Ikungi Walipwa Fidia na Jeshi Milioni 243.7

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
IKUNGI WALIPWA FIDIA NA JESHI MILIONI 243.7

Serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa vijiji vya choda na mkiwa wilaya ya Ikungi

Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ta Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amesema Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi 112 wa kijiji cha mkiwa na wananchi 48 wa kijiji cha Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia

Kwa upande wao baadhi ya wananchi ndugu Mayunga Mayunga luhende na Pascal Michael Ghula pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kuwalipa fidia ili wapishe shughuli za kambi ya jeshi katika kata ya mkiwa wamepongeza mchakato wote wa uthamini kuwa wa wazi na wa ukweli

Katika hatua ingine Mhe. Muro pia aliwaomba viongozi wa jeshi wanaosimamia kambi ya mkiwa kutumia busara kwa kuwaruhusu wananchi wamalize kutoa mazao yao ambayo waliyapanda katika mashamba yanayozunguka kambi hiyo kutokana na wao kuandaa na kupanda kabla ya kulipwa fidia ombi lililokubaliwa na msimamizi wa kambi hiyo

Tazama picha za matukio 👇🏾👇🏾

Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ikungi

IMG-20221110-WA0017.jpg
IMG-20221110-WA0015.jpg

IMG-20221110-WA0014.jpg

IMG-20221110-WA0016.jpg
 
hapana ni kama 1,500,000/= kila mtu, very interesting sana na inahuzunisha
Dah kwa kweli hii nchi ni maskini sana jamani
Hiyo ni hela nyingi kwa watu wa kijijini
 
Serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa vijiji vya choda na mkiwa wilaya ya Ikungi

Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ta Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amesema Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi 112 wa kijiji cha mkiwa na wananchi 48 wa kijiji cha Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia

Kwa upande wao baadhi ya wananchi ndugu Mayunga Mayunga luhende na Pascal Michael Ghula pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kuwalipa fidia ili wapishe shughuli za kambi ya jeshi katika kata ya mkiwa wamepongeza mchakato wote wa uthamini kuwa wa wazi na wa ukweli

Katika hatua ingine Mhe. Muro pia aliwaomba viongozi wa jeshi wanaosimamia kambi ya mkiwa kutumia busara kwa kuwaruhusu wananchi wamalize kutoa mazao yao ambayo waliyapanda katika mashamba yanayozunguka kambi hiyo kutokana na wao kuandaa na kupanda kabla ya kulipwa fidia ombi lililokubaliwa na msimamizi wa kambi hiyo

IMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA WILAYA IKUNGI
 
Million 243 kwa watu 160 ni wastani wa 1.5m kwa kila mtu!
Je hayo mashamba yalikuwa na ukubwa gani, yalikuwa miundombinu ya aina gani?
 
Back
Top Bottom