Sio Mwanasiasa
Senior Member
- Mar 4, 2011
- 115
- 13
samahan kama ntakukwaza,ila kama nimeelewa taarifa vizuri ni kwamba ikulu imesema hawez kutinga mahakaman coz hausiki nakesi ya msing iinayozungum,zwaTehe tehe teheeee!
Kazi kwelikweli.
'Hawezi kutinga mahakamani' who is he!
ishu hapa ni hati inayo onyesha Mr clean kaapa na sio huyo Banyamlenge anavyo tetea Ikulu.
Kwanza ni mgeni na shughuli za Ikulu na mala nyingi amekuwa anajibu majibu mengi kwa ufahamu wake na si IKulu
kutokana na kuto jua maadili ya TIS na kazi zao.
Hana jipya zaidi ya kusoma magazeti na kukurupuka na majibu ya mizaha. Any way fadhila za uwana mtandao hizo.
wana JF tusijadili sana suala la uraia wa reyemamu, hebu tulitazame kwa marefu na mapana suala la mstaafu Chinga kama nihaki afikishwe kizimbani au la; bado haijajulikana mbele ya sheria nani katoa melezo sahihi kati ya gazeti na Reyemam, naomba wanasheria mtufafanulie vizuri juu ya hili.:A S 39:
"Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. "Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Kwa kweli kama Salva kasema hivyo basi ameingilia uhuru wa mahakama na hakuna haki yeyote itakayotendeka hapo... Ni bora angesema kuwa hakuna summons yeyote iliyomuita Mhe. Mkapa mahakamani, lakini kusema kuwa Mkapa hahusika how did he know? Ina maana Ikulu ndio ofisi ya Presecutor? au ndio defensive counsel? INAMAANISHA IKULU INAJUA MWENENDO WOTE WA KESI HII...
Mkuu Limbani nimeandika bandiko hilo hapo juu kabla ya kusoma lako, lakini naona tunafikiri kitu kimoja.
Huyu Salva Rweyemamu mtupu kabisa. Anasema kigazeti kisicho na nguvu ya dola kinaingilia uhuru wa mahakama kwa kusema Mkapa atatinga mahakamani.
Wakati huo huo haoni kwamba yeye mwenye sauti ya juu kabisa katika dola letu, msemaji wa rais aliye juu ya sheria, rais anayeteua majaji wa mahakama, kwa kusema Mkapa ni safi na hana hatia katika swala ambalo bado liko mahakamani, haoni kwamba yeye ndiye anayeingilia uhuru wa mahakama.
Kama kuna jaji aliyepewa kesi hii, na jaji anaogopa ogopa watawala wa nchi, halafu anamsikia msemaji wa Ikulu anasema Mkapa hana hatia, halafu jaji akatazama kesi akaona Mkapa ana hatia, unafikiri hii kauli ya Rweyemamu haiwezi kupindisha haki katika hukumu ya huyu jaji kama jaji hana moyo wa ujasiri ?
Tayari kashajua Ikulu inataka Mkapa asipatikane na hatia kabla mahakama haijatoa hukumu.
Anayeingilia uhuru wa mahakama hapa ni nani? Gazeti au Rweyemamu na Ikulu yake ?