Iko wapi haki kwa mfanyabiashara anayetambulika kisheria?

Iko wapi haki kwa mfanyabiashara anayetambulika kisheria?

Mr.Mak

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2011
Posts
2,841
Reaction score
1,105
Nitangulie kwa kusema mie ni mfanyabiasha ninayefanya biashara kisheria.
Masikitiko yangu ni kuhusu suala la kuruhusu wanaoitwa machinga kuziba biashara zetu, ivi sie haki yetu iko wapi?
Mie nimepanga frem nalipa kodi ya frem,
Mie ninalipia TRA mapato
Mie nalipia leseni ya biashara
Etc

Then inakuwaje mie sionekani thamani yangu na anaonekana machinga anaruhusiwa kuziba biashara yangu kiasi kwamba hata njia ya wateja kufika Dukani kwangu au mie Mwenye Duka kupata hata nafasi ya kushushia mzigo kuingiza dukani.

Ivi mie haki yangu ni ipi? Wapi nikatoe malalamiko?

Kwanini hatuonekani sie?

Mie ninatii sheria kisha mwingine kwa kivuli cha umachinga anajenga kabisa kibanda mbele ya mlango.

Haki yetu ikoje.
Inaniuma sana aise
 
Pole sana mkuu i feel your pain, mwenye nchi ndio ashawapa kichwa. Ushauri wa bure ambao utaendana na hali ya sasa ni kuwa na sehemu ya kuuza kama machinga mbele ya duka lako hii nimeona inafanywa na watu wengi, mbali na hapo ni maumivu tu mkuu.
 
Bashite alikuja na plan nzuri ila mjomba wake akamsitisha. Watu walipungua sana barabarani na kariakoo ilikua inapitika kiurahisi sana
 
Back
Top Bottom