Iko wapi Royal Tour mliopiga chapuo kuwa italeta manufaa kwa Watanzania? Mbona tozo na ughali wa maisha unazidi kuwabana Watanzania

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Mlisema Royal Tour itatunyanyua kiuchumi na kuleta watalii lukuki na hivyo pato la taifa kunyanyuka.

Sasa kama Royal Tour ilikuwa muarobaini wa kulipatia taifa letu mapato sasa hizi tozo kandamizi za nini?

Mlipigia debe sana Royal tour kwa ushabiki wa kisiasa .Leo hii mnalia na kusaga meno.
 
Mlisema royal tour itatunyanyua kiuchumi na kuleta watalii lukuki na hivyo pato la taifa kunyanyuka.

Sasa kama royal tour ilikuwa muarobaini wa kulipatia taifa letu mapato sasa hizi tozo kandamizi za nini?

ulikuwa ni ushenzi na uchawa wa wapambe na huku maza aki consolidate power
 
Royal tour bila kuona The African Royal, "MASAI" imeleta ukwakwasi.
Unaendaje kuona Serengeti??

Nje ya mada.

Wapo walionyanyulika, ' waleee wapiga debe'

Watalii na huko waliko chaliiii

Pato lipo, la tozo.

Tutanyanyuka. Kitaeleweka.
 
Uwe na akili basi yaani investment ya tshs 7billiobs tu ilete unafuu wa maisha kwa nchi. Kwani wewe unajua utalii unachangia a percentage ngap ktk uchumi!? Daah pole sana.

Royal tour ililenga ku boost utalii tu na imefanya hivo..... na wapo waliofaidika kwa nafasi zao ktk sekta hiyo
 
Use na akili basi yaani investment ya tshs 7billiobs tu ilete unafuu wa maisha kwa nchi. Kwani wewe unajua utalii unachangia a percentage ngap ktk uchumi!? Daah pole sana.

Baada ya kuboost huo utalii mbona hazina pesa hakuna hadi imebidi mlete double taxation kwa jina la Tozo???
 
Kitu kinachoniudhi zaidi utasikia Mama katoa billion 50 za ujenzi wa daraja ..,.
Mama katoa trillion 3 za ujenzi wa daraja la Jangwani.

Ikiwa Mama ana uwezo wa kutoa mfukoni mwake fedha zote hizo sasa hizi tozo za nini !.

Huu upuuuzi wa kila jambo jema linalofanywa kunasibishwa na Mama wakati tunajua pasipo shaka maendeleo yote yanatokana na fedha kupitia kodi mbali mbali.
 
Wewe ndiye hufikirii kabisa.
Kwani ukiwekeza bilioni 70 unavuna bilioni 70 tu?
Learn the concept of input and output.
 
Kitu kinachoniudhi zaidi utasikia Mama katoa billion 50 za ujenzi wa daraja ..,.
Mama katoa trillion 3 za ujenzi wa daraja la Jangwani.

Ikiwa Mama ana uwezo wa kutoa mfukoni mwake fedha zote hizo sasa hizi tozo za nini !.

Huu upuuuzi wa kila jambo jema linalofanywa kunasibishwa na Mama wakati tunajua pasipo shaka maendeleo yote yanatokana na fedha kupitia kodi mbali mbali.
Mbona awamu iliyopita hukusema.
Hukusikia kauli ya "rais ametoa pesa?".
 
Mbona awamu iliyopita hukusema.
Hukusikia kauli ya "rais ametoa pesa?".
Magufuli ndio mwanzilishi wa huu ujinga,nifikiri Mama asingeingia katika hili dubwana la kujisifu hata kwa jambo lililo wazi.

Sasa umekuwa utaratibu wa chawa wake utasikia Mama anaupiga mwingi.Ukijiuliza hizo sifa au huo uchawa mbona hauna mashiko utaambiwa una wivu.

