Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

IMG_20201017_165845.jpg
IMG_20201017_165858.jpg
Screenshot_20201017-170035.png
 
Nimeamini hali mbaya Zanzibar mpaka movie zinatengenezwa, kwanini sasa bado siku 10 tu uchaguzi? hali tete sote tunajua.
 
Kwa muhtasari, hoja hizo ambazo hii leo zinasainiwa katika hati ya makubaliano kuziondoa katika zile hoja ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi ni pamoja na ushirikishwaji wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye masuala ya kikanda na kimataifa.

Hoja nyingine iliyopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Hoja ya tatu ni gharama za kushusha mizigo bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar.

Hoja ya nne ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia. Hoja ya namna ya kugawana mapato ya rasilimali ya mafuta na gesi asilia yatakapopatikana. Maelezo yanatolewa na Balozi Joseph Sokoine ambae ni naibu katibu ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na mazingira.

Balozi Sokoine: Ufumbuzi; Serikali zetu baada ya kujadiliana ziliamua kumtumia mshauri muelekezi, OPEC ya Uingereza ili atoe ushauri wa kitaalam kuhusu mgawanyo wa rasilimali ya aina hiyo kwa nchi za muungano. Kampuni ya OPEC ilikamilisha kazi hiyo na kuwasilisha mapendekezo kwa SMT na SMZ. Hata hivyo hoja nyingine ilijitokeza kwamba suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe katika orodha ya mambo ya Muungano.

Baada ya majadiliano pande zote mbili zilikubaliana kuondoa masuala ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano hivyo sheria ya mafuta namba 21 ya mwaka 2015 mamlaka ya kuanzisha vyombo vya kusimamia mafuta na gesi asilia kwa kutumia sheria ya Zanzibar.

Hoja ya tano ni utaratibu wa kikao vya kamati ya pamoja ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kushughulikia masuala ya Muungano.
========


Hapo inakuaje ikiwa mafuta yanapatikana within 200 nautical miles of each part Bara yupo within 200 miles na ZNZ nayo ipo within hizo 200 nautical miles?
 
Hii imechelewa sana na haitabadilisha muelekeo wa kuiondoa CCM madarakani, hizo pipi kuleni wenyewe kwa wenyewe.
Chini ya Maalim Seif na Tundu Lissu manufaa kwa Watanzania wote wala hakutakuwa na kudanganya, CCM imetufikisha tuwe waroho na imetufanya hatupo sawa, CCM walijali maslahi yao zaidi na hili hamna wa kumdanganya maana mkichaguliwa mtakuja na jipya, limo kwenye katiba tubadilishe katiba kwa maana hio itakuwa mumewapiga chenga WaZanzibari waliovaa mkenge huo kuwa sasa kila mtu na chake. Danganeni wenyewe kwa wenyewe.

CCM sasa basi imetosha hata mkivunja Muungano bado wananchi watataka muondoke madarakani, hivi kwa nini hamuelewi wananchi kuwa wamewachoka, mmebakia nyie wahafidhina tu umma umeshakikataa Chama Cha CCM
 
Wakati serikali inahamasisha watu waende kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu, Chadema walikua wakihamasisha watu wasiende kujiandikisha mpaka ipatikane katiba Mpya Chakushangaza baada ya matokeo kutangazwa watasema wameibiwa kura.
🚮🚮🚮
 
Back
Top Bottom