Ila tuwe serious, pesa ndio uhai, pesa ndio afya ya akili

Ila tuwe serious, pesa ndio uhai, pesa ndio afya ya akili

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
Ni kipi kilichowahi kuridhisha nafsi ya mwanadamu?

Ni kipi kilichowahi ponya moyo wa mwanadamu for good?

HAKUNA,

Ila ni kipi kinakupa faraja ya kuendelea ku-survive, ni pesa.

Manung'uniko na msongo ni sehemu ya maisha ila kwa mwenye pesa inakuja bila mwendelezo katika episodes tofauti tofauti ila kwa kapuku ni full season na extra episode🤣

Vijana wanatembea wanaongea wenyewe bara barani, wwngine wanarusha rusha mikono alafu akigundua umemuona anajifanya anaongea na simu, msongo ni mkali maana finance imebana
 
Ushamaliza kila kitu sasa sisi tutoe maon gan acha ujinga bwanamdogo dunia tunapita pesa pesa pesa kitu gan acha upumbavu we mweu kweli.ole wako u reply comment yangu mbavu zako..... Alisikika mlev mmoja akisema
 
Ushamaliza kila kitu sasa sisi tutoe maon gan acha ujinga bwanamdogo dunia tunapita pesa pesa pesa kitu gan acha upumbavu we mweu kweli.ole wako u reply comment yangu mbavu zako..... Alisikika mlev mmoja akisema
😁😁😁
 
Sema nawaonea sana huruma vijana wanaokua wakati huu. Sisi tumekua kwa ku Google, chochote unachotaka kujua una google.

Sasa hizi takataka wanazokutana nazo watoto wakati huu inasikitisha sana, inatisha sana, na kutia kinyaa.

KKinachoshangaza zaidi ni idadi ya waunga mkono! Ni wafuata mkumbo? Watoto wasiojua lolote? Ni wajinga hawana elimu? Au ni waovu tu waliotabiriwa tangu karne?


1) PESA SIO UHAI!

Watoto wa mitaani hawana pesa na wanaishi!

Wagonjwa wa akili na maskini wanaokula majalalani wanaishi!

Watu wenye vipato vya chini wanaishi!

Kwamba ukikosa pesa roho inakata? ?

Wenye mabilioni wanakufa mahospitalini, kwenye ajali wanaacha mabilioni . Mbona pesa imeshindwa kuwafanya waishi? ?

Pesa ni moja ya sanamu, mungu wa uongo:
Unaibudu: kuifanya kipaumbele na kufanya lolote uwezalo kuipata.

Unaisifu:
Unaiona ndiyo chanzo cha Uhai seriously! ! !


2) PESA NDIO AFYA YA AKILI? UONGO!


Hujawahi kuona Sokwe mwenye pesa? ? ? Pesa ipo lakini watu hawatamani kukaa na wewe. Wanakuvumilia wale pesa zako.

Total mental case! Hasira! Ugomvi! Makasiriko! Matusi! Hata uchoyo, ubinafsi. Akitoka ndani anasalimia majirani watafkiri mtu kumbe ni Sokwe mwenye pesa! ! !

PESA SIO AFYA YA AKILI.

Tena nadiriki kusema afya ya akili ya akili ya mtu inaweza kupimwa na mtu anavyo behave aidha akikosa pesa au akiwa nazo anazoziona na nyingi.

Ukiwa huna pesa unageuka kuwa Sokwe: unarukwa na akili, unataka kujiua, unafanya kila aina ya uovu uipate.


Ukizipata nyingi unageuka kuwa Sokwe mwenye suti: unarukwa na akili, unajiona mungu, unafanya kila aina ya uovu kutumia na ku maintain pesa zako.

"Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.

Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Mwenyezi Mungu ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu."

Methali.30.8-9.NENO


3) NI KIPI KILICHOWAHI KUPONYA MOYO WA MWANADAMU FOR GOOD?


Unajibu hakuna!

Usitujibie! ! !

Mioyo yetu wengine imeponywa na MUNGU: mahusiano na YESU ndio yaliyotuponya, wakati tukiwa apeche alolo.

MUNGU amesafisha mioyo yetu kutoka na ubovu wa kila aina, na anaendelea kufanya hivyo.