Bora magufuli aliwafungia umeme kaya masikini kwa Tsh 27,000.Huyu Mama kazi yake kubwa ni kutoa ajira kwa waZanzibar kihamishia fedha nyingi Zanzibar.Wazanzibar wakimsifu sawa.
 
royal tour ilikuwa kumpa kick ssh haikuwa na malengo ya kuongeza wataliii. sasa toka lini watanzani tukawa na interest ya utaliii. filamu inaonyeshwa buree tukaangalie ....then what next
 
Kwani huoni watalii wameongezeka na hivyo Pato kutoka huko limeongezeka, kwa upeo wako unazani secta ya utalii peke yake ndio itatatua kila kero? Hujaona ajira zikiongezeka Hilo kwa vijana hasa baada ya kuongezeka kwa mafuriko ya watalii, hujaona wamahoteli wakinufaika, mambo inayofanya serikali Ni mengi na makubwa ambayo hayawezi kumalizwa kwa mapato ya Wizara moja tu
 
royal tour ilikuwa kumpa kick ssh haikuwa na malengo ya kuongeza wataliii. sasa toka lini watanzani tukawa na interest ya utaliii. filamu inaonyeshwa buree tukaangalie ....then what next
Kwani wewe hujashuhudia mafuriko ya watalii wakimiminika hapa nchini? Hujaona kuwa Jambo Hilo limechangiwa na royal Tour? Huoni kuwa vijana wamenufaika na ongezeko Hilo la watalii
 
Kitu kinachoniudhi zaidi utasikia Mama katoa billion 50 za ujenzi wa daraja ..,.
Mama katoa trillion 3 za ujenzi wa daraja la Jangwani.

Ikiwa Mama ana uwezo wa kutoa mfukoni mwake fedha zote hizo sasa hizi tozo za nini !.

Huu upuuuzi wa kila jambo jema linalofanywa kunasibishwa na Mama wakati tunajua pasipo shaka maendeleo yote yanatokana na fedha kupitia kodi mbali mbali.
Ila wewe unamatatizo makubwa, kwani unazani msimamizi mkuu wa miradi ya maendeleo Ni Nani, unafikiri Nani kapewa mamlaka hayo kikatiba, unazani Ni kwanini kiongozi wa chini ikitokea kaharibu watu wanapaza sauti kwa Rais ili amuwajibishe, Rais ndio kila kitu na ndiye anayebeba sifa zote za kimafanikio,kwanini unasikia watu wakimsifia Hayati baba wa Taifa? Je alikuwa peke yake na kushika nafasi zote peke yake?
 
Baada ya kuboost huo utalii mbona hazina pesa hakuna hadi imebidi mlete double taxation kwa jina la Tozo???
Nani kakwambia hazina hakuna hela? Kama hakuna pesa watumishi wanalipwa mishahara toka hazina ya nchi gani? Wewe ndio msimamizi wa hazina? Acha maneno maneno ya uongo uongo hapa
 
Mlisema royal tour itatunyanyua kiuchumi na kuleta watalii lukuki na hivyo pato la taifa kunyanyuka.

Sasa kama royal tour ilikuwa muarobaini wa kulipatia taifa letu mapato sasa hizi tozo kandamizi za nini?

Mlipigia debe sana Royal tour kwa ushabiki wa kisiasa .Leo hii mnalia na kusaga meno.
Royal tour sio muujiza ila is real na matokeo yake ndio kama haya inaendelea kumimina watalii daily 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220911-202311.png
    Screenshot_20220911-202311.png
    62.4 KB · Views: 3
royal tour ilikuwa kumpa kick ssh haikuwa na malengo ya kuongeza wataliii. sasa toka lini watanzani tukawa na interest ya utaliii. filamu inaonyeshwa buree tukaangalie ....then what next
Kama ni kick ilimpa kweli kweli kwenye sekta ya utalii..

Ni Royal tour ndio imepelekea Marekani kuwa mtoa watalii wengi kuja Tzn tofauti na kabla ya Royal tour..

Vitendo vinaongea zaidi kuliko maneno 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220819-170716.png
    Screenshot_20220819-170716.png
    113.4 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220819-170704.png
    Screenshot_20220819-170704.png
    131.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom