Ila mambo mengine bwana, sasa kuwalazimisha walimu waandike maazimio ya kazi (schemes of work) kwa mkono ndo nini? Inaongeza ufaulu?

Ila mambo mengine bwana, sasa kuwalazimisha walimu waandike maazimio ya kazi (schemes of work) kwa mkono ndo nini? Inaongeza ufaulu?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Sijawajua vizuri sana viongozi wa kada zingine, lakini nadiriki kusema hawa wanaopanda ngazi na kuwa viongozi wa walimu hubadilika na kuwa na roho ngumu sana!

Katika karne hii ya sayansi na teknolojia, kizazi hiki cha computers ambapo hata vishikwambi vimeanza kufikiriwa kugaiwa kwa kila mwalimu ili kumrahisishia kazi, eti kuna viongozi hawataki kabisa walimu wafaidike na maendeleo haya. Imagine, viongozi eti wanawakataza walimu kuandaa maazimio yao kwa kuyachapa......wanataka waandike kwa mkono tu na si vinginevyo.

Ukiuliza sababu ya hili eti unaaambiwa kumzuia mwalimu 'asikopi' kazi ya mtu mwingine shaaaaabash!!!!!!!! Sasa akiandika kwa mkono hawezi kukopi? Lengo la wazi lililopo hapa ni kuwahangaisha tu walimu. Wanaowasimamia walimu; wakuu wa shule na walimu wakuu hupata tabu zaidi katika hili.

Hivi kufanya hivyo ndo ufaulu unaongezeka? Mbona shule zinazofaulisha vizuri kabisa hawana mambo hayo? Wao mpaka nukuu za masomo zinachapwa na mwalimu mwenyewe. Mambo yanakuwa safi! Mbona matokeo ya Form 2 ni mabovu tu, misifuri kibaaao!! Viongozi, muwe mnawafikiria na wenzenu na madhila yao.....muondoe vikwazo visivyo na ulazima viongozi.

Kwa msiowahi kupitia ualimu:
Azimio la kazi ni mpangokazi wa mwalimu katika kuliendea somo Lake kwa mwaka husika wa masomo sawa na kalenda ya mihula, mada kubwa na ndogo na lini na kwa namna gani zitafundishwa na kwa kutumia Materials gani huelezwa humo.

Hii, kutokana na uwingi wa vipengele vya kujaza na uwingi wa mambo ya kuyajaza humo, huandaliwa katika zile karatasi kubwa maarufu kama za A3. Somo moja, huchukua A3 tano (kwa ,wenye maarifa mazuri ya summarization) au zaidi.

Sasa afisa wewe unajisikia raha gani kumchoresha na kumuandikisha mtu kwa mkono miA3 kumi au zaidi? Ukweli ni kwamba, kwa kuchapa, mambo huwa mazuri kwani vinasomeka safi kabisa......sioni uhusiano wowote wa kuchapa na kukopi.
 
Ni sahihi kabisa fata utaratibu mwalimu acha ujuaji utaumia

Unapoandika kitu kwa mkono wako huwa ni rahisi kukaa kichwani na pia humlazimu mwandishi kijifunza zaidi na kupitia source mbali mbali

Pia humfanya mwalimu kuandika kwa mpangilio mzuri ambao utaeleweka na aina ya wanafunzi wake

Ndugu mwalimu acha uvivu

Amani iwe nawe
 
Wacha tuwauzie ila GPSA wanatabia mbaya sana wanauza vitu bei ya juu ila kukopesha kwa watu wa serikali no ni malipo ndio upate vitu.wakija kwetu wanataka makaratasi ya kukopeshwa wachukue vitu.
 
Nilichogundua miaka yangu ya kuisha hapa nchini kwangu Tanzania ni kwamba viongozi walioko kwenye nafasi zao ni very incompetent na hupenda kuwa rude (wakali na wenye roho mbaya) na hufanya hivyo kama defense mechanism na huona raha sana kuwanyanyasa walio chini yao. Mtu akipewa cheo anafikiri ni wajibu wake kuwanyanyasa walioko chini yake!
 
[emoji1491]Ujumbe mzuri
 
Ni sahihi kabisa fata utaratibu mwalimu acha ujuaji utaumia

Unapoandika kitu kwa mkono wako huwa ni rahisi kukaa kichwani na pia humlazimu mwandishi kijifunza zaidi na kupitia source mbali mbali

Pia humfanya mwalimu kuandika kwa mpangilio mzuri ambao utaeleweka na aina ya wanafunzi wake

Ndugu mwalimu acha uvivu

Amani iwe nawe
We utakuwa afisa taaluma wewe, na sijui kama siyo wa lindi manispaa wewe.

Mi sizungumzii kutoandika, nazungumzia kuandika kwa mashine kwani hakuna utofauti wowote kwakuwa hivyo pia unasoma. Feza na shule zingine kadhaa wanachapa hadi nukuu za somo (notice) kwa wanafunzi; je, wanafeli? Walimu wanapoteza ujuzi?!!! Isitoshe, mbali na azimio, bado kuna mambo kibao mwalimu anahitajika kuyaandika.......andalio la somo, notice n.k.

Acha unoko afisa taaluma!
 
Back
Top Bottom