Ila uswazi kuna raha jamani

Ila uswazi kuna raha jamani

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Wale wanaoishi mitaa hii tuna maisha yetu dizain flan ivi hayapatikani kokote. Mfano una hela au huna utakula tu japo kwa jirani,huna mke demu utapata tu,unaweza zuga kusonga kaugali kadogo halafu mboga kwa jirani,mipango yote ya chumbani kwa jirani unaisikia bila taabu,hamna CCTV wala nini unapenyeza jicho tu.
Watu wa huko magetini mna raha gani sasa,huku sherehe hazina kadi ni miguu yako tu na pilau unakula.
Sidhani kama ushuani kuna lolote bana.
 
Mkuu japo wengi tumeishi hayo maisha lakini naomba utofautishe kuzoea maisha na maisha matamu. Ni vitu tofauti
Kweli ni tofauti lakini kuwa mkweli tu msamaria hivi huko unaweza kwenda kucheki tv kwa jirani ukiishiwa star times!au kuweka kitoweo kwa jirani luku ikikata?Uswazi ni ujamaa na kutegemeana.
 
Kweli ni tofauti lakini kuwa mkweli tu msamaria hivi huko unaweza kwenda kucheki tv kwa jirani ukiishiwa star times!au kuweka kitoweo kwa jirani luku ikikata?Uswazi ni ujamaa na kutegemeana.

Nimesema ukweli kwamba tumeyaishi hayo maisha, boga inapikwa chumvi unaenda kuomba kwa jirani.

Nnachosisitiza ni kwamba sio maisha ya kiwango stahiki. Hakuna mtu anapenda kuishi hayo maisha kwa sasa ila yanabaki kuwa kumbukumbu mujarab
 
Nimesema ukweli kwamba tumeyaishi hayo maisha, boga inapikwa chumvi unaenda kuomba kwa jirani.

Nnachosisitiza ni kwamba sio maisha ya kiwango stahiki. Hakuna mtu anapenda kuishi hayo maisha kwa sasa ila yanabaki kuwa kumbukumbu mujarab
Lakini mkuu si ndiyo asili yetu?kwa nini tusijikubali tu[emoji16][emoji16]
 
kinachonikera uswazi nikipita na demu mkali watu siwakuti nje kama wanaambizana wasikae nje ila nikipita na demu wa hovyo hovyo watu nyomi
Timing zako mbaya labda,lazima ujue mida ya vibaraza[emoji16]ndo upite nae.
 
Hata kama huna hela muuza vitumnua anajua mpaka mlango wako na mama mwenye nyumba ni shost yake
Yaani huku ukiwa na shughuli hela utoe tu labda kwa kutojichanganya kwako. Dera unapewa au kuazimwa,chakula unapikiwa buuure!
 
Baba mwenye nyumba akishakusanya kodi yake anatoa sofa moja barazani na stool ana kunywa balimi yake taratibu. Akinywea ndani nani anajua?
Na kwanza anywe ndani kwa kumuogopa nani!ukinunua kanga jioni unajianika nayo barazani kwa raha zako.
 
Uswahilin raha huna redio jiran anayo baasi miziki yote utaipatia kwa jirani,kwa siku lazima ugomvi utokee

Matangazo madogo madogo laivu ya wauza dagaa,nyanya chungu,samaki,wapaka rangi,wauza mitumba bila kusahau wauza sumu za wadudu kitu cha kawaida
 
Uswazi full kuchambana,wamama kupigana mpaka wavuane khanga,
Kuibiana nguo kwenye kamba,mkaa jikoni
Hahaa kuombana mboga.
Mtoto wa jirani anakula kuanzia asubuhi mpaka jioni mama yake hana hata habari.

Kutoboleana nyavu za madirisha!
Kujuana undani kuliko hata wewe mwenyewe.

Uswazi sihami ng'oo
 
Uswahikin raha huna redio jiran anayo baasi miziki yote utaipatia kwa jirani,kwa siku lazima ugomvi utokee

Mtangazo madogo madogo laivu ya wauza dagaa,nyanya chungu,samaki,wapaka rangi,wauza mitumba bila kusahau wauza sumu za wadudu kitu cha kawaida
Taarifa ya habari unapata bila kununua redio,mawasiliano yote masikioni mwako!msiba gani utokee usiujue?mpaka kilichomuua marehemu utajulishwa tu. Yule alikuwa na ngoma!
 
Back
Top Bottom