Tumejifunza kuwa MUNGU ndiye ngome, hata dhoruba gani ije in life tunabaki imara, hatuhitaji daktari wa magonjwa ya akili wala mganga wa kienyeji wala madawa ya kulevya wala pombe wala mahusiano ya kimapenzi.

MUNGU anatupa AMANI ipitayo uelewaji wote. Yani amani ambayo watu wanawaza unawezaje kuwa na amani?

Waabudu pesa wamekuja na mapesa yao kwenye maisha yetu kutuvuruga, kututia najisi na kufanya tu question thamani ya pesa, wamefanya tuidharau pesa.

Matajiri wenye MUNGU ndo wamekuja kutubariki.

Ukishaona mtu ana mapesa na hana MUNGU ndani yake mkimbie mapema sana, maana hivyo vitamu vitakuwa vichungu in zero minutes.


4) NI KIPI KILICHOWAHI KURIDHISHA NAFSI YA MWANADAMU?

Ndomaana mnagongewa nyie waabudu pesa. Hapa hata siongezi neno.


5) KIPI KINAKUPA FARAJA KUENDELEA KU SURVIVE?

Usitujibie
, sio pesa.

Kinachonipa faraja ni:
TUMAINI LA KUISHI MILELE!
TUMAINI LA KUMUONA YESU!

I AM SO ANXIOUS!
I AM SO EXCITED!

I can't wait to meet the LORD and receive my crown from the King himself.

I will sit with him on the same table and eat with him and drink with him.

Hakuna raha nayopata humu duniani kushinda hii HOPE niliyonayo.

My hope is my Pleasure. Eternal Pleasure.


6) TAJIRI HANA MANUNG'UNIKO NA MSONGO WA MUDA MREFU. MASKINI ANAYO YASIOISHA.

Narudia hujawahi kukutana na sokwe mwenye pesa.

Ndo unakuja msemo: bora kulia kwenye gari kuliko kwenye baiskeli, watu wanavumilia misongo mingi ili wavune pesa.

Halafu we jamaa unaamini pesa zikiwepo zipo kila siku. Na zisipokuwepo hazitokuwepo kamwe. Kuna namna pesa imekupa a very false sense of security.

Siku utakayojua pesa zina mabawa, utalia na kusaga meno, na vile thamani yako yote umeiweka kwenye pesa ndo nyie mnaji al shabab!

"Maskini huyu alimwita Mwenyezi Mungu, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote."
Zaburi.34.6.NENO

"Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonesha kujizuia.

Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai.
"
Methali.23.4-5.NENO


7) WATU WANA MISONGO KWASABABU YA HALI NGUMU ZA KIUCHUMI.

Hiki ndo cha pekee cha ukweli umendika, hata chenyewe ni ukweli nusu.

Uchumi umekuwa mgumu dunia nzima, tuko kwenye majira yaliyotabiriwa hali za wengi zitakuwa ngumu.

MUNGU amewapa watu wake namna ya kukabiliana na hali hizi. (Hint: Sio tafuta pesa kwa nguvu zaidi.)

Mwenye pesa anaweza asiwe na msongo kwasababu ya uchumi:

akawa na msongo kwasababu ya ndoa yake,

watoto wake,

afya yake,

dhambi zake (mf. mtu analala na wanaume wenzie huku kajifanya family man mwenye mke na watoto),

nasikia wenye pesa wenyewe saa nyingine hawalali kwa amani maana wanahisi wataondoshwa muda wowote na wanafamilia, wafanyabiashara wenzao, au stress za kumaintain uchumi usishuke: kulala hadi wa boost na vidonge vya usingizi, madawa ya kulevya! !

"Usingizi wa kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo au kingi, lakini wingi wa mali humnyima tajiri usingizi."
Mhubiri.5.12.NENO


8) MUNGU ametuumba turidhike kwa kufanya kazi.


Mtu anayejishugulisha hata kama ana kipato kidogo, hata mama wa nyumbani anayetunza nyumba na mtoto mwenyewe, anaridhika kuliko mtu aliyekaa tu miaka nenda miaka rudi anasikilizia mchongo,

Na Mkaa bure sio sawa na mtembea bure.

"Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake."
Mhubiri.3.22.NENO
 
Back
Top Bottom