza. Yana addiction ya hali ya juu saaana huenda pengine kuliko pombe. Huwa inakuwa hivyo kwa sababu yanakupa kichocheo cha tamaa kwenye ubongo kuwa 'huenda leo ukicheza, utakula pesa nyingi'. Sasa hata uwe na milioni unaweza jikuta yote ukaenda kuchezea ikaisha.

Kinachotokea, mara nyingi mchezaji ana-tune akili kuwa nitumie mtaji mdogo wa labda 10,000 tu kati ya pesa aliyonayo mfukoni (labda laki). Atacheza na kuliwa. Kichwa kitamuelekeza kuwa sasa ongeza tena 10,000 ucheze ukomboe pesa zako. Ajabu, anaweza kucheza kweli akala hata 30,000 lakini ubongo utamwambia komaa ili upige pesa ndedu zaidi, leo ni siku yako. Ataongeza na dau ili ale pesa nyingi zaidi. Akizidi kucheza anajikuta ile pesa aliyokula yote inaisha na anazama mfukoni kutoa ile aliyonayo kwa sababu ya kichocheo kile kile.

Binafsi nimeliwa saaaana na hayo mabonanza ya coins, makasino ya namba 777, matunda n.k ila kwa sasa nimeacha kabisa kucheza hayo mabonanza na nina mwaka sijawahi cheza hata sitaki kuyaona.

Fanya haya kuacha hayo madude:
1. Weka kichwani mwako hofu ya Mungu kuwa hayo madude ni haramu. Kwamba kila utakapokuwa unacheza amini kuwa upo sehemu chafu sana na isiyofaa.

2. Fikilia pesa zote ulizoliwa na uone ni mangapi ungewezafanya kwa pesa hizo ulizopoteza. Amini kuwa hayo madude yamekuwa programmed kula pesa na si kumtahirisha mchezaji.

3. Usipende kupita ama japo kwenda kwenye eneo lililopo hayo madubwi. Jitenge kwenda hata kukaa tu. (Najua hili ni gumu kdg endapo imekuingia sn kwenye damu) ila mimi nimetumia zaidi njia hii. Mtaani kwangu hayo madude yapo karibu na sehemu yangu ya story na bar moja ambayo napenda sn kuangalizia mipira na kucheza draft. Yapo kwa nyuma. Baada siku 1 kuliwa 280,000 nikawaambia washkaji kuwa leo mimi ndio mwisho wangu kucheza haya madude. Nadhani Mungu ameamua kuninyoosha hivi ili pia iwe sababu ya ukombozi wangu. Nikakata mguu, nikawa sitaki hata kwenda tu kuangalia. Nikawa naishia kwenye draft na mpira tu kama sehem ya burudan kwangu.

4. Jiwekee Maazimio magumu kuwa, ninaapa kwako Mungu niwezeshe nisicheze mchezo huu tena na nikifanya hivyo niadhibu. Ishinde tamaa yako na usipende kutembea na pesa nyingi pasipo sababu.

Kiufupi, mahali lilipo hilo dude, kaza roho usipite kabisa na Mungu atakusaidia kuacha kama mimi. Kwa sasa ninauwezo hata siku nikiamua kwenda, nimeshalikana ndani ya nafsi yangu sitacheza. Ila sitaki kumkaribisha tena shetani. Naona hali yangu ya kipato inaimarika maana zamani pesa zangu zilikuwa zinapukutika sn. Naamini unauwezo wa kulishinda hilo dubwana na ukawa free. Naombea wote wenye lengo la kuacha na wazingatie hayo. Tumia hizo kanuni 3. Ji-control mwenyewe, Muogope Mungu na linda kipato chako.

Nimeandika hili kwa sababu vijana wengi sn wana hali mbaya juu ya kutawaliwa na hii biashara ya kamari. Imejaa kila kona, kichochoro, baa na mitaani tu. Kwa wale wa Dodoma ukienda pale Soko la Ndugai ni aibu. Soko zima ndani limejaa Madubwi kila mahali utadhani nayo ni bidhaa zinazouzwa watu wakatumie majumbani.

Kamari ni haramu, tupambane sote kuikomesha.

Nzwangendaba
 
KAbisa, na watu wanataka uwaambie wamelogwa ndio waridhike nafsi.

Nimeshapitia kwenye ulevi, ilikua ikitokea mtu anasema itakua kalogwa sio bureee, aloooh nasuuzika moyo nimepata wakuniliwaza na tatizo langu

Kumbe ni addiction tu, hamna mchawi
Hongera
 
Back
Top Bottom