Ila Polepole kazimishwa vizuri sana

Ila Polepole kazimishwa vizuri sana

Kachuo kake uchwara ka uongozi kamepotelea wapi sijui? Wahenga waliosema "Mbwa mwenye mnofu mdomoni hapigi kelele." Waliona mbali sana.

Siku anaapishwa kwenda kuwa balozi, alipigwa dongo na Rais Samiah, kwamba akae darasani kwanza afundishwe diplomasia halafu akimaliza mafunzo aende akaonane na Rais.
 
Huyu ni mchumia tumbo tu, tokea akane katiba kwamba haina faida maana ni makaratasi tu!! Ndio waTanzania walimdharau sana.

Alipokua Katibu mwenezi alikubali sheria kandamizi za Takwimu na maudhui ya habari n.k kupitishwa. Cha kushangaza sheria hiyo hiyo ikaja kusababisha aitwe TCRA na kipindi kufungiwa.

Usishangae akitumbuliwa atasema katiba ibadilishwe!!
 
Back
Top Bottom