Mabibi na mabwana katikati ya misukosuko na gonjwa hili lililotukalia vibaya mno hasa sisi wenye migogoro yoyote mingine ya kiafya, wale wenzetu na sisi wenye umri 50+, pia wale wafanyao shughuli zao kwenye mazingira yenye hatari zaidi, kwa hakika ina fikirisha sana.
Ikumbukwe kuwa hata huko kunako mabeberu na chanjo zao ni magroup hayo ndiyo pekee yaliyopewa umuhimu wa kwanza kuipokea chanjo hii sasa na katu si kila mtu katika awamu hii.
Huko huko kwa mabeberu na nia yao ya kumchanja hatimaye kila mtu ikiwezekana, itachukua miezi kadhaa hadi kuwafikia watu wao wote.
Ajabu na kweli hapa kwetu wanaopiga kelele zaidi za kuikataa na kuitafutia mashaka ya aina yoyote chanjo hii, si wale ambao kweli wamo kwenye magroup haya hatarini.
Hii si dhahiri kuwa wasiohusika hawa ni binadamu tu wanaoongelea mkuki wa nguruwe usiowahusu? Wataujuwa vipi binadamu hawa uchungu wa mkuki anaopigwa nao nguruwe?
Je, hawa wenye magonjwa mengine hawana umuhimu wowote kuishi au wao wanapungukiwa kuwa watu kamili kiasi kuwa hata wakipukutishwa vilivyo na gonjwa hili si kitu sana?
Hawa watumishi wa afya au hawa wa kwenye maeneo ya misongamano kama mabaa, mashule, mastendi, mabasi, madala dala, makanisa, misikikiti nk nao je? ni sahihi kuwasemea kwa vile tu hatari yao wewe mwingine haikuhusu?
Vipi kuhusu wazee? Pana makabila ambayo hayajali maisha ya wazee wao. Aghalabu huwauwa kinyama kwa tuhuma za uchawi. Si ajabu kwenye makabila hayo kwa kijana kumwua mzazi wake au kumkodia wauwaji kwa malipo manono kwa inayoitwa kazi hiyo.
Je tuna watu wa namna hii mahali kwenye mlolongo wa kuwahami watu hawa na labda sasa imepatikana sababu iliyofichika ya kuwasafishilia mbali?
Ndugu zangu katika hali ya kawaida tusilazimishe kuingilia mechi za wengine kama hazituhusu na hii kwa hakika ni kiroho safi tu.
Kuishadadia chanjo hii kwa kelele za kila namna wakati wewe haumo katika makundi haya kwa hakika ni dalili za wazi za ubinafsi uliopitiliza.
Tuyaache makundi hatarini haya yapambane kujishindia mechi zake. Nadhani huo ndiyo ulio uungwana na uzalendo uliotukuka.
Ninawasilisha.