Ikumbukwe Simba SC imetolewa hatua ya robo fainali Club Championship

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wenye vichwa vya panzi wanafanya karamu kufurahi Simba kutolewa,ila tu wanasahau kama Simba hii tishio imetolewa hatua ya robo fainali kwenye ligi kubwa kuliko zote Afrika. Imetolewa zikiwa zimebaki timu babe nane tu kati ya timu makumi zilizoanza hatua ya mchujo

Halafu imetolewa baada ya kuwafyeklea mbali wakali wenzie Nkana Fc, AS Vita na JS Saoura

Ingewezekanaje timu zote 8 ziende nusu?No,lazima kuna timu nne ziishie hapo,kama ambavyo Club bora kuliko zote Africa Al Ahl inaweza kutolewa usiku wa leo

Ikumbukwe zaidi kuwa tulijiwekea malengo saafi ya kufika hatua ya makundi,kwa hiyo wewe kichwa panzi jua hii ni Simba iliyovuka malengo

Kwa lugha rahisi Simba imeondoka kwenye level za Yanga imechumpa juu. Yanga atabaki kuwa mtani wa jadi tu
 
Ahahahahahaa utadhani wadhaifu walivyokuwa wanakataa kushirikiana na mkagiaji....!!! Maneno meeengiiii mwisho wameachia
 
Hiyo ni sawa na pale ajali napotokea. Baadhi wakafia eneo la tukio na mwingine akaenda kufia hospital. Kesha ndugu na jamaa wakaanza kusherehekea kwa ndugu yao kufia hospital badala ya eneo la tukio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mngekuwa mliyajua hayo msingetupigia kelele kila siku kuwa ushindi ni lazima.
Eti Simba Nguvu moja
Simba nguvu moja my foot
 
Pia ikumbukwe simba imechezea vichapo vikubwa sana ugenini! Jumla ya mabao ktk mechi za ugenini kuanzia hatua ya makundi ni 16 ( 5 + 5 + 2 +4)! Wastani wa goli 4 ktk kila mechi ! Duu ni karekodi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…