Ikulu Dar: Rais Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mussa Zungu apewa Wizara ya Mazingira

Ikulu Dar: Rais Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mussa Zungu apewa Wizara ya Mazingira

Roving Journalist,
Mbona sioni popote elimu ya "Zungu" mkuu,ni makusudi au.Na hili jina la Zungu ni la utani au la kiukweli.Kama ni la utani,hebu tufafanulie, kwa nini alipewa jina la utani la "Zungu?"
 
chakii,
Hivi Mh. Rais aliposema amehamia Ikulu ya Dodoma alikuwa anamaanisha Ikulu ya Dodoma iliyoko Magogoni Dar es Salaam au?
Dar Patamu Dodoma iliomshinda Mwl. Nyerere licha ya kuwa mwanzilishi sioni kama Magu ataimudu.
Karudi Dar baada week chache.Dar ndio mpango mzima.
Baada ya miaka 5,Dar itawika tena ni jambo la muda,ndio maana hata mabalozi wanausoma mchezo huo.
Dodoma ni matumizi yasio na tija.
 
Hivi ubalozi kumbe nayo ni adhabu!? Unaharibu hapa, unapelekwa kule ukaendelee kuharibu!

Bongo bana, wacha tuendelee kuwa masikini tu.....na hizi mambo za uhujumu uchumi kumbe huwa ni siasa tu na kutesa "tusiowapenda" tu?
 
sblandes,
Yeye mwenyewe anarukaruka kukaa dodoma alikuwa anamuunga mwalimu just kuunga tu hata vitu ambavyo ni outdated kama dodoma na stiglers George ukilinganisha na modern world atakuja elewa siku akiwa nje atabaki kuwalaumu kwann amkunishauri.

Huwezi cheza mpira ukiwa ndani thus ili ufanikiwe unahitaji wakosoaji maana wao wako nje hata wewe ukikaa nje ndipo utayaona makosa yako.Thus watawala Wa kiafrica huwa na akili wakiwa nje ya mfumoUthibitisho ni speech zao baada ya kustaafu
 
Wamesahau kutaja kuwa simbachawene aliwapa ofa ya bia wabunge wavitimaalumu chadema pale singida
 
Sisi tulijuwa mdomo mrefu wa Lugola haungemsaidia kudumu kwenye kiti kile kutukana waungwana.Kwa upande mwengine nampongeza raisi kwa kuona umbumbumbu wa waziri wake huyu.Yaonekana alikuwa akimnvutia hatua tu ili hatimae amtumbue kirahisi.
 
Hivi Wizara ya nchi za nje bado kuna 'carrier diplomats'? Tunaona teuzi za watu - ambao hawatoki huko lakini pia inaonekana kama adhabu au sehemu ya kuficha walioshindwa.

Tunakumbuka ahadi kuwa katika serikali ya awamu ya tano mtu atakayeshindwa hatahamishiwa kwingine bali ataondolewa.
 
Back
Top Bottom