Mkuu Limbani nimeandika bandiko hilo hapo juu kabla ya kusoma lako, lakini naona tunafikiri kitu kimoja.
Huyu Salva Rweyemamu mtupu kabisa. Anasema kigazeti kisicho na nguvu ya dola kinaingilia uhuru wa mahakama kwa kusema Mkapa atatinga mahakamani.
Wakati huo huo haoni kwamba yeye mwenye sauti ya juu kabisa katika dola letu, msemaji wa rais aliye juu ya sheria, rais anayeteua majaji wa mahakama, kwa kusema Mkapa ni safi na hana hatia katika swala ambalo bado liko mahakamani, haoni kwamba yeye ndiye anayeingilia uhuru wa mahakama.
Kama kuna jaji aliyepewa kesi hii, na jaji anaogopa ogopa watawala wa nchi, halafu anamsikia msemaji wa Ikulu anasema Mkapa hana hatia, halafu jaji akatazama kesi akaona Mkapa ana hatia, unafikiri hii kauli ya Rweyemamu haiwezi kupindisha haki katika hukumu ya huyu jaji kama jaji hana moyo wa ujasiri ?
Tayari kashajua Ikulu inataka Mkapa asipatikane na hatia kabla mahakama haijatoa hukumu.
Anayeingilia uhuru wa mahakama hapa ni nani? Gazeti au Rweyemamu na Ikulu yake ?