Tetesi: Ikulu ya Marekani yatangaza dawa dhidi ya Corona, shukrani sana wazungu, mbarikiwe


Huku Africa ni NYUNGU mwanzo mwisho.
 
CCM HOYEEEEEEEE!!!!

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
... mchina aanze kuifyatua sasa am-overtake US kwa u-super power, itamtoa sana hii. Maprofesa Afrika kaeni mkao wa kuandika dozi dawa imepatikana.
Kwamba wataalam wetu ni waandika dozi tuπŸ˜€πŸ˜†πŸ˜†. We jamaa mgomvi sana
 
... mchina aanze kuifyatua sasa am-overtake US kwa u-super power, itamtoa sana hii. Maprofesa Afrika kaeni mkao wa kuandika dozi dawa imepatikana.
Kwamba wataalam wetu ni waandika dozi tuπŸ˜€πŸ˜†πŸ˜†. We jamaa mgomvi sana
 
Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani (FDA) imetoa ruhusa ya dharura ya dawa ya Ebola inayofahamika kama 'remdesivir' kutumika kuwatibia wagonjwa wenye virusi vya corona.

Ruhusa ya kutumika kwa dawa hiyo kwa sasa imetolewa kwa watu ambao wamelazwa hospitalini tu kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Jaribio la hivi karibuni la kitabibu linaonyesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwasaidia watu mahututi wanaoumwa corona, na inaaminiwa kuwa inaweza kuwasaidia kupona haraka.

Hatahivyo, haijaonyesha kuwa inasaidia kupunguza idadi ya vifo.

Wataalamu wa dawa wametoa onyo kuhusu dawa hizo -ambazo zilitengenezwa ili kutibu Ebola, na zilitengenezwa na kampuni ya Gilead pharmaceutical iliyopo mjini California -kwamba visionekane kuwa ni jambo la ajabu sana kwa dawa hiyo kuanza kutumika kwa ajili ya kutibu virusi vya corona.

Dawa hiyo inaweza kuigwa na kuharibu utendaji wake.

Katika kikao na rais wa Marekani Donald Trump katika ofisi za Oval, Mkurugenzi mkuu wa Gilead Daniel O'Day alisema Mamlaka ya dawa FDA ndio hatua muhimu ya kwanza.

Kampuni hiyo itachangia chupa za dawa hiyo milioni 1.5 , alisema.

Kamishina wa FDA, bwana Stephen Hahn alisema kwenye mkutano huo: "Hii itakuwa tiba ya kwanza ya Covid-19 kupitishwa , tumefurahi sana kuwa sehemu ya uwezeshaji huo."

Mamlaka ya dharura ya FDA si sawa na ile ambayo inatoa idhini rasmi ambayo inahitaji uangalizai wa hali ya juu zaidi.

Ni nini tunafahamu nini kuhusu remdesivir?
Dawa hii haikutibu Ebola, na Gilead ilisema kwenye mtandao wake: "Remdesivir ni dawa ya majaribio ambayo ambayo haina ufanisi au usalama wa kutibu magonjwa yote." Gilead ilitoa angalizo la madhara makubwa ambayo yanaweza kumpata.

Ingawa rais Trump amekuwa akiiunga mkono remdesivir kwa kuizungumzia kuwa ni dawa sahihi ya virusi vya corona.

Katika jaribio la kitabibu, taasisi ya taifa ya mzio na magonjwa yanayoambukiza nchini Marekani (NIAID) imebaini kuwa remdesivir inapunguza muda wa dalili za ugonjwa huo kutoka siku 15 mpaka siku11.

Jaribio la dawa hilo lilifanyika kwa watu 1,063 katika hospitali mbalimbali duniani, - zikiwemo Marekani, Ufaransa, Italia,Uingereza, China na Korea kusini. Baadhi ya wagonjwa walipewa dawa hiyo na wengine walipewa tiba ya 'placebo'.

Dkt Anthony Fauci ambaye anaiongoza NIAID,alisema kuwa remdesivir imeonyesha wazi umuhimu wake ,kikubwa ni kuharakisha muda wa mtu kupona.

