Utakuta tumekopa mabilioni kujenga ikulu kubwa zaidi duniani. Tumekopa hata ramani ya Mjerumani aliyotumia kujenga ikulu ya Magogoni, mwonekano ni uleule hata Zanzibari muonekano ni ule ule, nani katufinyanga namna hii?
Ikulu ya kifahari kwa fedha za kukopa, kweli?! Embu angalia ikulu ya waziri mkuu wa Uingereza tunapokimbilia kukopa na kuomba pesa, halafu fananisha ya yetu. Utashangaa sana jinsi sisi Watanzania tusivyojali watu wetu na kwenda kufanya tusivyoviweza wala kuvihitaji. Ni ajabu!
Je, watu wa Dodoma wana maji masafi ya kunywa na ya kutosha? Watoto wetu hadi leo wanasomea chini ya miti, hawana madawati wala vitabu, hiyo ikulu itasaidia vipi kuondokana na madhila haya? Zipo changamoto nyingi mno nchini, watu wanakufa kwa kukosa dawa, vituo vya afya vipo mbali mno na gharama za matibabu ni kubwa mno. Kwanini tusiweke fedha zetu kwenye mambo haya?
Linganisha ikulu ya Waziri Mkuu wa Uingereza na ile ya kwetu ndio utajua kuwa Africa tuna safari ndefu.