Ila Dar, mnapasifiaga bure tu. Hakuna lolote!

Mkuu uwe na pesa halafu uisha dar….are you fuckin seriously,labda kibada.
Mbweni, Masaki, Bahari beach, makongo juu iliyoungana na goba sehem kibao.. ila namaanisha uwe na pesa utapata access ya Kila kitu me nmefanya kazi apo karibia na Le Grande casino town kabisa wenyewe wanaita Manhattan ya bongo watu wana pesa Mzee acha.

Kuna watu wamepangsha apartment twin towers juu kule Kodi $7000 kwa mwezi tena mbongo huyo utaanzaje mwambia dar pabaya view yake tu prosperity therapy inajitosheleza kwenye parking spaces brabus za kutosha.
 
Niko pamoja na wewe,ila kusema dar sio pazuri ni uongo labda baadhi ya maeneo,japo kwa asilimia kubwa Dar ni pabaya tuache unafki.Japo pesa inaweza kufanya jambo lolote,Swali unaweza kulipa $7,000 per month kisa nyumba?KAMA HUWEZI BADO DAR NI MBAYA KWA SABABU UTAISHI SEHEMU ZENYE KERO TU.
 
Mjini mipango kama bajeti haipo kwenye mipango sioni shida mtu kukukwepa kuja kiwanja ili tu kukufurahisha
 
Mkoa gani mzuri? elezea na uzuri wake
 
Kwa ufupi sioni mkoa wa kuulinganisha na Arusha kwa makazi.
Elezea uzuri wake ukiachana na hali ya hewa, Arsuha haifui dafu hata kwa Mwanza na Mbeya... Nmetembea mikoa karibu yote na me ni mzaliwa wa lake zone naipenda mwanza damuni ila Mbeya kimakazi ni mwisho wa reli. Usije kua unasema kisa tu kwenu huko.
 
Elezea uzuri wake ukiachana na hali ya hewa, Arsuha haifui dafu hata kwa Mwanza na Mbeya... Nmetembea mikoa karibu yote na me ni mzaliwa wa lake zone naipenda mwanza damuni ila Mbeya kimakazi ni mwisho wa reli. Usije kua unasema kisa tu kwenu huko.
Huenda vitu unavyovipenda wewe mimi sivipendi kikubwa wote hatuielewi Dar kimakazi.
 
Kwani kumiliki gari ni ishara ya kuwa na uwezo kifedha?
 
Huwa mnasema wakazi wa dar wapo weak sana ila hayo ni maneno tukija kiuhalisia hali ya maisha ya dar ni lazima uwe strong ili uweze kuishi kitu ambacho wengi wanashindwa. Ni muhimu kutumia nguvu na akili ili uendelee kuishi ndani ya dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…