Hata hivyo remdesivir inaweza kusaidia katika uponyaji - na kuzuia watu kutibiwa kwenye chumba cha dharura - majaribio ya dawa hiyo haijaonyesha wazi kuwa inaweza kuzuia watu kufa kutokana na virusi vya corona.

Maswali mengi yakiwa hayana majibu bado kuhusu muongozo wa tiba hiyo , Gilead alishauri kuwa wagonjwa watumie dozi ya siku kwa wale ambao wanatumia mashine ya kupumulia na siku tano kwa wagonjwa ambao hawatumii mashine.

Je, mataifa mengine yanaweza kutumia dawa hiyo ya remdesivir?
Gilead alisema kwa sasa wanatumia dawa ambazo zilikuwepo kwenye hifadhi ya dawa zao na si rahisi kusafirisha maeneo mengine.

Serikali ya Marekani itaweza kupanga namna remdesivir itafikishwa kwenye hospitali za kwenye miji mbalimbali nchini Marekani , ambayo imeathirika zaidi na ugonjwa huu wa Covid-19.

Hivyo haiko wazi kabisa , ni kiasi gani cha dawa kitasambazwa duniani kote na hata gharama yake haijajulikana bado.

Gilead imesema kuwa inachangia dozi milioni 1.5 ya dawa hiyo ya remdesivir, ambazo zitakuwa na uwezo wa kutibu watu zaidi ya 140,000 bila gharama yoyote ile.Kitengo cha dharura cha kusambaza dawa nchini Marekani kinahusika katika hilo.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona
Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona
Je, kujifukiza ni tiba ya corona?
Je unaweza kupata maambukizi ya corona kutoka kwa mfu?
Lakini dunia nzima kuna watu zaidi ya milioni tatu ambao wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa corona katika mataifa 185.

Gilead ilisema ina nia ya kuongeza uzalishaji wa dawa hizo haraka wawezavyo wakishirikiana na washirika wao duniani,

Kampuni hiyo imelenga kutengeneza dawa zipatazo 500,000 mpaka ifikapo mwezi Oktoba 1, na milioni 1 kwa ajili ya ifikapo Desemba 2020 na mamilioni zaidi kwa mwaka 2021, kamaTaasisi ya tiba na uchumi, nchini Marekani ambayo huwa inatafiti gharama za dawa imeweza kuweka makadilio ya dawa hiyo ya remdesivir kuuzwa kwa dozi ya siku 10 itagharimu dola 10 za kimarekani, lakini bei inaweza kutegemea gharama ambazo majaribio ya tiba yalivyotumika. kutakuwa na uhitaji.

Video captionCoronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?
Hali ya vifo vinavyotokana na corona New York ikoje
Taarifa ya tiba hiyo ambayo inawezekana kuwa na uwezo wa kutibu corona imekuja wakati New York ikiwa imeripoti kuwa na vifo 98 vinavyotokana na ugonjwa wa corona.

Kituo cha Isabella Geriatric kilichopo Manhattan kinasema kuwa watu 46 ambao ni wakazi wa eneo hilo walikufa baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya corona, huku wengine 52 walidhaniwa kuwa na virusi.

Na Dkt Fauci amekuwa akichunguzwa kutoa ushuhuda wiki ijayo katika mkutano wa kutathmini jinsi utawala wa Trump ulivyokabiliana na mlipuko huu.

"Wakati utawala wa Trump ukiendelea na kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, ikiwa pamoja na mipango ya kuifungua Marekani na kuharakisha upatikanaji wa chanjo,si jambo la busara kwa watu hao hao kuonekana wakihudhuria kusikiliza madai," msemaji wa White House Judd Deere alisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dawa ipo mda tu tangu Wuhan outbreak itokee hawa Gilead walitangaza kuifanyia majaribio dawa hii ya ebola kutibu corona.Baadae tukasikia wamesitisha ruhusa sababu haijawa efficient kiasi kina chotakiwa.
Lakini ghafla baada ya Madagascar kuja na dawa yake na baadhi ya nchi za kiafrika kuunga mkono,hawa nao ghafla wanasema dawa hii ya Remdesivir wameiruhusu huko kwao!!
Mie nashauri Tanzania twende na Madagascar kwanza.
 
Kaona Madagascar anampiga gap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…