Ikungi tunasema asante Waziri Mkuu Kasim Majaliwa

Ikungi tunasema asante Waziri Mkuu Kasim Majaliwa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
IKUNGI TUNASEMA ASANTE WAZIRI MKUU MHE. KASIM MAJALIWA MAJALIWA.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amemshukuru waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa kwa kufanya ziara ya ukaguzi na kisha kuweka mawe ya msingi ya chuo cha mafunzo ya ufundi Veta pamoja na hospital mpya ya wilaya ikungi na kutembelea kituo cha afya Iglanson

Mhe. Muro amesema ziara ya waziri imeleta faraja kwa wananchi wa ikungi kutokana na maelekezo yaliyotolewa na waziri mkuu majaliwa yanayokwenda kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo hospital mpya ya wilaya na kituo cha afya Iglanson na chuo cha veta ambavyo amevitembelea

Dc Muro amesema kwa upande wao wanajipanga pamoja na uongozi wa halmashauri na veta kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa waziri mkuu majaliwa ndani ya muda mfupi ili wananchi wapate huduma bora za kijamii

Tazama picha/video za matukio 👇🏾

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi
07/08/2022
 

Attachments

  • IMG-20220807-WA0059.jpg
    IMG-20220807-WA0059.jpg
    78.7 KB · Views: 11
  • IMG-20220807-WA0060.jpg
    IMG-20220807-WA0060.jpg
    100.8 KB · Views: 13
  • IMG-20220807-WA0056.jpg
    IMG-20220807-WA0056.jpg
    63.1 KB · Views: 12
  • IMG-20220807-WA0057.jpg
    IMG-20220807-WA0057.jpg
    94.8 KB · Views: 11
  • IMG-20220807-WA0058.jpg
    IMG-20220807-WA0058.jpg
    69.3 KB · Views: 11
  • IMG-20220807-WA0055.jpg
    IMG-20220807-WA0055.jpg
    61.5 KB · Views: 11
  • IMG-20220807-WA0054.jpg
    IMG-20220807-WA0054.jpg
    81.7 KB · Views: 11
Back
Top Bottom